Historia ya ndoa yangu

Historia ya ndoa yangu

hamna ndoa hapo kuna vyeti vya ndoa kuwafanya mshiriki kanisani na mkifa mzikwe bass
hapo kila mtu anatamani mwenzie atangulie kufa
 
Ushauri wangu (japo wanaume hawataupenda) ni kuwa jipende kupita maelezo...
Kama mwili umebadilika sababu ya watoto fanya mazoezi...
Yani jipende kweli kweli...
Tafuta ela...kuwa independent..tena hata ela ya watoto usimuombe...lakini omba talaka ili uwe huru

Who knows unaweza pata partner wa kumalizia siku zilizobaki duniani...
Usikubali partner kijana (sharobaro)...wala mume wa mtu...tafuta alofiwa na mke...ila mkapime afya...

Wanaume wengi jeuri yao ni kuona wake zao wamezeeka sababu ya kuwa na watoto...
Kuwakomoa ni kuwaonyesha kuwa uzee mwisho Msata...

napendaga sana comments zako ujue
 
pole sana mtoa mada ila naona hata wewe hukuwa na nia ya dhati ya kulinda ndoa yenu
 
Ushauri wangu (japo wanaume hawataupenda) ni kuwa jipende kupita maelezo...
Kama mwili umebadilika sababu ya watoto fanya mazoezi...
Yani jipende kweli kweli...
Tafuta ela...kuwa independent..tena hata ela ya watoto usimuombe...lakini omba talaka ili uwe huru

Who knows unaweza pata partner wa kumalizia siku zilizobaki duniani...
Usikubali partner kijana (sharobaro)...wala mume wa mtu...tafuta alofiwa na mke...ila mkapime afya...

Wanaume wengi jeuri yao ni kuona wake zao wamezeeka sababu ya kuwa na watoto...
Kuwakomoa ni kuwaonyesha kuwa uzee mwisho Msata...

Nimeupenda ushauri
 
Siku mapaa ya nyumba yakifumuliwa na kuta za viambaza vya nyumba kuporomoka, duniani hapatatosha.

Pole sana mwanamama, wewe endelea kupambana na maisha, usikate tamaa, pigania familia yako na Mungu atakujaalia.

Vv
 
Duh...!!

Huna watu wa ukweli unaofahamiana nao ambao unaweza ukawaeleza masahibu ya ndoa yako hadi uje humu kwa mazimwi......

NN, Mazimwi wapo hapa JF, lakini pia hata Malaika wamo.

BTW, wewe Nyani ngabu, nawe ni Zimwi?
 
Wana jamvi naamini mu wazima wa afya.

Nimeolewa miaka nane iliyopita na tumebahatika kupata watoto watatu,tangu nimeolewa hiyo miaka naweza sema nimeishi na mume wangu miaka mitatu,namaanisha ki-ndoa.Maisha ya ndoa yetu naweza sema ni ya ajabu sana kwa jinsi nionavyo mimi.

Mume wangu akinikosea huwa ninatabia ya kununa ili aniombe msamaha,na kwasababu mwanaume kuomba msamaha ni ngumu huwa nahitaji basi hata kutambua tu kosa lake. Lakini kwa mwenzangu imekua ni vigumu, nikinuna nae huwa ananuna.

Miaka mitano iliyobaki tumeishi maisha ya kununiana mpaka hivi leo hatuongei. Mnuno wa mwisho sababu yake nilimgundua anatembea na binti mmoja na kwa ushahidi, lakini hakujutia wala kuomba msamaha, badala yake nilinuna nae akanuna yapata mwaka mmoja sasa, tumelala kitanda kimoja hanigusi wala simgusi, mpaka sasa kakimbia nyumba, kaniacha mimi na watoto ikafikia hatua akakataa kutoa pesa ya chakula ikabidi nikamshitaki kwa wazee, ila ilishindikana, wazee wakaniambia nimpeleke mahakamani, hivi sasa anatoa ela ya chakula kwa amri ya mahakama ingawa hapendi.

Wanaume mkigombana na wake zenu muwahudumie watoto wenu maana ni wenu,baada ya kusema maneno haya kifua changu kimepumua na ninaamini kuanzia leo nitakula chakula vizuri na kuanza maisha mapya.

Usitukane wala usidharau maana ni dukuduku langu la muda sasa nitarudi kutumia id yangu ya siku zote.

Asanten

Kwahiyo yaambasa mwenzako akiwa kwenye hali kama hii humsaidii kabisa ? hivi unadhnai kweli mwanaume aliyekamilka anaweza endelea baki ndani kwa mazingira kama haya ya kunyimwa "conjugal right "
 
