Hivi daktari ana thamani kuliko binadamu wengine???

JF imevamiwa na madaktari.........halafu wanatoa vi-argument mbuzi mbuzi.....eti tulisoma udaktari miaka mingi, na therefore tulipwe zaidi....eti ili kutoa motisha kwa wengine wasome fani hiyo......duuuhh!
 
Ni kweli madaktari ni bora kuliko wengine, ndiyo maana wakigoma kila mtu analialia. Mie bado nawashangaa nyie watu. Daktari mwenye shahada ya kwanza analipwa 900,000 lakini karani wa benki kuu, au TRA asiye na shahada analipwa zaidi ya 1,000,000. mbunge ambaye hajamaliza hata darasa la saba analipwa 10,000,000. Halafu mnaongea kama wehu hapa. Unategemea huyo daktari anayefanya kazi ngumu ya kuokoa maisha ya watu alale njaa na watoto wake. Huo mshahara wa 900,000 mie niliupata miaka 9 iliyopita. Kwanza nashangaa mtu anawezaje kuishi na kamshahara kadogo hivyo hapa Dar. Lengo la kusoma ni kuwa na maisha mazuri. Msilete longolongo zenu zisizo na maana
mkuu samahan 900,000 waringe hiyo ni kabla ya kodi -680,000 kwa matumiz
 
Naona mwanzisha mada ni mwl, tena wa shule ya msingi, walim wote na polisi ni form 4 faluires.
 
Madakatari wa Tanzania kwani kulikuwa hakuna njia ingine ya kuigomea serikali iwasikiliza madai yao kuliko kutumia mbinu za kigaidi watu wasiokuwa na hatia wapoteze maisha ili maslahi yao yatimizwe.

Kisa wao ni watu wenye akili sana kuzidi wengine.
 
Madakatari wa Tanzania kwani kulikuwa hakuna njia ingine ya kuigomea serikali iwasikiliza madai yao kuliko kutumia mbinu za kigaidi watu wasiokuwa na hatia wapoteze maisha ili maslahi yao yatimizwe.

Kisa wao ni watu wenye akili sana kuzidi wengine.

Na Wasijidanganye kwa hilo...........
 
majadiliano yakifail kinachofuata ni kushinikiza tu.....mkuu hii nchi siyo Mali ya watu wachache walio na madaraka the so called Serikali ,hii nchi ni Mali ya watu wote na Lazima tukubaliane namna ya kuiendesha .sasa kusema madaktari wakimbie changamoto za nchi yao kwa kwenda nje(ambako ofcourse kuna room kwa wao kupata mafao bora kirahisi). Go on Doctors ,hakuna mtu mwenye hati miliki wa hii nchi eti useme madokta wanaweza kwenda nje wakati watanzania tunawahitaji huku sekta ya Afya ipo hoi bin taabani. Huo ni UDHAIFU wa kiuongozi ,kiakili ,kiimani na kiutawala.
shame be upon you all mnaosupport eti madaktari waondoke ,tumieeni ubongo.

Mkuu, mimi nafikiri kila mtu ana mawazo yake, na pia usifiikri kuwa mawazo yako na mtazamo wako na itikadi zako ndo sahihi na kila mtu atakubaliana na wewe, hayo ndo maisha, hata uklienda wapi. Kumbuka hilo!
 
JF imevamiwa na madaktari.........halafu wanatoa vi-argument mbuzi mbuzi.....eti tulisoma udaktari miaka mingi, na therefore tulipwe zaidi....eti ili kutoa motisha kwa wengine wasome fani hiyo......duuuhh!
vipi na wewe umefanyiwa usaili wa kusimamia Sensa?
 
Madakatari wa Tanzania kwani kulikuwa hakuna njia ingine ya kuigomea serikali iwasikiliza madai yao kuliko kutumia mbinu za kigaidi watu wasiokuwa na hatia wapoteze maisha ili maslahi yao yatimizwe.

Kisa wao ni watu wenye akili sana kuzidi wengine.
hebu washauri wewe kama njia gani mkuu? na siyo kusema tu wangetumia njia nyingine ,semeni zipi hizo maana wabongo kazi yenu kulalamika tu na kulaumu tu vitendo hakuna.
 
