Historia ya ndoa yangu

Historia ya ndoa yangu

yaambasa

Member
Joined
Oct 11, 2014
Posts
31
Reaction score
18
Wana jamvi naamini mu wazima wa afya.

Nimeolewa miaka nane iliyopita na tumebahatika kupata watoto watatu,tangu nimeolewa hiyo miaka naweza sema nimeishi na mume wangu miaka mitatu,namaanisha ki-ndoa.Maisha ya ndoa yetu naweza sema ni ya ajabu sana kwa jinsi nionavyo mimi.

Mume wangu akinikosea huwa ninatabia ya kununa ili aniombe msamaha,na kwasababu mwanaume kuomba msamaha ni ngumu huwa nahitaji basi hata kutambua tu kosa lake. Lakini kwa mwenzangu imekua ni vigumu, nikinuna nae huwa ananuna.

Miaka mitano iliyobaki tumeishi maisha ya kununiana mpaka hivi leo hatuongei. Mnuno wa mwisho sababu yake nilimgundua anatembea na binti mmoja na kwa ushahidi, lakini hakujutia wala kuomba msamaha, badala yake nilinuna nae akanuna yapata mwaka mmoja sasa, tumelala kitanda kimoja hanigusi wala simgusi, mpaka sasa kakimbia nyumba, kaniacha mimi na watoto ikafikia hatua akakataa kutoa pesa ya chakula ikabidi nikamshitaki kwa wazee, ila ilishindikana, wazee wakaniambia nimpeleke mahakamani, hivi sasa anatoa ela ya chakula kwa amri ya mahakama ingawa hapendi.

Wanaume mkigombana na wake zenu muwahudumie watoto wenu maana ni wenu,baada ya kusema maneno haya kifua changu kimepumua na ninaamini kuanzia leo nitakula chakula vizuri na kuanza maisha mapya.

Usitukane wala usidharau maana ni dukuduku langu la muda sasa nitarudi kutumia id yangu ya siku zote.

Asanten
 
Wanaume mkigombana na wake zenu muwahudumie watoto wenu maana ni wenu,baada ya kusema maneno haya kifua changu kimepumua na ninaamini kuanzia leo nitakula chakula vizuri na kuanza maisha mapya.Usitukane wala usidharau maana ni dukuduku langu la muda sasa nitarudi kutumia id yangu ya siku zote .Asanten

Duh...!!

Huna watu wa ukweli unaofahamiana nao ambao unaweza ukawaeleza masahibu ya ndoa yako hadi uje humu kwa mazimwi?

Ila cha muhimu ni wewe kujiskia vizuri. Kwa hiyo kama umejisikia vizuri kwa kufunguka humu basi haina shida.
 
hivi mtu akiuudhi kununa ndo suluhisho? Mume hanuniwi ulikosea tangu mwanzo kama kakosa kaa nae chini mwambie 1,2,,3 sijapenda baada ya hapo kama anajirekebisha maisha yanasonga kama kawa na mwanaume asiechepuka hapa duniani ni moja ya kumi baada ya kugundua anachepuka usingenuna ungesuluhisha sidhani kama mngefika mahakamani
 
unakipaji cha pekee wewe embu inunie jf miezi mitatu tuu tuone kama ni kweli unajua kununa au unaigiza
 
Duh...!!

Huna watu wa ukweli unaofahamiana nao ambao unaweza ukawaeleza masahibu ya ndoa yako hadi uje humu kwa mazimwi?

Ila cha muhimu ni wewe kujiskia vizuri. Kwa hiyo kama umejisikia vizuri kwa kufunguka humu basi haina shida.
bora mazimwi ya humu hata akitueleza hatuwezi kumsambaza kuliko ya uraiani
 
Duh...!!

Huna watu wa ukweli unaofahamiana nao ambao unaweza ukawaeleza masahibu ya ndoa yako hadi uje humu kwa mazimwi?

Ila cha muhimu ni wewe kujiskia vizuri. Kwa hiyo kama umejisikia vizuri kwa kufunguka humu basi haina shida.

Kwa upande wangu bora hawa unaowaona mazimwi kuliko hawa wanaonizunguka,amini nimepumua kweli
 
wanaume wengine hawajui kubembeleza
pole dada angu ila elewa hawa wanaume sio binadamu ni watu
 
Duh ndoa ngumu mno aise..kuomba msamaa naweza nisiombe ila kula papuchi nnayolala nayo pembeni hata kwa wiki tu siwezi vumilia..au umeongeza chumvi ww mwaka mzima ..dah..huyo jamaa kabilagani kwanza..?!
 
Ni kweli ukiongea mtu unajisikia umetua mzigo...hata ukiongelea kwenye chungu...

Ila sasa kama mmenuniana miaka 5 imekuwaje mna watoto 3?

Kingine ameondoka kuelekea wapi?

Kama ana tabia za hovyo huko alikoenda nako atatoka dima...atakuwa mtu wa kuhama hama...

Ila hapo mbona ndoa imeshakwisha...mtu kaondoka mwenyewe...hakuna ndoa hapo...lea wtoto..jipe raha kila upatapo nafasi...
 
hivi mtu akiuudhi kununa ndo suluhisho? Mume hanuniwi ulikosea tangu mwanzo kama kakosa kaa nae chini mwambie 1,2,,3 sijapenda baada ya hapo kama anajirekebisha maisha yanasonga kama kawa na mwanaume asiechepuka hapa duniani ni moja ya kumi baada ya kugundua anachepuka usingenuna ungesuluhisha sidhani kama mngefika mahakamani

Huwa nanuna lakini mwisho namuomba msamaha,moyo si wachuma jamani tumeumbwa tofauti
 
Duh ndoa ngumu mno aise..kuomba msamaa naweza nisiombe ila kula papuchi nnayolala nayo pembeni hata kwa wiki tu siwezi vumilia..au umeongeza chumvi ww mwaka mzima ..dah..huyo jamaa kabilagani kwanza..?!

Amini ninachokuambia hata wazee walishangaa, inawezaje tuishi nyumba moja kitanda kimoja hata kugusana hakuna
 
Ni kweli ukiongea mtu unajisikia umetua mzigo...hata ukiongelea kwenye chungu...

Ila sasa kama mmenuniana miaka 5 imekuwaje mna watoto 3?

Kingine ameondoka kuelekea wapi?

Kama ana tabia za hovyo huko alikoenda nako atatoka dima...atakuwa mtu wa kuhama hama...

Ila hapo mbona ndoa imeshakwisha...mtu kaondoka mwenyewe...hakuna ndoa hapo...lea wtoto..jipe raha kila upatapo nafasi...

Watoto ni watatu,wawili wamepishana mwaka mmoja, ila kumbuka nimekadiria hiyo miaka ya manunio
 
Mmmmnnnnhhhhh...kukuchiti akuchiti yeye..msamaha uombe wewe...hapana aisee...

Ukinichiti nikakununia kaogee maji ya bahari...timbwili lake kununa ni cha mtoto...ntakusimanga mpaka uone dunia chungu...

nuna mchepuko unazidisha manjonjo zaidi mafahari wawili hawakai zizi moja
 
Back
Top Bottom