Historia ya ndoa yangu

Historia ya ndoa yangu

Wana jamvi naamini mu wazima wa afya

Nimeolewa miaka nane iliyopita na tumebahatika kupata watoto watatu,tangu nimeolewa hiyo miaka naweza sema nimeishi na mume wangu miaka mitatu,namaanisha ki-ndoa.Maisha ya ndoa yetu naweza sema ni ya ajabu sana kwa jinsi nionavyo mimi.Mume wangu akinikosea huwa ninatabia ya kununa ili aniombe msamaha,na kwasababu mwanaume kuomba msamaha ni ngumu huwa nahitaji basi hata kutambua tu kosa lake.Lakini kwa mwenzangu imekua ni vigumu,nikinuna nae huwa ananuna.

Miaka mitano iliyobaki tumeishi maisha ya kununiana mpaka hivi leo hatuongei.Mnuno wa mwisho sababu yake nilimgundua anatembea na binti mmoja na kwa ushahidi,lakini hakujutia wala kuomba msamaha,badala yake nilinuna nae akanuna yapata mwaka mmoja sasa,tumelala kitanda kimoja hanigusi wala simgusi, mpaka sasa kakimbia nyumba,kaniacha mimi na watoto ikafikia hatua akakataa kutoa pesa ya chakula ikabidi nikamshitaki kwa wazee,ila ilishindikana,wazee wakaniambia nimpeleke mahakamani,hivi sasa anatoa ela ya chakula kwa amri ya mahakama ingawa hapendi.

Wanaume mkigombana na wake zenu muwahudumie watoto wenu maana ni wenu,baada ya kusema maneno haya kifua changu kimepumua na ninaamini kuanzia leo nitakula chakula vizuri na kuanza maisha mapya.Usitukane wala usidharau maana ni dukuduku langu la muda sasa nitarudi kutumia id yangu ya siku zote .Asanten

Mwanamke Mpumbavu huvunja nyumba yake mwenyewe kwa mikono yake,,huu usemi waliousema hawajakosea umeona ufahari kumfanyia visanga mmeo angalia unavyoivunja nyumba yako kwa maelezo yako kuna shoga yako unamuelezaga matatizo yako ya ndan anakushauri ujinga km huo ndoa ni kuvumiliana na kusamehane angalia sasa mpk hela ya kula unaenda kuidai mahakaman
 
Jitahidi sana muyamalize kukuza watoto pekee yako si lelemama waweza chizika. Elimu, chakula,afya, malazi na mengineyo kwako utamudu?
 
Kununa mwaka? Ratiba yenu ikoje, hakuna outing? Holidays? Vacations au hata hamuombi Mungu? There must be a problem!!
 
Duh...!!

Huna watu wa ukweli unaofahamiana nao ambao unaweza ukawaeleza masahibu ya ndoa yako hadi uje humu kwa mazimwi?

Ila cha muhimu ni wewe kujiskia vizuri. Kwa hiyo kama umejisikia vizuri kwa kufunguka humu basi haina shida.

Nyani Ngabu Embu toa maelezo ya kina ina maana na mimi ni zimwi!? :wacko: nina mkia? mmh mbona siuoni...
 
Ha ha ha haaaa samahai hiyo naamini mmevunja rekodi ya dunia hapo hakuna kujitetea ni walewale tuu muda wote huo bila kulipiza kisasi? Kama kweli ulivumilia wewe ni mama shujaa kama ulishindwa chapa mwendo.
 
Wana jamvi naamini mu wazima wa afya

Nimeolewa miaka nane iliyopita na tumebahatika kupata watoto watatu,tangu nimeolewa hiyo miaka naweza sema nimeishi na mume wangu miaka mitatu,namaanisha ki-ndoa.Maisha ya ndoa yetu naweza sema ni ya ajabu sana kwa jinsi nionavyo mimi.Mume wangu akinikosea huwa ninatabia ya kununa ili aniombe msamaha,na kwasababu mwanaume kuomba msamaha ni ngumu huwa nahitaji basi hata kutambua tu kosa lake.Lakini kwa mwenzangu imekua ni vigumu,nikinuna nae huwa ananuna.

Miaka mitano iliyobaki tumeishi maisha ya kununiana mpaka hivi leo hatuongei.Mnuno wa mwisho sababu yake nilimgundua anatembea na binti mmoja na kwa ushahidi,lakini hakujutia wala kuomba msamaha,badala yake nilinuna nae akanuna yapata mwaka mmoja sasa,tumelala kitanda kimoja hanigusi wala simgusi, mpaka sasa kakimbia nyumba,kaniacha mimi na watoto ikafikia hatua akakataa kutoa pesa ya chakula ikabidi nikamshitaki kwa wazee,ila ilishindikana,wazee wakaniambia nimpeleke mahakamani,hivi sasa anatoa ela ya chakula kwa amri ya mahakama ingawa hapendi.

Wanaume mkigombana na wake zenu muwahudumie watoto wenu maana ni wenu,baada ya kusema maneno haya kifua changu kimepumua na ninaamini kuanzia leo nitakula chakula vizuri na kuanza maisha mapya.Usitukane wala usidharau maana ni dukuduku langu la muda sasa nitarudi kutumia id yangu ya siku zote .Asanten

Kwanza pole kwa masahibu ya ndoa, pole kwa kazi ngumu ya kuishi kwa kununiana na mumeo, pole kwa pilika za mahakamani, pole kwa kulea wanao bila baba yao karibu. Pole kwa ndoana, na Mwisho Pole kwa wivu mkali uliosababisha kila kitu kinacho endelea sasa.

Mpaka kufikia kuwaeleza wazazi kwamba ndani kuna mgogoro uwa ni hatua ya mbali sana, nimeshuhudia maswala mengi yanayo fika kwa wazazi yanayohusu ndoa kutofanikiwa kupata suluhu, maswala yanayoenda baraza la usuluhishi, ustawi wa jamii, mashirika ya utetezi wa haki, viongozi wa dini na mpaka mahakama huwa hakuna nusuru ya ndoa.

Suluhu ya ndoa ni mume na mke kukaa pamoja, narudia kukaa pamoja kuongea tofauti zenu wenyewe bila mtu mwingine katikati. Hapo maridhiano huweza kupatikana, kuongea kwa busara na upole kunafungua moyo. Kosa kubwa kwenye ndoa ni kufunga mawasiliano, ukifunga ndani ukakimbilia upande wa pili kufungua huko huwa haisaidii. Ninaongea kwa uzoefu.

Hatua mliyofikia...mpaka mahakamani ni mtihani kufungua mawasiliano mapya, itabidi mkaribishe uwepo wa Mungu ndio mambo yatakuwa sawa. Naamini muda si mrefu mtarudi kuishi pamoja na kununa kutakuwa historia, inawezekana. Amini hakika inawezekana.
 
Kama kaenda akikupa mimba nyingine useme pia usitufiche.
 
Duh ndoa ngumu mno aise..kuomba msamaa naweza nisiombe ila kula papuchi nnayolala nayo pembeni hata kwa wiki tu siwezi vumilia..au umeongeza chumvi ww mwaka mzima ..dah..huyo jamaa kabilagani kwanza..?!

Mkuu na kibaridi cha asubuhi uspime kabisa,masika yako kiangazi chako,we umenuna tu.
 
kwa maeelezo yako nimengudua wewe umbo lako ni mboge.!!
 
Nimeamua tu ili baada ya kuutua huu mzigo niliokuwa nao moyoni, niweze kuchangia mada zingine kama kawaida

yaambasa kwani ungetumia ID ya kila siku ungepungukiwa nini? Au una watu humu wanakufahamu? Unaogopwa kusemwa?

Hii taasisi ni delicate sana. Kama tukishindwa kuiendesha haya ndio matokeo take. Mnanuniana kwa miaka mitano? Inawezekanaje? Vyuoni wangeanzisha courses za 'ndoa management ' lol. Naona zinawashinda walio wengi sasa.

Pole Sana!!
 
Last edited by a moderator:
Kwanza pole kwa masahibu ya ndoa, pole kwa kazi ngumu ya kuishi kwa kununiana na mumeo, pole kwa pilika za mahakamani, pole kwa kulea wanao bila baba yao karibu. Pole kwa ndoana, na Mwisho Pole kwa wivu mkali uliosababisha kila kitu kinacho endelea sasa.

Mpaka kufikia kuwaeleza wazazi kwamba ndani kuna mgogoro uwa ni hatua ya mbali sana, nimeshuhudia maswala mengi yanayo fika kwa wazazi yanayohusu ndoa kutofanikiwa kupata suluhu, maswala yanayoenda baraza la usuluhishi, ustawi wa jamii, mashirika ya utetezi wa haki, viongozi wa dini na mpaka mahakama huwa hakuna nusuru ya ndoa.

Suluhu ya ndoa ni mume na mke kukaa pamoja, narudia kukaa pamoja kuongea tofauti zenu wenyewe bila mtu mwingine katikati. Hapo maridhiano huweza kupatikana, kuongea kwa busara na upole kunafungua moyo. Kosa kubwa kwenye ndoa ni kufunga mawasiliano, ukifunga ndani ukakimbilia upande wa pili kufungua huko huwa haisaidii. Ninaongea kwa uzoefu.

Hatua mliyofikia...mpaka mahakamani ni mtihani kufungua mawasiliano mapya, itabidi mkaribishe uwepo wa Mungu ndio mambo yatakuwa sawa. Naamini muda si mrefu mtarudi kuishi pamoja na kununa kutakuwa historia, inawezekana. Amini hakika inawezekana.
ASANTE KWA HIYO ELIMU 1st AID
 
Last edited by a moderator:
Subirini katiba pendekezwa ipite kwanza maana humo haki zote zitakuwa sawa kwa wanandoa, hata haki ya kununa itakuwa sawa.
 
Ila muda mwingine usiwe mwepesi kununa, mwanaume hanuniwi... ungeangalia kakosa nini kwako hadi kafata nje, yote hayp yasingetokea eti!!!

ACHA BASI USHAURI WA KI MEMKWA unavyosema mwanaume hanuniwi unamaanisha hata ukimfumania ufurahi tu, asipotoa matumizi ya watoto unampongeza au? huu ni mfumo dume wakishamba sana. we jiweke kwenye nafasi ya mwanamke ambaye mumewe haongei naye. hatunzi watoto. ana michepuko live hazira itakujia automatically. huyo akifulia nakupata ukimwi atarudi wewe ndo wakati wa shida yule mwingine niwaraha eeh.mtoto umleavyo yawezekana alianza kidogokidogo hukuoonyesha msimamo wako
 
Back
Top Bottom