MCHANGO WA TANGA KTK BANDARI
19 August 2026
Tanga, Tanzania
MELI YENYE UREFU WA MITA 199 IMETIA NANGA BANDARI YA TANGA
View: https://m.youtube.com/watch?v=kiusAcouFPQ
Meli yenye urefu wa meta 199 sawa takriban na viwanja viwili vya mpira imetia nanga katika bandari ya Tanga ikitokea nchini China ikiwa na mizigo mchanganyiko malori, nondo, coil bundle malighafi za viwanda vya kutengeneza mabati n.k
Sasa bandari ya Tanga inahudumia bidhaa za nchi jirani za Rwanda, Uganda, Kenya pia, Congo, Malawi na hadi nchi ya Zimbabwe wanaitumia bandari ya Tanga ya leo.
Toka nafasi za vibarua wa ajira za siku kutoka 6,000 hadi 17,000 huku maajenti wa forodha wakiongezeka toka 32 tu hadi kampuni 508 huku ma pilot wa tugboats na marine service, wafanyakazi wa TRA kukusanya kodi wakiongezeka hivyo sasa bandari ya Tanga inazidi kuchangamsha uchumi wa mkoa wa Tanga
Toka kutumia matishari mainstream kuhudumia meli kwa gharama kubwa hadi 2019 kuwekeza mlango wa meli wa kina mita 13 na ujenzi za gati kuwezesha meli kuegesha ktk gati za kisasa hivyo meli nyingi kuingia bandarini moja kwa moja kuegesha ktk bandari ya kisasa.
Kaimu Port manager wa bandari ya Tanga Bw. Peter Milanzi anatupa za ndani kuhusu bandari hii muhimu ya kimkakati toka enzi za Mjerumani kuchukua Tanganyika kama koloni lake miaka hiyo ya
1884 baada ya Berlin Conference
1884
TRC RELI NA MAMLAKA YA BANDARI, TANGA PORT
View: https://m.youtube.com/watch?v=aXiSL7ytvvU
Shirika la Reli Tanzania (TRC) la pokea vipande 17,006 vya reli pamoja na vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya takribani U$S dola za Marekani milioni 56, uwekezaji huo utaongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo kutoka bandarini kuchochea biashara na kukuza uchumi wa mkoa wa Tanga, kanda ya kaskazini , Taifa na kikanda kwa ujumla eneo hili la Afrika Mashariki, Maziwa Makuu pia kusini mwa Afrika .....
29 August 2026
Tanga, Tanzania
BANDARI YA TANGA : UCHAMBUZI WA KINA WA SHUGHULI, MAFANIKIO NA FURSA ZA KIUCHUMI
View: https://m.youtube.com/watch?v=uQl744Pr-rw
Toka Germany East Africa 1884 hadi Tanzania ya hivi leo 2026
Tanga Kitovu pia Ushindani na bandari za Maputo Mozambique, Durban South Africa, Mombasa Kenya
Source : mjengwa digital