Unataka kutwambia kwamba. Watu wote sawa? Mbona baba yako huwa hawi na msafara kama wa kikwete anaposafiri?
Naomba mnijibu jamani, kwa nini hawa madaktari wantumia uhai wetu kuomba nyongeza ya mshahara
Kwani wao ni bora kukliko hawa wafuatao
POLISI
WANAJESHI
WALIMU Nk
Daktari alipwe shs 10,000,000 halafu mwalimu aliyemfundisha alipwe laki nne??
Halafu wanatumia kisingizio cha huduma bora kudai mihela.
Hebu nisaidieni mawazo yenu
 
hebu washauri wewe kama njia gani mkuu? na siyo kusema tu wangetumia njia nyingine ,semeni zipi hizo maana wabongo kazi yenu kulalamika tu na kulaumu tu vitendo hakuna.

Hawashauriki hawa madaktari kwanza watakuambia wao wameangaika sana kwenye masomo yao.
 
Nilifikiri baada ya kumwona kova anadanganya ungejifunza kwamba yote alosema raisi wako kuhusu na madaktari kuhusu mishahara yao kwamba ni uongo tu sawa na wa huyu mkenya. Ni nini kinachokufanya uulize swali kama hili ikiwa unajua kwamba serikali yako ni waongo tena waliokubuhu hawana hata simile. Kama bado una mawazo haya jaribu kufikiria zaidi ya hapo, utapata ukweli, kama una lako jambo siyo juu yetu kukuelimisha
 
Sentesi inajitosheleza na ndio maana serikali inapigana nao...Ofcoz ni wa muhimu as they rescue our lives let them be valued as well...
 
nakuombea ili akili yako wewe mleta mada hii ufunguke ufahamu wako mapema,maana watu kama nyie ndo mnaorudisha nyuma maendeleo ya nchi hii,hivi umeangalia hizo picha ulizowekewa hapo juu kweli wewe maisha hayo siutakufa mapema kwa sababu ya mazingira hayo,tatizo lako wewe hutibiwi huko ndo maana unabwabwaja,chunga mdomo wako iko cku maneno yako yatakuhukumu
 
LA KUACHA WALIPA KODI WAFE?.....HAPANA!!!!! vifaa tiba havipo tunakubali, lakini uwepo tu wa daktari maeneo yale mgonjwa angalau ana kuwa na matumaini fulani. Chonde madaktari rudisheni mioyo nyuma ili mtuhudumie wagonjwa. hii serikali tuachieni sisi tuitie discpline kwenye ballot box 2015. MUNGU AWABARIKI SANA
 
Mbona hujauliza kama wabunge na Graduate anayeanza kazi BOT, Tanroads, TRA na wanaofanana nao kama wana thamani kuliko kada tajwa? Toka kale daktari anasifa yake, unataka kubadirisha leo?
Kwa ufupi madaktari wanastahili kulipwa zaidi ili tupate motisha kwa watoto kuzidi kusoma kozi za udaktari. La sivyo wakilipwa sawa na mwalimu, hakutakuwa na umuhimu wa watu kusoma miaka tano hadi sita ili awe daktari wakati ukisoma kozi ya miaka miwili mitatu tu unatoka kimaisha.

So soft touches, eti walimu wakilipwa sana watoto hawatapa motisha ya kusoma udaktari ndo nini ulichosema? unajielewa kweli? kwamba madaktari walipwe sana ili tu watu wapate motisha ya kusoma hiyo course, na vipi mwalimu akilipwa kidogo na watu wakose motisha ya kusoma ualimu hao waalimu wa kuwafundisha madr watatoka wapi? Hapo ndipo tunarudi pale pale kwamba kuna watu mnaamini udaktari ndo kazi ya muhimu kuliko zote nchini na hivyo wanaweza fanya chochote kile na kitimizwe kwa muda watakao. Wabongo wengi mnashadadia migomo ya madaktari bila kujua mantiki ya hawa madaktari.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom