Historia ya ndoa yangu

Historia ya ndoa yangu

Duh kwangu kunaungua kwa mwezangu kunateketea. Kama ukifkiria kuachana basi haina haja kuangaika na ndoa kama vile . POLE NDUGU YANGU
Wana jamvi naamini mu wazima wa afya

Nimeolewa miaka nane iliyopita na tumebahatika kupata watoto watatu,tangu nimeolewa hiyo miaka naweza sema nimeishi na mume wangu miaka mitatu,namaanisha ki-ndoa.Maisha ya ndoa yetu naweza sema ni ya ajabu sana kwa jinsi nionavyo mimi.Mume wangu akinikosea huwa ninatabia ya kununa ili aniombe msamaha,na kwasababu mwanaume kuomba msamaha ni ngumu huwa nahitaji basi hata kutambua tu kosa lake.Lakini kwa mwenzangu imekua ni vigumu,nikinuna nae huwa ananuna.

Miaka mitano iliyobaki tumeishi maisha ya kununiana mpaka hivi leo hatuongei.Mnuno wa mwisho sababu yake nilimgundua anatembea na binti mmoja na kwa ushahidi,lakini hakujutia wala kuomba msamaha,badala yake nilinuna nae akanuna yapata mwaka mmoja sasa,tumelala kitanda kimoja hanigusi wala simgusi, mpaka sasa kakimbia nyumba,kaniacha mimi na watoto ikafikia hatua akakataa kutoa pesa ya chakula ikabidi nikamshitaki kwa wazee,ila ilishindikana,wazee wakaniambia nimpeleke mahakamani,hivi sasa anatoa ela ya chakula kwa amri ya mahakama ingawa hapendi.

Wanaume mkigombana na wake zenu muwahudumie watoto wenu maana ni wenu,baada ya kusema maneno haya kifua changu kimepumua na ninaamini kuanzia leo nitakula chakula vizuri na kuanza maisha mapya.Usitukane wala usidharau maana ni dukuduku langu la muda sasa nitarudi kutumia id yangu ya siku zote .Asanten
 
Kwani hujawahi sikia ukweli una uma ndugu? Teena wanume wengine wana toa dozi mda huo huo mungu aniweke mbali na mabalaa haya
hivi mtu akiuudhi kununa ndo suluhisho? Mume hanuniwi ulikosea tangu mwanzo kama kakosa kaa nae chini mwambie 1,2,,3 sijapenda baada ya hapo kama anajirekebisha maisha yanasonga kama kawa na mwanaume asiechepuka hapa duniani ni moja ya kumi baada ya kugundua anachepuka usingenuna ungesuluhisha sidhani kama mngefika mahakamani
 
Ila una moyo dada yangu, yani kakuchiti msahama kashindwa kuomba, kanuna, mwisho wa yote kaamua kukutelekeza wewe na watoto na o bado unamuita mumeo? unasubiri nini kuivunja hiyo ndoa? au unataka yakimshinda huko arudi kuja kumalizia shida zake kwako?
 
Ni kweli wakati mwingine inatubidi tuwe na moyo,namuita mume sababu hatujapeana talaka, ila hata yakimshinda hawezi maliza shida zake tena kwangu
 
mmmh! inagusa! pole sana! kiukweli, nimejifunza kitu hapa!
 
Ila ndoa yenu kiboko Mmoja akinuna na mwenzie ananuna hakuna wa kushuka

lakini huyo mwanaume wa ajabu anakosea yeye na bado anakununia sijawahi ona,kwa kifupi ni mkorofi ,anacheat harafu hajali
,Mwenzio pia huwa na katabia ka kununa ila haizidi siku mbili uzalendo unanishinda :A S 11:
 
Haya mambo ya kusema mtu kaondoka atarudi...atakuja ku propose upya kama ntakuwa available...ni talaka tu...

Wanarudigi wakisha ukwaa...nani akuudumie ukiwa mgonjwa na starehe umekula mwenyewe...

