Historia ya ndoa yangu

Historia ya ndoa yangu

yaambasa kwa asilimia 90 kama sio 100 wewe ndio chanzo kikubwa cha hio ndoa kuvunjika na huyo mwanaume ni mvumilivu sana na ana haki kuondoka. Kasoro yake ni kutohudumia watoto tu!
 
Last edited by a moderator:
Mmmmnnnnhhhhh...kukuchiti akuchiti yeye..msamaha uombe wewe...hapana aisee...

Ukinichiti nikakununia kaogee maji ya bahari...timbwili lake kununa ni cha mtoto...ntakusimanga mpaka uone dunia chungu...
Mie naomba kufahamu, mwenzako umemkamata anachepuka ukamnyima si ndo unampa warrant ya kuimarisha penzi la kuchepuka? Hivi unadhani dawa ya moto ni moto (yaani unakula k ya mwenzangu, yangu nakunyima) au ni maji (kama una hamu ya k njoo upate na usaze)? Naamini mwanaume kumwacha mke wake na kuchepuka si jambo dogo na litakuwa lina mzizi ingawa yanayoonekana ni majani tu. Hivyo kutibu majani hakutaokoa mti bali kutibu mzizi. Karibu Njinjo
 
nuna mchepuko unazidisha manjonjo zaidi mafahari wawili hawakai zizi moja
Nimeipenda comment yako. Binadamu lazima tuache jino kwa jino katika mapenzi hata ndoa. Lazima ujiulize umuhimu wa mwenzako katika ustawi wa familia na wewe pia. Kushuka ingawa ni shubiri lakini ni muhimu. Hata mkikwaruzana mchana, baada ya taa kuzimwa acha wapenzi waendelee, hawa ninaoita wapenzi (wanaoitwa vikojoleo) ni wasuluhishi wazuri katika mapenzi ndugu yangu. Wao wakipatana hakuna linaloharibika. Kununa ni SUMU.
 
Ushauri wangu (japo wanaume hawataupenda) ni kuwa jipende kupita maelezo...
Kama mwili umebadilika sababu ya watoto fanya mazoezi...
Yani jipende kweli kweli...
Tafuta ela...kuwa independent..tena hata ela ya watoto usimuombe...lakini omba talaka ili uwe huru

Who knows unaweza pata partner wa kumalizia siku zilizobaki duniani...
Usikubali partner kijana (sharobaro)...wala mume wa mtu...tafuta alofiwa na mke...ila mkapime afya...

Wanaume wengi jeuri yao ni kuona wake zao wamezeeka sababu ya kuwa na watoto...
Kuwakomoa ni kuwaonyesha kuwa uzee mwisho Msata...
Hivi nani atakubali kuoa mwanamke na watoto watatu? Je, kama na huyo mwanaume ana watoto si muungano tata kama muungano wa Tanzania siku za usoni?
 
pole sana.kuna wanaume ni wakatili sana hawajali kabisa maumivu wasababishayo kwa wake zao wala watoto.cha msingi umeshamjua ni mume wa aina gani
ushauri wangu kama anatoa matumizi kwa watoto wewe lea wanao.na jitahidi kutomfuatafuata.maana ukifanya hivyo anazidi kukudharau!na hata kama asipoleta pesa kama unajimudu lea tu wanao na kama hujimudu tafuta means ya kuweza kujiongezea kipato.kwa tabia ya mumeo wala usiwe na wasiwasi huko alikoenda kama kwa mwanamke basi nae atamshindwa!
 
yaambasa kwani ungetumia ID ya kila siku ungepungukiwa nini? Au una watu humu wanakufahamu? Unaogopwa kusemwa?

Hii taasisi ni delicate sana. Kama tukishindwa kuiendesha haya ndio matokeo take. Mnanuniana kwa miaka mitano? Inawezekanaje? Vyuoni wangeanzisha courses za 'ndoa management ' lol. Naona zinawashinda walio wengi sasa.

Pole Sana!!

Humu hakuna wanaonifahamu, ila yeye ndio sikutaka ajue id ninayotumia humu ndio sababu ya kutumia id nyingine
 
Hivi nani atakubali kuoa mwanamke na watoto watatu? Je, kama na huyo mwanaume ana watoto si muungano tata kama muungano wa Tanzania siku za usoni?

Mkuu labda huko kwenu... Huku kuna mwanaume alifunga ndoa na mwanamke ana watoto 6, tena wawili tu ndio wa baba mmoja na waliobaki kila.mtu na baba yake. Walipendezaje??
 
Mkuu labda huko kwenu... Huku kuna mwanaume alifunga ndoa na mwanamke ana watoto 6, tena wawili tu ndio wa baba mmoja na waliobaki kila.mtu na baba yake. Walipendezaje??