Last edited by a moderator:
INASIKITISHA JAMANI SOMA HII! Baba na
mama baada ya kurudi kazini pamoja wakakuta
BARUA iko mezani SEBULENI ikisema.... "Baba
na mama, ni matumaini yangu kuwa mtasoma
ujumbe wangu huu kwenye karatasi niliyoiweka
juu ya meza, naomba msishtuke maana ni
mambo ya kawaida kwenye maisha tunayoishi,
najua mtaumia kwa vile bado nasoma na ndo
nipo kidato cha kwanza..." Napenda
kuwajulisha kwamba sasa hivi mnaposoma hii
barua sipo nyumbani, nimetoroka maana
nimegundua nina uwezo wa kujitegemea kwa
sababu mimi ni kijana mwenyewe umri wa miaka
14 na ninajua kipi chema na kipi kibaya. Tangu
mwezi mmoja uliopita nilikuwa na uhusiano na
binti mmoja aliyeitwa Rachel, mwenye umri wa
miaka 27 na kwa sasa ndo naishi naye kwenye
chumba alichopanga. Nilipokuwa nyumbani
sikuwa napata hela za kutosha ila sasa
nimeanza kushika noti za shilingi 10,000...
Msichana niliyenaye ni mzuri sana wa umbo na
ninampenda sana, amenifundisha njia za
kutafuta hela. Amenipangia kazi ya kuuza
madawa ya kulevya na yeye ikifika usiku
anaenda kuuza mwili wake, basi kila siku
tunapata hela ya kutosha, huyu mchumba
wangu ni msichana mwenye bidii, kwa siku
analala masaa 6 tu maana mwanaume yeyote
akija lazima awe naye chumbani kwa muda wa
masaa 3. Msiwe na hofu, nipo salama kabisa
na nimeamua kumwoa Rachel mana ni kila kitu
kwangu. Pia amenunua gari la kubebea mbao
kwa hiyo biashara inakwenda vizuri, Rachel
amekwenda kupima afya na amekutwa na
upungufu wa kinga mwilini, mara nyingi
namridhisha anapotaka kitu fulani, iwe kufanya
naye mazoezi ya viungo au kufanya naye
mapenzi, si mnajua unapokuwa na mgonjwa
unatakiwa kuwa naye karibu, ila mimi pia
sijihisi vizuri
maana kila saa nakohoa tu na sina uhakika
kama nimeathirika. Tumepanga baada ya miaka
miwili tutawatembelea, nadhani mpaka miaka
miwili iishe atakuwa ameshajifungua, na ni
furaha yangu mtamwona mjukuu wenu. Wazazi
wangu sina la kuongeza kwaherini Mungu
akipenda tutaonana. N.B: "Baba na mama, mimi
nipo chumbani kwangu najisomea,
mnachokisoma ni home work ya mwalimu wa
kiswahili alituambia tutunge hadithi fupi ya
kusisimua, naomba muiangalie kama kuna
makosa!"

Hahahah hii stori imenishtua afu mwisho nimekenua kwa kicheko sijui mama mtu alikuwa kwenye hali gani kabla ya kumalizia kusoma mwisho kabisa
 
wakati mie nina watoto 4 na natafuta mchumba
Kuolewa ni rahisi ila watoto wakikua hapo ndo muziki unogile.....Kila mtoto anajipambanua kwa ubini na Mama anaanza kuside na watoto aloolewa nao. Kukiwa na kidume ndicho kinaharibu mambo yote. Na kwa huyu mwanaume kama atakuwa na mtoto wa kike, akiwa mkubwa kunachimbika kwa mama wa kambo. Jamani angalia familia muungano zilivyo uzeeni. Unless Baba ana watoto wa kiume tu na mama ana wa kike tu (ingawa mbele ya safari si ajabu kukuta wajukuu wa ndani)
 
umenchekesha sana
tena huyo anao wa baba mmoja anaolewa kabisas

watoto sita huyo mwanaume anayefanya maamuzi magumu namna hiyo kama hana matatizo ya kizazi au akili basi atokapo alikuwa na mwanamke mzigo kama gunia la misumari
 
Nimeupenda ushauri

ili ndoa iwe salama ni lazima mwanamke awe ndo kipoozeo moto unapokuwa mkubwa lakini mwanamke akiwa petroli na ugomvi unapotokea anaimimina ndoa hiyo itakufa tu au mtapeana UKIMWI tu.WANAWAKE siku hizi wamesahau sana kuwa wao ni wanawake wanajaribu kushindana nasi hamtaweza ngo sanasana utazalishwa tu wanawake wenzio wanaojua kubembeleza wanamfaidi mumeo.NIWASHAURI WANADADA NA WANANDOA WANAWAKE MUME NI MFANO WA........ HIVYO MUHESHIMU AKIKUFANYIA KOSA ONGEA NAYE TARATIBU NA MPE USHAURI KWA KOSA ALILOFANYA NAYE ATAUMIA MOYONI MWAKE NA KUTAMBA NA KUFURAHI NA KUJIVUNA NINA MKE NA SI LIMWANAMKE. SISI HATUTAKI WANAWAKE WANAOPIGA MAKELELE TU AMA KULIA AMA KUFOKA TUNATAKA WANAWAKE WAPOLE NA WANYENYEKEVU
 
Duh...!!

Huna watu wa ukweli unaofahamiana nao ambao unaweza ukawaeleza masahibu ya ndoa yako hadi uje humu kwa mazimwi?

Ila cha muhimu ni wewe kujiskia vizuri. Kwa hiyo kama umejisikia vizuri kwa kufunguka humu basi haina shida.
Kwa hiyo na wewe ni mmoja wa mazimwi wa humu.
 
yaambasa

Naomba kukuuliza, hakuna chanzo kingine ni hilo la kucheat tu?

Halafu huko alikokimbilia ni kwa hyo aliyekuwa anacheat nae?


Naona hapa kuna tatizo kubwa!
Spiritual husband&spiritual wife
Hakuna mshindi lzm ndoa ivunjike unless seek the face of God
 
Back
Top Bottom