Historia ya ndoa yangu

Historia ya ndoa yangu

yaambasa

Naomba kukuuliza, hakuna chanzo kingine ni hilo la kucheat tu?

Halafu huko alikokimbilia ni kwa hyo aliyekuwa anacheat nae?


Naona hapa kuna tatizo kubwa!
Spiritual husband&spiritual wife
Hakuna mshindi lzm ndoa ivunjike unless seek the face of God

Ni moja kati ya comments nlizozielewa vizur katika uzi huu!! i wish mtoa mada aelewe zaidi ya nlivyoelewa na atamani kufanyia kazi swala uliloshauri.
 
Wana jamvi naamini mu wazima wa afya.

Nimeolewa miaka nane iliyopita na tumebahatika kupata watoto watatu,tangu nimeolewa hiyo miaka naweza sema nimeishi na mume wangu miaka mitatu,namaanisha ki-ndoa.Maisha ya ndoa yetu naweza sema ni ya ajabu sana kwa jinsi nionavyo mimi.

Mume wangu akinikosea huwa ninatabia ya kununa ili aniombe msamaha,na kwasababu mwanaume kuomba msamaha ni ngumu huwa nahitaji basi hata kutambua tu kosa lake. Lakini kwa mwenzangu imekua ni vigumu, nikinuna nae huwa ananuna.

Miaka mitano iliyobaki tumeishi maisha ya kununiana mpaka hivi leo hatuongei. Mnuno wa mwisho sababu yake nilimgundua anatembea na binti mmoja na kwa ushahidi, lakini hakujutia wala kuomba msamaha, badala yake nilinuna nae akanuna yapata mwaka mmoja sasa, tumelala kitanda kimoja hanigusi wala simgusi, mpaka sasa kakimbia nyumba, kaniacha mimi na watoto ikafikia hatua akakataa kutoa pesa ya chakula ikabidi nikamshitaki kwa wazee, ila ilishindikana, wazee wakaniambia nimpeleke mahakamani, hivi sasa anatoa ela ya chakula kwa amri ya mahakama ingawa hapendi.

Wanaume mkigombana na wake zenu muwahudumie watoto wenu maana ni wenu,baada ya kusema maneno haya kifua changu kimepumua na ninaamini kuanzia leo nitakula chakula vizuri na kuanza maisha mapya.

Usitukane wala usidharau maana ni dukuduku langu la muda sasa nitarudi kutumia id yangu ya siku zote.

Asanten

Hukulazimishwa kuolewa. Uliyataka mwenyewe. Hayatuhusu
 
Huwa nashindwa kabisa kumuelewa mwanaume mwenye tabia ya kununa nuna
 
pole sana dada yangu, yaan haya majanaume sijui yakoje.
lkn wewe liache malipo ni hapahapa duniani, kabla hapajakucha atakutafuta, I mean kabla hajafa atarudi nyumbani.
Nyumba kubwa ni nyumba kubwa tu na michepuko sio dili.

Akishafunzwa na ulimwengu atarudi kwako tena mikono ikiwa nyuma.
 
hivi mtu akiuudhi kununa ndo suluhisho? Mume hanuniwi ulikosea tangu mwanzo kama kakosa kaa nae chini mwambie 1,2,,3 sijapenda baada ya hapo kama anajirekebisha maisha yanasonga kama kawa na mwanaume asiechepuka hapa duniani ni moja ya kumi baada ya kugundua anachepuka usingenuna ungesuluhisha sidhani kama mngefika mahakamani

mi siamini kama wewe miss neddy ni msichana lazima utakuwa ni mmama mtu mzima wa busara yaani umetoa ushauri wa busara sana ningejua uko wapi ningemleta mke wangu umpe ushauri maana na yeye ni mamaa kununa
 
miss neddy nadhani nilimwelewa uzuri mkuu Nyani Ngabu hata kama sikubaliani nae kwamba MMU wote ni mazimwi ni masihara niliweka, ukichunguza kuna ka ukweli maana ushauri mwingine unaishia kushindwa kushangaa.

Binafsi nawaachia wanao nifahamu washuhudie matendo yangu, ingawa kuna wakati nakuwa mtata sana kama sina moyo wanyama vile.
waweza kuwa zimwi kwa matendo
 
Kwahiyo yaambasa mwenzako akiwa kwenye hali kama hii humsaidii kabisa ? hivi unadhnai kweli mwanaume aliyekamilka anaweza endelea baki ndani kwa mazingira kama haya ya kunyimwa "conjugal right "

Ni bahati mbaya sana hajawahi kuwa katika hali hiyo,mpaka anaondoka
 
Back
Top Bottom