Me dada yangu aliachwa huku kashazaa watoto watatu...na kuna jamaa kashafika bei, soon tunakula mpunga
 
Hivi kwanini mnaleta matatizo yenu humi
 
Hivi nani atakubali kuoa mwanamke na watoto watatu? Je, kama na huyo mwanaume ana watoto si muungano tata kama muungano wa Tanzania siku za usoni?

wanaume wengi wanaotesa wake zao baada ya kuwazalisha watoto wengi hujidanganya kuwa mwanamke akishazalishwa watoto wengi hawezi kuolewa na mwanaume mwingine.dhana hii sio ya kweli kabisa.nina auntie yangu aliteswa ten yrs na ana watoto watano!mumewe kutwa anamsimango utaenda wapi wewe ushazeeka akutake nani? Mungu sio john wala alex bwana katokea mdingi anayeyajua mateso ya yule mwanamke mana mtaani kote wanaona vitimbwi vya mumewe!mzee wa watu kamchukua mazima mazima.sasa hivi anakula bata na mumewe netherland!jamaa kalia wee hadi kachoka!na yule mdingi anawasomesha watoto kams wake!nae ana wakwake watatu!hela anazo!mdada karudije kijana!mrembo haswa!cha msingi mdada asikurupuke kuchukuliwa na wanaume atulie kwanza ila pia usiwr unanuna .
 
Wana jamvi naamini mu wazima wa afya

Nimeolewa miaka nane iliyopita na tumebahatika kupata watoto watatu,tangu nimeolewa hiyo miaka naweza sema nimeishi na mume wangu miaka mitatu,namaanisha ki-ndoa.Maisha ya ndoa yetu naweza sema ni ya ajabu sana kwa jinsi nionavyo mimi.Mume wangu akinikosea huwa ninatabia ya kununa ili aniombe msamaha,na kwasababu mwanaume kuomba msamaha ni ngumu huwa nahitaji basi hata kutambua tu kosa lake.Lakini kwa mwenzangu imekua ni vigumu,nikinuna nae huwa ananuna.

Miaka mitano iliyobaki tumeishi maisha ya kununiana mpaka hivi leo hatuongei.Mnuno wa mwisho sababu yake nilimgundua anatembea na binti mmoja na kwa ushahidi,lakini hakujutia wala kuomba msamaha,badala yake nilinuna nae akanuna yapata mwaka mmoja sasa,tumelala kitanda kimoja hanigusi wala simgusi, mpaka sasa kakimbia nyumba,kaniacha mimi na watoto ikafikia hatua akakataa kutoa pesa ya chakula ikabidi nikamshitaki kwa wazee,ila ilishindikana,wazee wakaniambia nimpeleke mahakamani,hivi sasa anatoa ela ya chakula kwa amri ya mahakama ingawa hapendi.

Wanaume mkigombana na wake zenu muwahudumie watoto wenu maana ni wenu,baada ya kusema maneno haya kifua changu kimepumua na ninaamini kuanzia leo nitakula chakula vizuri na kuanza maisha mapya.Usitukane wala usidharau maana ni dukuduku langu la muda sasa nitarudi kutumia id yangu ya siku zote .Asanten

We mama iko na tatiso aisee! Kama wakuwa muke yangu ntakunyoosha tu. Hivi wewe unadhani ukimnunia my husband wako ndo unamkomoa? Take it from me, unamwambia azidi kuisaliti ndoa!
 
yambasa pole sana dada yangu na hongera kwa kucheua lilolokuwa linakukera. Uwe na amani sasa. Kula vizuri, jipendezeshe ile mbaya tena kama kabinti ila chunga usile sana ukafutuka maana umeshaondoa stress. Sasa muda muafaka ukifika nawe pata hapo kipoozeo chako ila mpimane vvu kwanza na sharti condom kila wakati. Baada ya hapo maisha yako yatabadilika sana kwa pande zote yaani amani na kimaendeleo. Niliapa nilipoamua kuoa kuwa sitakaa nimkoseshe mke wangu raha. Kukosana madogo madogo kupo ila tunayamaliza and to be frank mimi ninajua kuomba msamaha direct and indirect by doing little extras. Wanaume wrngu tu vyanzo vya migogoro ya ndoa. Tukubali.
 
Last edited by a moderator:
Kwanza pole kwa masahibu ya ndoa, pole kwa kazi ngumu ya kuishi kwa kununiana na mumeo, pole kwa pilika za mahakamani, pole kwa kulea wanao bila baba yao karibu. Pole kwa ndoana, na Mwisho Pole kwa wivu mkali uliosababisha kila kitu kinacho endelea sasa.

Mpaka kufikia kuwaeleza wazazi kwamba ndani kuna mgogoro uwa ni hatua ya mbali sana, nimeshuhudia maswala mengi yanayo fika kwa wazazi yanayohusu ndoa kutofanikiwa kupata suluhu, maswala yanayoenda baraza la usuluhishi, ustawi wa jamii, mashirika ya utetezi wa haki, viongozi wa dini na mpaka mahakama huwa hakuna nusuru ya ndoa.

Suluhu ya ndoa ni mume na mke kukaa pamoja, narudia kukaa pamoja kuongea tofauti zenu wenyewe bila mtu mwingine katikati. Hapo maridhiano huweza kupatikana, kuongea kwa busara na upole kunafungua moyo. Kosa kubwa kwenye ndoa ni kufunga mawasiliano, ukifunga ndani ukakimbilia upande wa pili kufungua huko huwa haisaidii. Ninaongea kwa uzoefu.

Hatua mliyofikia...mpaka mahakamani ni mtihani kufungua mawasiliano mapya, itabidi mkaribishe uwepo wa Mungu ndio mambo yatakuwa sawa. Naamini muda si mrefu mtarudi kuishi pamoja na kununa kutakuwa historia, inawezekana. Amini hakika inawezekana.

Asante kwa ushauri wako
 
Back
Top Bottom