Hivi JK anapokelewaje airport za Marekani na nchi zote za G 8?

swala la mapokezi kwa viongozi wakuu wote, ni itifaki ya kimataifa ambayo inazingatiwa na mataifa wote.. ulinzi anaopata Obama au Bush kwenye nchi za ulimwengu wa 3 sio sawa na anavyokwenda Urussi, au FRANCE, jerumani...unapewa ulinzi na wahusika, sio kama anavyokuja huku na lundo la walinzi..kumbuka hata hapa kwetu kuna wakati wanakuja maraisi JK anakuwa busy, anamtuma makuamu wa rais, au pinda kwenda kumpokea... tofauti na hapo lazima KIongozi au mwenyeji awepo air port kumpokea mwenzake. katika umoja wa mataifa, viongozii wakuu wa ncho wote wana hadhi sawa, haijalishi unatoka katika nchi ndogo au maskini kiasi gani. sema JK anakosa mapokezi mazuri, coz anaenda mno mara kwa mara, mpaka wamemchoka sasa

Hapo mwishoni nimepapenda!
 
Huyu hapa:

IMG_0018.jpg
Hapa kama vile anaingia shopping?
 
Uwanja wa ndege,Rais hupokelewa na ujumbe mfupi wa watu walioandaliwa kumpokea.Si kama hapa ambapo Rais yeyote hupokelewa na Rais wetu.Ujumbe si lazima uwe na Waziri hata mmoja.Pia,walinzi wengi ni wale anaotoka nao huku pamoja na wale wa kutoka Ubalozini(Ubalozi wa pale Marekani nk).Hasa ni Maafisa Usalama.Mapokezi yake ni ya kawaida sana kuliko inavyofikiriwa.Hakuna hata gwaride kama hapa.From my experience...
 
swala la mapokezi kwa viongozi wakuu wote, ni itifaki ya kimataifa ambayo inazingatiwa na mataifa wote.. ulinzi anaopata Obama au Bush kwenye nchi za ulimwengu wa 3 sio sawa na anavyokwenda Urussi, au FRANCE, jerumani...unapewa ulinzi na wahusika, sio kama anavyokuja huku na lundo la walinzi..kumbuka hata hapa kwetu kuna wakati wanakuja maraisi JK anakuwa busy, anamtuma makuamu wa rais, au pinda kwenda kumpokea... tofauti na hapo lazima KIongozi au mwenyeji awepo air port kumpokea mwenzake. katika umoja wa mataifa, viongozii wakuu wa ncho wote wana hadhi sawa, haijalishi unatoka katika nchi ndogo au maskini kiasi gani. sema JK anakosa mapokezi mazuri, coz anaenda mno mara kwa mara, mpaka wamemchoka sasa
Sawa Mkuu... lakini je huwa anapokelewa kwa msafara wa mapikipiki na magari hadi njia zinasimama kwa mda?
Na hapo airport analakiwa na nani? Gavana wa jimbo,meye, au Rais wa nchi? Je imehahi tokea Rais wa Marekani
kwenda airport kumpokea Kikwete?
 
Ni kweli mkuu, wazungu wamemchoka sana JK, ipo siku watamtemea mate usoni...
 
Jibu lako ni rahisi. Hivi Matonya akienda kwa Bakhresa au Mengi anapokelewa na nani? Au tufanye hivi, hivi ukitembelewa na jamaa unayemjua kwa kukupiga mizinga ofisini mwako huwa unafanyaje? Jibu linatosha kwa leo
 
Kwa siku moja kuna zaidi ya Marais 20 wankuwa NYC.......imagine kuruhusu misafara itakuwaje? Anakuwa mtu wa kawaida kule with a few security details

mkuu, kama kuna marais mbau(20) wanaotembelea usa per day basi obama angekuwa hana muda wa kufanya kazi nyingine zaidi ya kuwa busy kuwapokea hao marais. mi kwa muono wangu nadhani pale state department kuna kitengo maalum cha kuwapokea marais and etal hivyo obama halazimiki kwenda viwanja vya ndege kusubiri kuwapokea.
 
Hata mizinga wakati mwingine huwa apigiwi!Mkuu watu huko wako busy na mambo yao ni wapokea wageni kutoka balozi zetu ndiyo kazi yao!
 
Huyu hapa:

IMG_0018.jpg

huyu mzee bana sijui kaweka lisimu mfukoni angalia mfuko wa koti ulivo tepeta kama kaweka jiwe ..yaania nawaza kuchat kwenye fb muda wote tu....mwee jk bwana ...na suruwali sijui inamlegea angalia hapo kwenye zipu .....
 
Kwa kawaida Rais wa Marekani na viongozi wote wa nchi tajiri duniani (G8) wanapowasili Airport ya Bongo
huwa wanapokelewa zaidi ya VIP....yaani ulinzi unakuwa mkali,mapikipiki ya msafara na magari maalumu ya
msafara hadi ikulu na siku hiyo njia zote za katikati ya jiji huwa zinafungwa kwa mda wa masaa kadhaa.

Sasa swali langu ni -:
Je na Rais wetu Kikwete atambeleapo nchi za viongozi hawa huwa anapata the same VIP service? i mean
mapikipiki ya msafara,magari maalumu kuanzia Airport na njia zao kufungwa kwa mda kupisha msafara wake?
Na hapo airport anapokelewa na nani? Gavana wa jimbo,meya,au Rais wa nchi?

Msaada jamani kwa faida yangu na watu wengine.

Marekani ni nchi kubwa sana Duniani, ni nchi inayobeba vikao muhimu ya kibiashara, ulinzi na uchumi wa dunia hii. Kwa siku moja nchi hii hupokea viongozi Wakuu wa nchi mbali mbali wasiopungua ishirini na tano.
Kama Serikali ya Marekani itaamua kuweka itifaki ya kuwapokea viongozi Wakuu wa nchi wanakwenda kwao kwa itifaki kama zifanyavyo nchi nyingine, basi shughuli za maisha ya watu waishio ktk miji hiyo zitasimama.

Suala la itifaki hupangwa na nchi husika kutokana na vile waonavyo kwao ni sahihi.

Baada ya mchango wangu huu, naomba kujua kutoka kwa mtoa hoja, je, kujua mapokezi ya Rais wetu nchini Marekani kunatusaidia nini watanzania? Nikielimishwa vizuri juu ya hili utanisaidia kuchangia zaidi.
 
Sawa Mkuu... lakini je huwa anapokelewa kwa msafara wa mapikipiki na magari hadi njia zinasimama kwa mda?
Na hapo airport analakiwa na nani? Gavana wa jimbo,meye, au Rais wa nchi? Je imehahi tokea Rais wa Marekani
kwenda airport kumpokea Kikwete?

mshikachuma,
obama hajawahi kumpokea jk airport hata siku moja. marais wote wanaotembelea usa km wana appointment ya kukutana na obm huwa ni kwenda ikulu ambapo kama ni mgeni rasmi wa obm ndo huwa anapokelewa rasmi pale. sio uwanja wa ndege.
 
Kwa kawaida Rais wa Marekani na viongozi wote wa nchi tajiri duniani (G8) wanapowasili Airport ya Bongo
huwa wanapokelewa zaidi ya VIP....yaani ulinzi unakuwa mkali,mapikipiki ya msafara na magari maalumu ya
msafara hadi ikulu na siku hiyo njia zote za katikati ya jiji huwa zinafungwa kwa mda wa masaa kadhaa.

Sasa swali langu ni -:
Je na Rais wetu Kikwete atambeleapo nchi za viongozi hawa huwa anapata the same VIP service? i mean
mapikipiki ya msafara,magari maalumu kuanzia Airport na njia zao kufungwa kwa mda kupisha msafara wake?
Na hapo airport anapokelewa na nani? Gavana wa jimbo,meya,au Rais wa nchi?

Msaada jamani kwa faida yangu na watu wengine.

Kuna ujio wa Urais wa aina nyingi, binafsi, ziara ya Kitaifa, ziara ya kikazi, ziara ya kuhudhuria mkutano? ndio maana utaona zingine zina mizinga zingine hazina. Hutegemea na safari yenyewe.
 
mkuu, kama kuna marais mbau(20) wanaotembelea usa per day basi obama angekuwa hana muda wa kufanya kazi nyingine zaidi ya kuwa busy kuwapokea hao marais. mi kwa muono wangu nadhani pale state department kuna kitengo maalum cha kuwapokea marais and etal hivyo obama halazimiki kwenda viwanja vya ndege kusubiri kuwapokea.

Sio viongozi wote wanaokwenda Marekani huenda kwa Rais Obama. Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa yapo Marekani. Ofisi Kuu za Benki ya Dunua zipo Marekani. Ofisi Kuu za Shirika la Fedha Duniani zipo Marekani, just a few to mention.
 
Mapokezi ya rais kutoka katika nchi zinazoendelea kama Tanzania huwa wanamapokezi ya aina mbili:

  1. Kama amealikwa na kiongozi mkuu wa nchi hiyo, airport hupokewa wa gavana wa jiji atakapofikia wakiongozwa na msafara wa mapikipiki kama kawaida na mwenyeji wake humsubiri ikulu ambako hupata heshima za mkuu wa nchi na kupigiwa mizinga 21.
  2. Kama amekwenda kwa ziara binafsi au katika mikutano ya mashirika ya kimataifa kama Umoja wa Mataifa hupokewa na viongozi wa mashirika husika na huweza kupangiwa ratiba ya kwenda kumsalimu kiongozi mkuu (Courtesy call) wa nchi aliyoitembelea kama atakuwepo nchini kwake
 
watu wa itifaki mambo ya nje watatusaidia zaidi; nijuavyo mimi kuna ziara za aina mbili
1: state visit- katika nchi nyingi kama hapa kwetu, ziara kama hizi zina vikolombwezo vingi kama ulivyovitaja; kaqma kukagua gwaride la kijeshi; mizinga 21 na dhifa ya kitaifa; lakini kupokelewa na Rais mwenzie inategemea taratibu za itifaki za nchi husika; Marekani Rais wao humpokea mkuu wa nchi pale pale kwenye viwanja vya White house siku inayofuata ujio wake na wala sio uwanja wa ndege.
2: ziara za kawaida: kama kuhudhuria mikutano katika nchi mbali mbali; misafara huwa ni ya kawaida ya kiusalama zaidi mbwembwe nyingine huwa hakuna na kama atakuwa na appointment na Rais wa nchi husika basi hakuna mbwembwe za ziada ukiondoa zile za kiusalama na itifaki lazima izingatiwe. wataalamu zaidi watakuongezea hapo
 
Marekani ni nchi kubwa sana Duniani, ni nchi inayobeba vikao muhimu ya kibiashara, ulinzi na uchumi wa dunia hii. Kwa siku moja nchi hii hupokea viongozi Wakuu wa nchi mbali mbali wasiopungua ishirini na tano.
Kama Serikali ya Marekani itaamua kuweka itifaki ya kuwapokea viongozi Wakuu wa nchi wanakwenda kwao kwa itifaki kama zifanyavyo nchi nyingine, basi shughuli za maisha ya watu waishio ktk miji hiyo zitasimama.

Suala la itifaki hupangwa na nchi husika kutokana na vile waonavyo kwao ni sahihi.

Baada ya mchango wangu huu, naomba kujua kutoka kwa mtoa hoja, je, kujua mapokezi ya Rais wetu nchini Marekani kunatusaidia nini watanzania? Nikielimishwa vizuri juu ya hili utanisaidia kuchangia zaidi.
Mkuu,hapo kwenye bold jibu ni simple tu....kwanza nilitaka tu kujuwa hawa viongozi wa nchi za Africa wanapokelewa vipi
waendapo kwenye hizo nchi tajiri duniani,pili huwa ninajiuliza why Raisi wetu anakwenda USA mara kwa mara? So nikafiki
ria labda kinachompeleka huko ni mapokezi ya ki VIP kama kufungwa barabara,mapikipiki,magwaride,mizinga na misafara
ya magari hadi ikulu ya white house. Lakini kupitia uzi huu kunakitu naanza kujifunza...tuendelee mkuu
 
Back
Top Bottom