Hivi daktari ana thamani kuliko binadamu wengine???

Chilisosi

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2008
Posts
3,050
Reaction score
748
Naomba mnijibu jamani, kwa nini hawa madaktari wantumia uhai wetu kuomba nyongeza ya mshahara
Kwani wao ni bora kukliko hawa wafuatao
POLISI
WANAJESHI
WALIMU Nk
Daktari alipwe shs 10,000,000 halafu mwalimu aliyemfundisha alipwe laki nne??
Halafu wanatumia kisingizio cha huduma bora kudai mihela.
Hebu nisaidieni mawazo yenu
 
barbecue.gif
 
mpcn299l.jpg
 
Ngoja na mimi nikujibu kwa picha

Sawa nijibu kwa picha lakini wasijione kuwa bora kuliko wengine.
Wao ni watumishi wa serikali na wanalipwa kwa kazi wanayofanya hivyo ni wajibu wao kututibu wakileta uzembe inabidi washitakiwe na wafungwe na vibali vyao vinyanganywe
 
Naomba mnijibu jamani, kwa nini hawa madaktari wantumia uhai wetu kuomba nyongeza ya mshahara
Kwani wao ni bora kukliko hawa wafuatao
POLISI
WANAJESHI
WALIMU Nk
Daktari alipwe shs 10,000,000 halafu mwalimu aliyemfundisha alipwe laki nne??
Halafu wanatumia kisingizio cha huduma bora kudai mihela.
Hebu nisaidieni mawazo yenu
Mnafiki. Wewe utakuwa kilaza hata hujui bilogia ni nini?
 
Mbona hujauliza kama wabunge na Graduate anayeanza kazi BOT, Tanroads, TRA na wanaofanana nao kama wana thamani kuliko kada tajwa? Toka kale daktari anasifa yake, unataka kubadirisha leo?
Kwa ufupi madaktari wanastahili kulipwa zaidi ili tupate motisha kwa watoto kuzidi kusoma kozi za udaktari. La sivyo wakilipwa sawa na mwalimu, hakutakuwa na umuhimu wa watu kusoma miaka tano hadi sita ili awe daktari wakati ukisoma kozi ya miaka miwili mitatu tu unatoka kimaisha.
 
Hili nalo neno, napita tu nitarudi baadaye
 
Daktari kumbuka anasaini kifo chako na uhai wako wanatakiwa kuheshimiwa sana na kupewa haki zao
 
Mbona hujauliza kama wabunge na Graduate anayeanza kazi BOT, Tanroads, TRA na wanaofanana nao kama wana thamani kuliko kada tajwa? Toka kale daktari anasifa yake, unataka kubadirisha leo?
Kwa ufupi madaktari wanastahili kulipwa zaidi ili tupate motisha kwa watoto kuzidi kusoma kozi za udaktari. La sivyo wakilipwa sawa na mwalimu, hakutakuwa na umuhimu wa watu kusoma miaka tano hadi sita ili awe daktari wakati ukisoma kozi ya miaka miwili mitatu tu unatoka kimaisha.
Mkuu umeongea machache lakini yana point kali. Naakushukuru kwa jibu. lakini mshahara usiwe wa kutisha. mie sikatai walipwe vizuri na wapewe usafiri / mkopo. Ni kweli kabisa kozi ya polisi ni miezi sita na hakuna kufeli wakati udaktari unasoma mpaka kichwa kinauma. kwa hilo nakushukuru
 
Naomba mnijibu jamani, kwa nini hawa madaktari wantumia uhai wetu kuomba nyongeza ya mshahara
Kwani wao ni bora kukliko hawa wafuatao
POLISI
WANAJESHI
WALIMU Nk
Daktari alipwe shs 10,000,000 halafu mwalimu aliyemfundisha alipwe laki nne??
Halafu wanatumia kisingizio cha huduma bora kudai mihela.
Hebu nisaidieni mawazo yenu
Hapana. Daktari hana thamani. Wenye thamani ni wanasiasa kama Lusinde wanaolipwa mara kumi zaidi ya malipo ya madaktari. Tumeambiwa na Chikawe juzi kuwa wenye thamani ni wajumbe wa tume ya katiba kama Salim Salim ambao pamoja na kugharamia nyumba anayoishi kama waziri mkuu mstaafu, bado tunalazimishwa kumlipa posho ya pango. Orodha ni ndefu sana lakini madaktari hawamo kwenye orodha hiyo.
 
hapa madaktari hawawezi na watakimbia tu kuwaachia JWTZ
Kwa hiyo Dr sii lolote wao wangekaa pembeni wapo wenye moyo hata huko JW wapo MUNGU atatusaidia MGOMO sinema yake imeisha, tusianze kutafuta mshindi. Stearling hauawi
 
Hembu tufafanulie uthamani wa binadamu ukoje? Ili tuweke mlinganyo sahihi wa Dk na binadamu.
 
Hebu soma story kama hii utafakari, utaelewa ni kwa nini mambo haya yanatokea. Na huu ndiyo ukweli wa kazi yao kila siku:

Daktari, " sister tuwe tunafanya urine Dipstick kuangalia urine protein kwa huyu mgonjwa kila siku"

Nurse, "Daktari hizo ziliisha mwezi sasa labda tukaazime kwenye wodi xx"

Daktari, " BP ya huyu mgonjwa ni 160/100 anapata dawa huyu??"
...
Nurse, "Kila mara pharmacy wanaandika o/s kwenye prescription"

Daktari, " wapatie ndugu wakanunue basi"

Daktari, "watu wa xray wanasemaje??"

Nurse, " wanasema film zimeisha mpaka ziletwe"

Daktari, " nataka kucheck RBG ya huyu mgonjwa"

Nurse, " mpaka nikaazime Glucometer yetu imeharibika mwezi sasa"

Daktari, " Dada nahitaji kukutibu ila hakuna dawa, kipimo cha picha ya kifua hakuna, kipimo cha mkojo hakuna, kipimo cha sukari hakuna kwa hiyo tusubiri mpaka vitakapopatikana ila kama unaweza kuwaambia nduguzo wakakugharimikie nje sawa"

Mgonjwa, " mimi sina hela na ndugu zangu hawana uwezo. Naomba unisaidie Daktari"

Hebu mshauri hapo daktari afanyaje mkuu ?

hlf huo uthamani wa binadamu unaupima kwa kutumia vigezo gani?
 
Back
Top Bottom