Hivi dini zingine hawaruhusiwi kuchinja?

Wakristo sio tu kwamba haturuhusiwi kuchinja, tunaweza na tunaruhusiwa kula chochote isipokua nyamafu tu. Tukiamua kuchinja wenyewe hakuna tatizo lolote kwa upande wetu, tatizo jamii zetu zimeingiliana na kuna ukaribu wa hali ya juu sana na ujirani kati ya waumini wa dini hizi mbili, sasa kwa wengine hawaruhusiwi kula kilichochinjwa bila kufuata taratibu zao, kuamua kuchinja wenyewe italeta kuwanyima ushiriki wa hao ndugu na jamaa zetu.

Tunafanya hivyo kwa kuweka maelewano tu na kujumuika, kuchinja tunaweza sana. Kama hatuwezi, mnyama nani hua anachinja?
Safi sana, mungu akuongezee hekma na busara. Umejibu kwa hekma sana suala hili...!! Bravo
 
Ni vema kufanya hivyo kutokana na ugeni wa uislamu kwa waislamu walio wengi. Ila kiuhalisia waislamu wanaruhusiwa kula kilichochinjwa na wakristu pia mayahudi kwani ktk Qur-ani ipo aya inaruhusu kula vilivyochinjwa na watu walioteremshiwa Taurati na Injili. Ila si halali kula kilichochinjwa na mshirikina hata kama ni muislamu kama wale wanaojitia kutibu kwa kutumia majini na wapiga nyota.
Pia ktk uislamu mwanamke aruhusiwa kuchinja.
Ukija na Aya itathibiti ukweli wako..!!
 
Wakristo sio tu kwamba haturuhusiwi kuchinja, tunaweza na tunaruhusiwa kula chochote isipokua nyamafu tu. Tukiamua kuchinja wenyewe hakuna tatizo lolote kwa upande wetu, tatizo jamii zetu zimeingiliana na kuna ukaribu wa hali ya juu sana na ujirani kati ya waumini wa dini hizi mbili, sasa kwa wengine hawaruhusiwi kula kilichochinjwa bila kufuata taratibu zao, kuamua kuchinja wenyewe italeta kuwanyima ushiriki wa hao ndugu na jamaa zetu.

Tunafanya hivyo kwa kuweka maelewano tu na kujumuika, kuchinja tunaweza sana. Kama hatuwezi, mnyama nani hua anachinja?
Jibu nzuri sana!
 
Hapa hatuzungumzii muislamu mmoja mmoja twazungumzia sheria ya kiislamu juu ya vichinjwa vya ahlul kitab (watu waliopewa kitabu; mayahudi & wakristu)
Watu wa kitabu zama hizi wapo. Vitabu vyenyewe vishachakachuliwa sio tena kama walivyoteremshiwa.
 
Sisi tunaamini katika MOLA , Mungu Mmoja asiyekuwa na Mshirika hajazaa wala Hajazaliwa. Muumba mbingu na Dunia na vilivyopo ndani Yake. Kama na wewe unaamini katika hili ni Ruksa Kuchinja ilimuradi kabla ya Kuchinja uchinje kwa Kumtaja yeye na Kumkusudia yeye MOLA WETU. ! !
Kula chakula ambacho hakijachinjwa kwa kumtaja "MOLA WETU" kinakuwekaje mbali nae? Una uhakika gani kama hana watoto? Mzazi wa Adam ni nani?
 
Mkuu usihofu, kwenye mshuko nakuita unachinja wewe, sisi sote ni ndugu, hizi dini tumeletewa haziwezi kuvunja uhusiano wetu.
Mkuu andaa kitu kama hii
Karibu mboka mkuu, ila kuwa makini maeneo ya stendi ukifika unitaarifu wasije watoto wa ng'ambu wakakuibia mabegi yako.
Poa mkuu uje unipokee ila njoo na gobole.
 
Mbona huwa tunachinja kitimoto na baadhi ya watu wanaodai ni haramu kwao huja na kula? sie huwa hatupendi ujinga, tunachinjaga tu na bado wanakulaga!
 
Watu wa kitabu zama hizi wapo. Vitabu vyenyewe vishachakachuliwa sio tena kama walivyoteremshiwa.
Kuchakachuliwa ni toka wale waliokuwa ktk enzi za mtume Muhammad, na ndio maana utakuta aya kedekede ndani ya Qur-an zikiwazungumzia ktk kwenda kwao kinyume na vitabu vyao na pia kuvichakachua...nimeshajibu swali hili hapo nyuma na nimeweka aya hizo na maelezo ya ahlul-ilmi ktk jambo hilo.
 
Ukija na Aya itathibiti ukweli wako..!!
Aya nimeshazimimina kibao na hadithi za mtume na uelewa wa wanazuoni tegemezi. Wale wapingao ni jukumu lao walete hapa aya au hadithi ya mtume inayokataza muislamu asile vinavyochinjwa na myahudi au mkristo....na hajaleta hata mtu mmoja hapa zaidi ya maelezo makavu tuliyorithi kwa babu zetu.
 
Kula chakula ambacho hakijachinjwa kwa kumtaja "MOLA WETU" kinakuwekaje mbali nae? Una uhakika gani kama hana watoto? Mzazi wa Adam ni nani?
Mola hawezi kuwa na watoto yeye ni muumbaji siyo mzazi , uzazi ni sifa ya viumbe siyo ya MOLA ! Adam ni kiumbe kama wewe aliumbwa na Mola , Ukafiri unaanzia pale binadamu anapojipa au anapo pewa sifa ya MOLA "ALLAH" ni Haramu kumshirikisha Mola katika Ufalme wake.
 
Aliyekuumba ukimuita Baba unakosea? Mzazi ni nani?
 
Sausage zinatoka American Garden,zinachinjwa wa wamarekani wakristo.

Nyama za makopo nyingi zinatoka Israel ,Denmark & Sweden!

Mimi naishi Banana nna kuku zaiidi ya mia tano na mnachinja mwenyewe ,wanakula hao watakatifu .

Ukienda uchagani hakuna waislamu ama wapo walowezi tu na wanakula nyama!
Acheni akili za kikoloni za kiarabu,fungukeni mpate hata elim dunia,!
 
Back
Top Bottom