Hivi haya madai ya waziri Nyalandu dhidi ya Wabongo waishio ughaibuni yamekaaje?

wana blogu waishio nje ya nchi hawana lolote zaidi ya kujaza ma page ya discussions za matatizo ya Tanzania. Utakosoaje mapungufu yetu wakati we ulishayakimbia?

Na wana blogu waishio ndani wana nini? Mbona kila siku wanajaza makurasa kwa kulialia kuhusu rumba lilivyo kali....mara ooh mgao wa umeme...mara maji hakuna...mara mvua zimenyesha na kuleta madimbwi na matope....wangekuwa na lolote wangekuwa washafanya ya maana...

basi hata kama ni kupiga domo mpigie domo ya maana, wapi, kazi kujadili jinsi ya kuongoza urefu wa sehemu za siri, ndo mada zetu humu kutwa

Kwa taarifa yako idadi kubwa ya wapiga domo wa ngono na uzinzi wako Tanzania. Angalia ni mida gani ambapo jukwaa la "mapenzi" ndo huchanganya....ni ile mida ambayo watu bongo wako maofisini!!!!!!!!! Ishafika saa kumi na moja jioni na kwenda mbele linaanza kupooza tena. Acha zako hizo wewe....kutwa nzima mijitu inashinda inazungumzia "infidelity" na pombe na vikao vya baa. Cha kuchekesha zaidi ni kwamba wao wenyewe hudai eti jukwaa lile ni "stress" reliever....mweeee hilo Taifa wanalijenga saa ngapi?
 
Na wana blogu waishio ndani wana nini? Mbona kila siku wanajaza makurasa kwa kulialia kuhusu rumba lilivyo kali....mara ooh mgao wa umeme...mara maji hakuna...mara mvua zimenyesha na kuleta madimbwi na matope....wangekuwa na lolote wangekuwa washafanya ya maana...
wana moral legitimacy ya kulalamika kwa sababu wako humu humu kwenye madimbwi ya mvua na kukatika umeme na maji, wewe umekimbia

waliopo hapa wanavyolalamikia TANESCO na DAWASCO ndio wanawatia pressure wahusika, citizen outrage, and above all, they go to vote, kitu kinachowatisha wahusika na kujenga hiyo miundombinu

wewe umekimbia!

...kutwa nzima mijitu inashinda inazungumzia "infidelity" na pombe na vikao vya baa. Cha kuchekesha zaidi ni kwamba wao wenyewe hudai eti jukwaa lile ni "stress" reliever...
ndio mainstay ya hili jamvi, utahakiki vipi kama ni bikra ya kweli au ya kuchakachua, tigo, ku boost urefu wa uume, dream ya kumega Jimama lenye watoto watatu, Kumega Mama Mkwe, na dem wangu anapiga sana kelele. Ndio chambuzi zetu for the most part.

Na siasa za wanavijiji, ambao mara ya mwisho kuiona vijiji miaka ishirini ishapita

mweeee hilo Taifa wanalijenga saa ngapi?
na wewe hili Taifa utalijenga lini wakati ushakimbia?

Waziri Nyalandu is right, the diaspora class is but noise pollution not worth a penny

He went to Waldorf College for two years, so what, he came the heck back and used that modest education, is a minister now, changing the world of the country of his nativity, and what the heck are u, a social security no. with bad credit waiting for Lady Gaga on Late Show at the end of the day and a tax refund at end of the year. Mtatusaidia nini
 
wana moral legitimacy ya kulalamika kwa sababu wako humu humu kwenye madimbwi ya mvua na kukatika umeme na maji, wewe umekimbia

Acha kubahatisha. Hujui nilipo. Halafu nani kakupa mamlaka ya kuamua nani ana "moral legitimacy" na nani hana?

waliopo hapa wanavyolalamikia TANESCO na DAWASCO ndio wanawatia pressure wahusika, citizen outrage, and above all, they go to vote, kitu kinachowatisha wahusika na kujenga hiyo miundombinu

Yaani hao Tanesco na Dawasco hawajui wajibu hao hadi waje JF kusoma mashinikizo ya wanazi wa ngono? Ndo maana tumelosti....lol.

wewe umekimbia!

Thibitisha.

ndio mainstay ya hili jamvi, utahakiki vipi kama ni bikra ya kweli au ya kuchakachua, tigo, ku boost urefu wa uume, dream ya kumega Jimama lenye watoto watatu, Kumega Mama Mkwe, na dem wangu anapiga sana kelele. Ndio chambuzi zetu for the most part

"Zetu"....safi sana.

