Hivi Kiongozi anaepeleka mtoto wake Shule ya Milioni 10 atatoa Mawazo Gani ya Maana ya kuendeleza shule za Serikali?

RNA

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
1,584
2,683
Katika pitapita zangu nimekutana na video ya Anthon Mtaka akizungumza kuhusu Elimu, hii hapa chini
Your browser is not able to display this video.

Nikaona kaongea ukweli fulani ,Hivi wana JF ,mtu ambae hajawahi somesha mtoto shule ya serikali hasa ya kata anawezaje akawa na mipango ya maana kuhusu hizi shule?
 
Elimu ni power (whatever it is). Japo wengine wanatumia jina la elimu (wanalazimisha pesa ndiyo iwe elimu), kwa lengo la kuhodhi mamlaka.

Lengo la kupump pesa kwenye taasisi hizo za elimu ni kuhakikisha rasimali zote (watawala bora, wataalamu makini, watumishi waadilifu, walimu wabobezi na mahiri, na wafanyakazi wachapazi, plus materials na facilities zote za kisasa) zinamakinikishwa (concentrated) hapo as much as possible!

First-class ya kila item inaenda huko.

Mwalimu gani wa viwango atakubali kwenda kufundisha kwenye shule ya kijijini, mbovu--esp. kama hana uzalendo?

See? The problem is very obvious!

Nyerere alisema vyema kwamba nchi yetu inakabiliwa na maadui ^war-tar-two:^ UJINGA, MARADHI, na UMASKINI. Ujinga ni mama na baba yao, maradhi ni watoto wake identical twins!)
 
Hakuna ubaya kwa wenye uwezo kusomesha watoto wao vizuri. Mzazi mwenye uwezo ana wajibu wa kusomesha wanae vizuri.
Kusomesha vizuri na kusomesha vibaya kupoje?

Umaanisha kwamba shule zisizotoza ada (serikali) zina elimu duni na zile zinazotoza ada kubwa zina elimu bora?
 
Reactions: RNA
Elimu ni suala la jamii, sio mtu mmoja mmoja, elimu ni mali ya jamii, inamilikiwa na wana jamii wenyewe, itawezeshwa na wana jamii wenyewe, si jambo la watawala wala viongozi. Elimu ni silaha dhidi ya ujinga kisha umasikini, elimu lazima igharamiwe, kwa gharama yoyote ile, lazima igharamiwe.
 
Kusomesha vizuri na kusomesha vibaya kupoje?

Umaanisha kwamba shule zisizotoza ada (serikali) zina elimu duni ma zile zunazotoza ada kubwa zina elimu bora?
Tafuta pesa acha mbwembwe.......
 
Hakuna ubaya kwa wenye uwezo kusomesha watoto wao vizuri. Mzazi mwenye uwezo ana wajibu wa kusomesha wanae vizuri.
Ningependa kujua upande wa pili, yani kusomesha vibaya. Halafu mimi, nita 'correlate' na hiyo video hapo juu.
 
Shule za kata ni kutuandaa sisi kuja kuwa walinzi na wauza bar
 
Kusomesha mtoto mahela mengi siyo ubora wa elimu ni ulimbukeni tu na kutaka kujenga social classes hakuna kingine. Ktk matokeo ya form six mwaka huu miongoni mwa shule kumi bora zipo shule za kata mfano Ziba Sekondari iliyoko Mkoa wa Tabora Wilaya ya Igunga, Dareda Sekondari iliyoko Mkoa wa Manyara Wilaya ya Babati.

Wakifika Vyuo vikuu wale waliosoma shule za gharama kubwa wanapigwa mbaya sana na wale waliotoka shule za serikali tena mnazoita za kata. Mi nachoomba serikali mboreshe shule zetu za serikali waache wajinga wachezee pesa zao sana sana wataambulia kujua zaidi lugha ya wakoloni.
 
Kusomesha vizuri na kusomesha vibaya kupoje?

Umaanisha kwamba shule zisizotoza ada (serikali) zina elimu duni ma zile zunazotoza ada kubwa zina elimu bora?
Inawezekana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…