Hivi haya madai ya waziri Nyalandu dhidi ya Wabongo waishio ughaibuni yamekaaje?

Kinyasi

Member
Nov 22, 2010
72
31
Wandugu,
Kama ilivyo ada yangu kuyapitia magazeti ya bongo, nimekutana na hii habari ya Mhe. Nyalandu, Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko akimpongeza ndugu John Nduguru mfanyabiashara wa KiTz aishie Marekani aliyeamua kuja kuwekeza bongo kwenye biashara ya usafirishaji kwa njia ya anga. Pamoja na kumpongeza ndugu J. Nduguru, Mhe. Nyalandu amewaponda WaTz waishio ughaibuni kwamba ni WALALAMISHI na wanapenda kupiga MAJUNGU kwenye mitandao ya Internet badala ya kusaka fursa za uwekezaji nyumbani. Je kuna ukweli kiasi gani kwenye hayo madai yake?

Nawasilisha!

Nyalandu: Watanzania wa nje walalamikaji

Sunday, 12 December 2010

James Magai

NAIBU Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Lazaro Nyalandu, amesema sehemu kubwa ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi, wamekua walalamikaji tu kuhusu taratibu za uwekezaji, lakini hawachukui hatua.

Nyalandu alitoa kauli hiyo wiki iliyopita, wakati akizungumza na Mwananchi baada ya kuzindua Kampuni ya Ndege ya Bold Air, inayomilikiwa na , John Ndunguru, Mtanzania anayeishi Marekani.

Uzinduzi wa kampuni hiyo, ulifanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

"Watanzania waache kulalamika tu kwenye mablog. Wengi wamekuwa walalamikaji tu, lakini hawachukui hatua," alisema Nyalandu.

Naibu wazkiri huyo aliwataka Watanzania hao, watumie muda wa kukaa kwenye mitandao, kuangalia taarifa zinazohusu fursa za uwekezaji zinazopatikana pia hata kwenye mtandao wa Kituo cha Uwekezaji cha Tanzania na kusaidia shughuli za uwekezaji hapa nchini.

"Kitendo cha kulalamika bila ya kuchukua hatua ni ishara kwamba wengi wao sio wabunifu. Nampongeza ndugu yangu John Nduguru, kwa kutumia fursa hiyo na kuanzisha kampuni hii," alisema.

Nyalandu alimpongeza Ndunguru kwa uamuzi wa kuja kuwekeza nyumbani, jambo ambalo alisema litasaidia katika kuinua uchumi wa Tanzania.

"Pamoja na kwamba Ndunguru amekuwa akifanya biasharas zake nchini Marekani, lakini ameiona umuhimu wa kuwekeza nyumbani jambo ambalo litasaidia kuinua uchumi na kutengeza ajira kwa Watanzania wenzake," alisema Naibu waziri.

Kwa upande wake, Ndunguru aliishauri serikali iangalie na kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali za uwekezaji ukiwemo mlolongo mrefu kuhusu mchakato wa uwekezaji.

Alisema mchakato wa uwekezaji n chini ni mrefu, jambo linalowafanya Watanzania wengi walioko nje, wakate tamaa, na kwamba hiyo inachangiwa na tatizo la kutakiwa kutumia muda mrefu katika kumilisha taratibu za uwekezaji.

"Tataratibu zetu bado ni ngumu, maana mtu anatumia muda mrefu na gharama na kubwa, jambo linalowakatisha tamaa Watanzania wengi kuja kuwekeza nyumbani," alisisitiza.

Alisema ameamua kuwekeza katika usafiri wa anga kwa kuwa kuna nafasi nyingi za kufanya biashara na kwamba wakati umefika kwa watanzania, kuachana dhana kwamba huduma ya usafiri wa ndege ni ya watu maalum tu na wenye fedha nyingi.

"Zamani biashara hii ilitawaliwa na Wahindi na Waarabu ambao walitujengea hisia na dhana kwamba huduma hiyo ni ya gharama kubwa sana na kwa hiyo ni ya watu maalumu tu. Hii si kweli, hata Mtanzania wa kawaida anaweza kumudu gharama za usafiri huu," alisema.

Kwa upande wake, Nyalandu alisema ni azma ya Serikali ya Awamu ya Nne, kuwaandalia Watanzania mazingira bora ya uwekezaji kama ambavyo imekuwa ikifanya, ili kila Mtanzania aliyeko nje na mwenye uwezo wa kuwekeza, aje kufanya hivyo.

Alisema kwa sasa serikali iko katika mchakato wa kuangalia mfumo mzima wa kodi za uwekezaji, ikiwa ni hatua ya kuboreesha zaidi mazingira ya uwekezaji, ili kuwavutia wawekezaji wengi wakiwemo wazawa.

Kampuni hiyo ya Bold imeingiza ndege mbili kwenye soko, moja ikiwa ni ya aina ya Cessna 310 na nyingine aina ya Seneca 1, zote zikiwa na uwezo wa kuchukua abiria sita kila moja kwa wakati mmoja.
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
90,739
104,908
Hivi huyu jamaa soo lake la kumbaka msichana wa ki Namibia kule Waldorf College liliishaje?
 

Kinyasi

Member
Nov 22, 2010
72
31
Ndugu Kevin Ambrose,
Mbona unatoka nje ya mada? si uchangie kwenye kauli yake juu ya Wabongo waishio ughaibuni kukosa ubunifu na kubaki kulalamika kuliko kuanza kuchafua hali ya hewa. Ishu ya ubakaji haihusiani kabisa na suala hili, ni afadhali ukaanzisha mada yake inayojitegemea.
 

Kinyasi

Member
Nov 22, 2010
72
31
Hivi huyu jamaa soo lake la kumbaka msichana wa ki Namibia kule Waldorf College liliishaje?

Ndugu Kevin Ambrose,
Mbona unatoka nje ya mada? si uchangie kwenye kauli yake juu ya Waongo waishio ughaibuni kukosa ubunifu na kubakli kulalamika. kuliko kuanza kuchafua hali ya hewa. Ishu ya ubakaji hakihsiani kabisa na suala hili, ni afadhali uakianzaishia mada yake inayojitegemea.
 

Masauni

JF-Expert Member
Aug 15, 2010
386
57
Hivi huyu jamaa soo lake la kumbaka msichana wa ki Namibia kule Waldorf College liliishaje?
Jamani mimi namfahamu sana nyarandu ni mtu wa hovyo sana!! anapenda sana wanawake lakini anajificha chini ya mwamvuli wa ulokole, ni mtu anayependa sifa na kujiinua sana. Kuhusu swala la watz walioko nje anasema upuuzi tu. Mtz ukitaka kwenda kuwekeza nyumbani watakusumbua sana sana lakini lakini asiye mtz huyo ndo wanaona ni mwekezaji kweli. Bongo upuuzi mtupu
 

Tom

JF-Expert Member
May 14, 2007
470
20
Hapo waziri mwenewe analalamikia watanzania wanoishi nje (hataki walalamikie mapungufu ya waziri) - Aache kulalamika lalamika badala yake kama waziri afanye kazi yake kwa ufanisi ili wanaopenda kuwekeza TZ wapate imani.
 

Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
9,503
9,923
WATANZANIA bwana,bingwa kushabikia udaku badala ya maendeleo. Hapa tunazungumzia uwekezaji wewe unatumbukiza"UBAKAJI"
 

andrewk

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
3,102
484
Jamani mimi namfahamu sana nyarandu ni mtu wa hovyo sana!! anapenda sana wanawake lakini anajificha chini ya mwamvuli wa ulokole, ni mtu anayependa sifa na kujiinua sana. Kuhusu swala la watz walioko nje anasema upuuzi tu. Mtz ukitaka kwenda kuwekeza nyumbani watakusumbua sana sana lakini lakini asiye mtz huyo ndo wanaona ni mwekezaji kweli. Bongo upuuzi mtupu

na hasa ukiwa sio mwa CCM hupati ushirikiano kabisaaaaaaaaa, siasa kwanza uchumi baade
 

Mbaha

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
697
73
"Zamani biashara hii ilitawaliwa na Wahindi na Waarabu ambao walitujengea hisia na dhana kwamba huduma hiyo ni ya gharama kubwa sana na kwa hiyo ni ya watu maalumu tu. Hii si kweli, hata Mtanzania wa kawaida anaweza kumudu gharama za usafiri huu," alisema.

Huyu ana laana sijui ya nani??!!! Hivi kweli watanzania wa kawaida tokalini tukaweza kumudu gharama za usafiri wa ndege???!! Kwa maisha gani bora kwa kila mtanzania waliyotuletea????!!! Imbecile!!!
 

Kicheruka

JF-Expert Member
Feb 2, 2009
792
93
Kuwekeza Tanzania bado ni changa moto kubwa kwani urasimu,rushwa, lobbing bado ni mkubwa mno. Kama wanataka wawekezaji genuine wakae wao kama mawaziri na kuondoe vikwazo kwa wawekezaji
 

BRUCE LEE

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
2,097
1,325
na hizo ndege zinafanya safari za kwenda wapi? Na pia zina ma agent katika nchi au mikoa ipi? Na gharama za usafiri zikoje? Ni vizuri wakatujuza. Yangu ni hayo tu
 
Jan 7, 2010
20
0
Jamani mimi namfahamu sana nyarandu ni mtu wa hovyo sana!! anapenda sana wanawake lakini anajificha chini ya mwamvuli wa ulokole, ni mtu anayependa sifa na kujiinua sana. Kuhusu swala la watz walioko nje anasema upuuzi tu. Mtz ukitaka kwenda kuwekeza nyumbani watakusumbua sana sana lakini lakini asiye mtz huyo ndo wanaona ni mwekezaji kweli. Bongo upuuzi mtupu
Jamani i know nyalandu ni mtu anyependa kuonekana kafanya through media but in real sense hana lolote.Ni fisadi sana sana na kweli wa madem but also fedha anajificha kwenye mwamvuli wa ulokole ki ukweli hana lolote.Yaan sijui huko wizarani itakuaje watalipa sana vikao hewa vya hotelini kwa ajili yake atakavyo kuwa anaenda kulala na wadada akaja kuclaim wizarani
 

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,437
Nasikia huyu jamaa aliishi Marekani kwa Muda Mrefu, Je katika Kipindi cha kuishi kwake Marekani alishawahi kufanya Uwekaji wowote au na yeye alikuwa mlalamikaji kwenye Blog mpaka akaja kuwekeza Kwenye Ubunge?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom