Semilong
JF-Expert Member
- Mar 5, 2009
- 1,712
- 219
NAIBU Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Lazaro Nyalandu, amesema sehemu kubwa ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi, wamekua walalamikaji tu kuhusu taratibu za uwekezaji, lakini hawachukui hatua.
"Watanzania waache kulalamika tu kwenye mablog. Wengi wamekuwa walalamikaji tu, lakini hawachukui hatua," alisema Nyalandu.
.jibu lake hili hapaKwa upande wake, Ndunguru aliishauri serikali iangalie na kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali za uwekezaji ukiwemo mlolongo mrefu kuhusu mchakato wa uwekezaji.
Alisema mchakato wa uwekezaji n chini ni mrefu, jambo linalowafanya Watanzania wengi walioko nje, wakate tamaa, na kwamba hiyo inachangiwa na tatizo la kutakiwa kutumia muda mrefu katika kumilisha taratibu za uwekezaji.
"Tataratibu zetu bado ni ngumu, maana mtu anatumia muda mrefu na gharama na kubwa, jambo linalowakatisha tamaa Watanzania wengi kuja kuwekeza nyumbani," alisisitiza.
baada ya kuwakandia watu wanalalamika tu, na ndunguru nae akalalamika sijui jamaa alijisikiaje