Na siasa za wanavijiji, ambao mara ya mwisho kuiona vijiji miaka ishirini ishapita

Sijui hayo umejuaje....

na wewe hili Taifa utalijenga lini wakati ushakimbia?

Hayo ya kukimbia umeyatoa wapi? Na John Ndunguru katokea wapi vile?

Waziri Nyalandu is right, the diaspora class is but noise pollution not worth a penny

That includes Mr. Ndunguru and others like him, right?

He went to Waldorf College for two years, so what, he came the heck back and used that modest education, is a minister now, changing the world of the country of his nativity, and what the heck are u, a social security no. with bad credit waiting for Lady Gaga on Late Show at the end of the day and a tax refund at end of the year. Mtatusaidia nini

Yeah...he came back but do you know what he left behind? Ask him about that Namibian girl. Ask him about a guy named Tashi who wanted to eff him up at Wartburg?
 
Nasikia huyu jamaa aliishi Marekani kwa Muda Mrefu, Je katika Kipindi cha kuishi kwake Marekani alishawahi kufanya Uwekaji wowote au na yeye alikuwa mlalamikaji kwenye Blog mpaka akaja kuwekeza Kwenye Ubunge?

Mkuu ukiwa mwanasisasa na unatakiwa kuongea kitu unaongea tu. Uwekezaji Tanzania unakatisha tamaa ndio maana nchi yetu haina wawekezaji wa kutosha, huyo jamaa aliyewekeza anatakiwa kupongezwa, kwa kuwa anatafuta maslahi yake na anawasaidia watanzania wenzake. Lakini awe tayari kutoa rushwa, kusumbuliwa na awe tayari kutafuta njia mbadala baada ya biashara yake kusumbuliwa.

Lakini swali, yeye mh waziri aliwekeza wapi alipokuwa huko US? Hakulalamikia uozo? Hakuna ubaya ya kumfahamu vizuri mtu anayesema kitu fulani. So hata kama alibaka tunastahili kujua pia ili tujue sincerity ya anayosema, inawezekana ndio yale ya kusema kwa media tu lakini yaliyopo moyoni mwako ni madudu matupu.
 
wandugu,
kama ilivyo ada yangu kuyapitia magazeti ya bongo, nimekutana na hii habari ya mhe. Nyalandu, waziri wa viwanda, biashara na masoko akimpongeza ndugu john nduguru mfanyabiashara wa kitz aishie marekani aliyeamua kuja kuwekeza bongo kwenye biashara ya usafirishaji kwa njia ya anga. Pamoja na kumpongeza ndugu j. Nduguru, mhe. Nyalandu amewaponda watz waishio ughaibuni kwamba ni walalamishi na wanapenda kupiga majungu kwenye mitandao ya internet badala ya kusaka fursa za uwekezaji nyumbani. Je kuna ukweli kiasi gani kwenye hayo madai yake?

Nawasilisha!

Nyalandu: Watanzania wa nje walalamikaji

sunday, 12 december 2010

james magai

naibu waziri wa viwanda, biashara na masoko, lazaro nyalandu, amesema sehemu kubwa ya watanzania wanaoishi nje ya nchi, wamekua walalamikaji tu kuhusu taratibu za uwekezaji, lakini hawachukui hatua.

nyalandu alitoa kauli hiyo wiki iliyopita, wakati akizungumza na mwananchi baada ya kuzindua kampuni ya ndege ya bold air, inayomilikiwa na , john ndunguru, mtanzania anayeishi marekani.

uzinduzi wa kampuni hiyo, ulifanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere, jijini dar es salaam.

“watanzania waache kulalamika tu kwenye mablog. Wengi wamekuwa walalamikaji tu, lakini hawachukui hatua,” alisema nyalandu.

naibu wazkiri huyo aliwataka watanzania hao, watumie muda wa kukaa kwenye mitandao, kuangalia taarifa zinazohusu fursa za uwekezaji zinazopatikana pia hata kwenye mtandao wa kituo cha uwekezaji cha tanzania na kusaidia shughuli za uwekezaji hapa nchini.

“kitendo cha kulalamika bila ya kuchukua hatua ni ishara kwamba wengi wao sio wabunifu. Nampongeza ndugu yangu john nduguru, kwa kutumia fursa hiyo na kuanzisha kampuni hii,” alisema.

nyalandu alimpongeza ndunguru kwa uamuzi wa kuja kuwekeza nyumbani, jambo ambalo alisema litasaidia katika kuinua uchumi wa tanzania.

