Gari siyo hitaji la lazima!Hata kavitz kanakushinda?
Jamani leo naona jirani yangu niliyezoea kumuomba 'lift',
nadhani huenda baada ya 'kunichoka' kutokana na katabia
kangu ka kumuomba lifti wakati wa kwenda kazini.
Huenda aliamua kunitolea uvivu, au pengine nilikuwa namboa, au pengine
kwa mtazamo wake, anadhani ninao uwezo au labda ni ubahili
wangu.......hata sijui why....ila kifupi mara baada ya kupanda, akionekana
hana furaha, neno lake la kwanza likawa 'Hivi jirani kwa nini hununui
gari likusaidie usafiri wa kwenda na kurudi ofisini? Abiria wengine wawili walokuwa
ndani ya gari walibaki kuangaliana tu, maana nao kama wasaidiwa
huenda walihis hilo 'dongo' linawahusu pia
Kwa kuhisi huenda jamaa kanichoka, nililoweza kufanya ni
kuguna tu, mhhhhhh bila kujibu kitu huku nikiwa na aibu tele usoni.
Baada ya kwenda kama mita 70 hivi, nikajidai nimesahau simu na kumuomba jamaa
anishushe niirudie simu yangu nyumbani. Baada ya kushuka
nikapanda zangu daladala na kuelekea job.
Hapa kazini hii stori imekuwa gumzo kwani abiria wale wengine waliifikisha
hii skendo ofisini na imekuwa gumzo la siku. Kila mtu 'ananitania' kwa kurudia
kauli ya mshikaji, 'Hivi jirani kwa nini hununui gari'? Nabaki nacheka tu hapa
ofisini!
Hapa kazini hii stori imekuwa gumzo kwani abiria wale wengine waliifikisha
hii skendo ofisini na imekuwa gumzo la siku. Kila mtu 'ananitania' kwa kurudia
kauli ya mshikaji, 'Hivi jirani kwa nini hununui gari'? Nabaki nacheka tu hapa
ofisini!
Ila swali linabaki pale pale ''hivi jirani kwa nini hununui gari''?? au mipango haijakaa sawa kwasasa??
Ujumbe ulifika the very moment ulipotolewa, na ndiyo maana nilishuka aisee. I felt humiliated to the maximum!Hii mada pia ni ya hapa MMU!!! Anyway, kwa kuwa umeposti hapa ngoja tuchangie! Kwa kifupi jamaa inaonekana kachoshwa na tabia yako ya kuomba lifti, so anauliza indirectly kukupa meseji tu kuwa kachoka.
Kimtazamo si tabia njema aliyoionyesha, maana kila mtu ana priorities zake katika maisha na pia kununua gari kunategemea na other factors ukiacha hizo priorities kama uwezo nk.
Ni vizuri kupanda kidala dala na kuachana na lifti yake, itakutesa kisaikolojia.
Hii mada pia ni ya hapa MMU!!! Anyway, kwa kuwa umeposti hapa ngoja tuchangie! Kwa kifupi jamaa inaonekana kachoshwa na tabia yako ya kuomba lifti, so anauliza indirectly kukupa meseji tu kuwa kachoka.
Kimtazamo si tabia njema aliyoionyesha, maana kila mtu ana priorities zake katika maisha na pia kununua gari kunategemea na other factors ukiacha hizo priorities kama uwezo nk.
Ni vizuri kupanda kidala dala na kuachana na lifti yake, itakutesa kisaikolojia.
huwezi kununua gari kwa sababu tu jirani amesema, ila pale mambo yako yatakapokaa shwari...
pia kutokuwa na gari haina maana daily unadandia lifti, mtu akose hata privacy, kama ana kinyumba ndogo chake ashindwe kukipitia kuogopa jirani atamuona.
au unaishi nyumba ya kupanga ya bei ghalii? ndo maana jirani kashangaa unalipa kodi kubwa halafu kutwa kwenye magari ya watu?
ila chukulia hiyo kama challange...
jipange
uwiiiii! jirani kweli kakuchoka mkuu!
alikuwa nakuhesabia tu unavyocut down expenses zako hata wese huchangii teh!
swali la ziada, umepanda io lift kwa muda gan mkuu?? hehehe usiniambie mwaka duuh!
Aisee kwa kweli ni dalili ya kushoshwa na kuomba kwako lift,
Lakini huyo nae anadhani gari ni kipaumbele kwa kila mmoja,
Naamini ni limbukeni wa magari maana hata kama angekupa lift mwaka mzima bado alitakiwa kujua kuwa kila kitu kinafanyika kwa mipango.
Kwa kifupi huyo bwana amekosa Busara na zaidi inawezekana hana maarifa.
Pole sana Mkuu.