Watatu watatu kwenye vitanda, wamelala mpaka chini, kuambukizana magonjwa nje nje. Sasa hapo kama wewe ni daktari na ofisi yako ndo hiyo day in day out, si unakuwa katika risk kubwa ya wewe mwenyewe kuambukizwa maradhi na kuyapeleka majumbani kwao? Au wao wana kinga fulani kutoka mbinguni hatuijui.........Ahhhhh gomeni tu hayo mazingira ya kazi siyo kabisa....
Tusiwe mambumbumbu kwa hali hii (jumlisha na mziki wa shule yao ya miaka umri wa mtoto kuzaliwa hadi kufika darasa la pili), risk allowance haki yao, sindano za kinga haki yao, posho ya mazingira magumu haki yao, ongezeko la mshahara haki yao, tena hata hayo madai ya maboresho ya huduma ya afya wala msingepigia kelele, mngetuacha wavunja miwa wenyewe tupigike mpaka tutakapoona haja ya kuiwajibisha serikali dhaifu!!