"pamoja na kwamba ndunguru amekuwa akifanya biasharas zake nchini marekani, lakini ameiona umuhimu wa kuwekeza nyumbani jambo ambalo litasaidia kuinua uchumi na kutengeza ajira kwa watanzania wenzake," alisema naibu waziri.

Kwa upande wake, ndunguru aliishauri serikali iangalie na kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali za uwekezaji ukiwemo mlolongo mrefu kuhusu mchakato wa uwekezaji.

Alisema mchakato wa uwekezaji n chini ni mrefu, jambo linalowafanya watanzania wengi walioko nje, wakate tamaa, na kwamba hiyo inachangiwa na tatizo la kutakiwa kutumia muda mrefu katika kumilisha taratibu za uwekezaji.

“tataratibu zetu bado ni ngumu, maana mtu anatumia muda mrefu na gharama na kubwa, jambo linalowakatisha tamaa watanzania wengi kuja kuwekeza nyumbani," alisisitiza.

Alisema ameamua kuwekeza katika usafiri wa anga kwa kuwa kuna nafasi nyingi za kufanya biashara na kwamba wakati umefika kwa watanzania, kuachana dhana kwamba huduma ya usafiri wa ndege ni ya watu maalum tu na wenye fedha nyingi.

“zamani biashara hii ilitawaliwa na wahindi na waarabu ambao walitujengea hisia na dhana kwamba huduma hiyo ni ya gharama kubwa sana na kwa hiyo ni ya watu maalumu tu. Hii si kweli, hata mtanzania wa kawaida anaweza kumudu gharama za usafiri huu,” alisema.

Kwa upande wake, nyalandu alisema ni azma ya serikali ya awamu ya nne, kuwaandalia watanzania mazingira bora ya uwekezaji kama ambavyo imekuwa ikifanya, ili kila mtanzania aliyeko nje na mwenye uwezo wa kuwekeza, aje kufanya hivyo.

Alisema kwa sasa serikali iko katika mchakato wa kuangalia mfumo mzima wa kodi za uwekezaji, ikiwa ni hatua ya kuboreesha zaidi mazingira ya uwekezaji, ili kuwavutia wawekezaji wengi wakiwemo wazawa.

Kampuni hiyo ya bold imeingiza ndege mbili kwenye soko, moja ikiwa ni ya aina ya cessna 310 na nyingine aina ya seneca 1, zote zikiwa na uwezo wa kuchukua abiria sita kila moja kwa wakati mmoja.
aondoe kwanza nyumba za tembe kwenye jimbo lake ndio alete mada kama hii hapa ..
 
Hoja yake ipo juu ya kulalamika katika Blogs; nadhani ndio kitu cha msingi hapa siyo kuwekeza, maana sidhani hata kama serikali ina data za nani yupo wapi na anafanya nini na alienda vipi huko, amabacho ni msingi mkubwa wa kuwekeza yeye kwa mtazamo wangu baada ya kusoma habari hii nadhani moja ya eneo amabayo CCM itafanyia kazi kwa nguvu zake zote ni Blogs watakuwa wanaamini kuwa Ushindi wa Dr. Slaa na Udhaifu wa CCM umejengwa sana kupitia Blogs na hii ndio Ujinga wa Viongozi wetu uwezo mdogo na kuropoka sasa nadhani maana yake ni kuendeleza mapambano ujumbe umefika; hajui hata maana ya kuwekeza amekalili moja ya kufanyabiashara basi akili yake yote imeishia hapo, kama wangekuwa na takwimu za watanzania mmoja mmoja ndani na nje ya Tanzani na kuheshimu uwekezaji wa akili tungekuwa mbali sana maana wapo sawa wanaoweza kuwekeza assets na liabilities katika biashara kama yeye anavyojua kuwa ndio uwekezaji pekee lakini tupo ambao tunaweza kuwekeza akili na akili zetu zinatumika huku nje na kuheshimika majibu ya matatizo mengi yangepatikana haraka kwa bei rahisi lakini kama hawawezi kupokea hata uwekezaji wa Akili ya Dr. Slaa hapo nyumbani sisi tulio mbali hawataweza hatakidogo, kwanza atwambie katika Bunge lilipita kwa miaka yote mitano Dr. Slaa aliwekaza rasilimali akili kiasi gani? naSerikali imetumia kiasi gani na inampango gani zaidi katika kuendeleza uwekezaji huo ndio atugeukie sisi alete hoja sio lawama.

Kwa kifupi ndio hivyo nadhani anataka kutoa ujumbe kuwa walio nje wengi sio CCM, kwa lugha raisi ila kwa vile akili yake teketeke anasema wanalalamika.
 
Back
Top Bottom