Like Like
 
Mwanamke Mpumbavu huvunja nyumba yake mwenyewe kwa mikono yake,,huu usemi waliousema hawajakosea umeona ufahari kumfanyia visanga mmeo angalia unavyoivunja nyumba yako kwa maelezo yako kuna shoga yako unamuelezaga matatizo yako ya ndan anakushauri ujinga km huo ndoa ni kuvumiliana na kusamehane angalia sasa mpk hela ya kula unaenda kuidai mahakaman

Hapa unamtetea tu mwanaume mwenzenu
Ndoa ni watu wawili kuijenga
Huyo mwanaume ni jeuri ,msaliti na mzinzi
Kama mme ni kichwa cha nyumba kwa nini mkewe akinuna na yeye ananuna kama mwanamke
hana sifa za kuongoza familia ndio maana kiruka njia
 
Mwanamke kununa ndoa raja yake. Imagine mkeo unawasiliana nae toka asubuhi upo kazini kwa raha ukitoka job unawahi kumpitia kazini kwake immediately anakuona tu mnuno unaanza salami haitikii inavyopaswa, atabamiza milango safari yote kimyaa mkifika nyumbani anashuka km hamkuja wote. Nina yenu ndo inatufanya tutafute kwenye amani. Mdada ulinuna ukadhani utafaidi sasa yamekuathiri. Jirekebisheni
 
He aende zakee etii mwanamke huvunja ndoa kwa mikono take mwenyewe eti nimfumanie nimchekee eti nitavunja kwa mikono yangu thubutu kwani yake ya gold au anayo yeye pke take apeleke alikopeleka
 
Wana jamvi naamini mu wazima wa afya

Nimeolewa miaka nane iliyopita na tumebahatika kupata watoto watatu,tangu nimeolewa hiyo miaka naweza sema nimeishi na mume wangu miaka mitatu,namaanisha ki-ndoa.Maisha ya ndoa yetu naweza sema ni ya ajabu sana kwa jinsi nionavyo mimi.Mume wangu akinikosea huwa ninatabia ya kununa ili aniombe msamaha,na kwasababu mwanaume kuomba msamaha ni ngumu huwa nahitaji basi hata kutambua tu kosa lake.Lakini kwa mwenzangu imekua ni vigumu,nikinuna nae huwa ananuna.

Miaka mitano iliyobaki tumeishi maisha ya kununiana mpaka hivi leo hatuongei.Mnuno wa mwisho sababu yake nilimgundua anatembea na binti mmoja na kwa ushahidi,lakini hakujutia wala kuomba msamaha,badala yake nilinuna nae akanuna yapata mwaka mmoja sasa,tumelala kitanda kimoja hanigusi wala simgusi, mpaka sasa kakimbia nyumba,kaniacha mimi na watoto ikafikia hatua akakataa kutoa pesa ya chakula ikabidi nikamshitaki kwa wazee,ila ilishindikana,wazee wakaniambia nimpeleke mahakamani,hivi sasa anatoa ela ya chakula kwa amri ya mahakama ingawa hapendi.

Wanaume mkigombana na wake zenu muwahudumie watoto wenu maana ni wenu,baada ya kusema maneno haya kifua changu kimepumua na ninaamini kuanzia leo nitakula chakula vizuri na kuanza maisha mapya.Usitukane wala usidharau maana ni dukuduku langu la muda sasa nitarudi kutumia id yangu ya siku zote .Asanten

Still loarding....
 
Attachments

  • mmd.jpg
    mmd.jpg
    60.3 KB · Views: 108
  • mmm.jpg
    mmm.jpg
    43.1 KB · Views: 109
  • mmmf.jpg
    mmmf.jpg
    38.4 KB · Views: 94
  • mms.jpeg
    mms.jpeg
    11.7 KB · Views: 212
Ni kweli wakati mwingine inatubidi tuwe na moyo,namuita mume sababu hatujapeana talaka, ila hata yakimshinda hawezi maliza shida zake tena kwangu

trust me yakimshinda huko mwisho wa siku atarudi hapo hapo kwako na kujifanya kajutia sana na ni mtiifu sana
 
Mkuu labda huko kwenu... Huku kuna mwanaume alifunga ndoa na mwanamke ana watoto 6, tena wawili tu ndio wa baba mmoja na waliobaki kila.mtu na baba yake. Walipendezaje??

Ndio wanavyojipa moyo...kama wao wanavyooa hata 6 time huku wako used (mtumba) na mwanamke anaolewa sana...

Wanaume wa kiafrika wamewaaminisha wake zao kuwa wakiwaacha basi...ha ha ha...

Its just attitude...

Unaniacha leo naolewa mwakani if I want to...
Kwa kuwa sitaki bas nakuwa na partner wangu by next year...

Wewe ushangai wanawake wa kiislamu wana divorce na kuolewa number of times...

Attitude...tulishaaminishwa hatuwezi na tukaamini hivyo...
 
INASIKITISHA JAMANI SOMA HII! Baba na
mama baada ya kurudi kazini pamoja wakakuta
BARUA iko mezani SEBULENI ikisema.... "Baba
na mama, ni matumaini yangu kuwa mtasoma
ujumbe wangu huu kwenye karatasi niliyoiweka
juu ya meza, naomba msishtuke maana ni
mambo ya kawaida kwenye maisha tunayoishi,
najua mtaumia kwa vile bado nasoma na ndo
nipo kidato cha kwanza..." Napenda
kuwajulisha kwamba sasa hivi mnaposoma hii
barua sipo nyumbani, nimetoroka maana
nimegundua nina uwezo wa kujitegemea kwa
sababu mimi ni kijana mwenyewe umri wa miaka
14 na ninajua kipi chema na kipi kibaya. Tangu
mwezi mmoja uliopita nilikuwa na uhusiano na
binti mmoja aliyeitwa Rachel, mwenye umri wa
miaka 27 na kwa sasa ndo naishi naye kwenye
chumba alichopanga. Nilipokuwa nyumbani
sikuwa napata hela za kutosha ila sasa
nimeanza kushika noti za shilingi 10,000...
Msichana niliyenaye ni mzuri sana wa umbo na
ninampenda sana, amenifundisha njia za
kutafuta hela. Amenipangia kazi ya kuuza
madawa ya kulevya na yeye ikifika usiku
anaenda kuuza mwili wake, basi kila siku
tunapata hela ya kutosha, huyu mchumba
wangu ni msichana mwenye bidii, kwa siku
analala masaa 6 tu maana mwanaume yeyote
akija lazima awe naye chumbani kwa muda wa
masaa 3. Msiwe na hofu, nipo salama kabisa
na nimeamua kumwoa Rachel mana ni kila kitu
kwangu. Pia amenunua gari la kubebea mbao
kwa hiyo biashara inakwenda vizuri, Rachel
amekwenda kupima afya na amekutwa na
upungufu wa kinga mwilini, mara nyingi
namridhisha anapotaka kitu fulani, iwe kufanya
naye mazoezi ya viungo au kufanya naye
mapenzi, si mnajua unapokuwa na mgonjwa
unatakiwa kuwa naye karibu, ila mimi pia
sijihisi vizuri
maana kila saa nakohoa tu na sina uhakika
kama nimeathirika. Tumepanga baada ya miaka
miwili tutawatembelea, nadhani mpaka miaka
miwili iishe atakuwa ameshajifungua, na ni
furaha yangu mtamwona mjukuu wenu. Wazazi
wangu sina la kuongeza kwaherini Mungu
akipenda tutaonana. N.B: "Baba na mama, mimi
nipo chumbani kwangu najisomea,
mnachokisoma ni home work ya mwalimu wa
kiswahili alituambia tutunge hadithi fupi ya
kusisimua, naomba muiangalie kama kuna
makosa!"
 
Back
Top Bottom