Historia batili: Riwaya mpya na JK episode 02

Historia batili: Riwaya mpya na JK episode 02

Usiogope kupendwa wang challenge hzo, some of them 2napenda kaz so mapenz

Hahahahhaaa..nashukuru..hata ukinipendea mapenzi sawa pia..maana na mm nahitaji kupendwa eti..si mnaju Jesca alinisalti baadae??
 
Naona story tuu mzigo sioni mi nasepa zangu kitaa
 
Hahahaa dah MKUU mapumziko yakiwa marefu wanafunzi husahau somo lililopita kitakacho fuatia ni kupata zero ( 0)
 
RIWAYA: HISTORIA BATILI(Fake History)
MTUNZI & MWANDISHI: Jumaa Khatib Mdharuba(Jk)

+255718274130
mdharuba@gmail.com
www.facebook.com/khatibj
www.instagram.com/mdharubajk

EPISODE O19
★★★★★★★★★★★★★★★★
“Shem, mbona umenisusa?”
“Kwanini unasema hivyo shem? Mi mbona sijakususa?”
“Sio kawaida yako shem, wiki ya pili sasa..sijapata simu yako..una tatizo lolote?”
“Daah..hapana Sarah..nisamehe, ni majukumu tu, si unajua niko katika michakato ya kukamilisha zoezi la mirathi ya marehemu dadaako”
“Ok shem sawa..mi nikadhani kuna tatzo lolote shem, maana si kawaida yako..kama ni hivyo sawa hakuna shida”
“Ok sawa shem nashukuru kwa kunielewa.. Vipi pesa ya chakula ipo au nikutumie nyingine?”
“Ninayo ya kama siku tatu hivi..baada ya hapo nitahitaji tena..”
“Ok sawa shem..nitakutumia nyingine baadae..”
“Sawa shem asante, have a nice day”
“Ok, you too”
Khatib alimalizia maongezi haya na kukata simu.. Kwa kipindi chote alichokuwa Canada asingeweza kumpigia simu Sarah kwani hakutaka afahamu kuwa yeye yupo Canada..na mawasiliano yao makubwa yeye na Sarah yalikuwa ni kwa kupigiana simu. Hivyo basi, kama angepiga simu, ni dhahiri ingeonyesha kuwa Khatib yupo Canada kwa namba ambayo angetumia..akaona busara ni kukaa kimya, Sarah alishajaribu kumtafuta shem wake kwa namba yake ya Tanzania mara zaidi ya tatu ndani ya wiki mbili hizi, lakini hakupatikana. Mpaka leo ambapo tayari alikuwa amesharudi Tanzania.
Pamoja na kumuua Sauda, Khatib alikua bado anaendelea kumsomesha Sarah kwa kumlipia ada na kumpatia fedha za matumizi kama kawaida, kitendo ambacho pia kiliacha maswali miongoni mwa watu wengi. Habari za Sauda kufariki Sarah alizipata kupitia kwa shemeji yake huyu, na akamueleza sababu ya kifo chake kama ambavyo Dokta Mwinyi alielezea.. Na kutokana na ratiba za chuo kuwa 'tight', Sarah alishindwa kuhudhuria mazishi ya dada yake licha ya kuwa Khatib alitaka kumkatia tiketi ya ndege ili hata kama hatowahi kuzika, lakini awepo katika zile siku tatu za msiba. Ilishindikana!!
Sarah ambaye alikuwa anasoma Bachelor of Commerce katika chuo namba moja kwa ubora nchini Canada, vile vile kikiwa namba 17 katika 'rank' za vyuo vikuu vyote duniani-University of Toronto. Kiufupi Sarah alikua anasoma katika moja ya vyuo vikuu bora zaidi duniani. Khatib alilipa ada kubwa sana kwa ajili yake, na alikua akimpa fedha nyingi sana ya matumizi yake ya kila siku. Kitendo hiki kilimfanya Sarah amuamini zaidi Khatib kuliko mtu yeyote. Alitekwa kisaikolojia na Khatib..na hiyo ndiyo kawaida yake bwana huyu. Hata marehemu dadaake alipokua hai mara nyingi alikua akimpa malalamiko mengi kuhusu kutoeleweka kwa Khatib..lakini Sarah alikua hasikilizi sana maneno ya Sauda..yeye siku zote alikuwa upande wa Khatib tu. Na hii ni moja kati ya sababu zilizofanya ushahidi juu ya kuwa kweli Sauda aliuliwa kuwa mdogo mno.. Sarah kama angekua na umakini kumsikiliza dadaake nini anamwambia, angekua shahidi mzuri sana katika hili. Lakini siku zote alikuwa hataki hata kidogo kusikia mtu yeyote anamsema vibaya Khatib.
★★★★★★★★★★★★★★★★
“Hisham Omar Mikidadi..ndo hivyo jina lako?! Nimetamka vizuri??! Aliuliza Dokta yule ambaye kwa bahati mbaya hakuwa akimfahamu Hisham vizuri..
“Hivi wewe Dokta unahisi kila mtu ana muda wa kupoteza kama ulivyo wewe? Wewe hapa ni ofisini kwako, ndo panapokuingizia pesa na ukapata kula na wanao..mimi pia nina ofisi yangu nduguu..mbona unapenda kurefusha mambo?? Nipe majibu niondoke mimi..acha ujinga bana..” Hisham mara hii hakuwa tena amekaa kwenye kiti..anayasema haya akiwa kasimama na anazunguka zunguka mle ofisini kwa Dokta..kisha akaenda kuegemea meza kwa mikono yake yote miwili huku anamtizama Dokta yule ambaye alionekana kushangaa..hajawahi kukutana na 'client' wa aina hii tangu aanze kazi yake hii.
“Kaka, naomba basi ukae hapo kwenye kiti..nakupa majibu yako unaondoka..hivyo unavyofanya sio vizuri..” Dokta aliongea kwa upole sana na kumfanya Hisham atii alichoambiwa bila kuongea neno lolote.
“Majibu yanaonyesha kuwa uko poa, damu yako haina virusi”
“Dokta..be serious banaa.. Unasema niko negative?”
“Yeah..ndivyo majibu yetu yanavyoonesha..hongera sana kaka, sasa kama ulikua unajihusisha na ngono zembe huu ndo muda wa kuacha na kuangalia zaidi kuhusu maisha yako, Mungu bado anakupenda.” Dokta alianza kumshauri Hisham ambaye anaonekana baada ya majibu yale aliamua kumsikiliza Dokta.. Ni kitu ambacho hakukitegemea.
“Dokta, yaani wala usizungumzie kuhusu ngono zembe, sina kabisa hizo habari..nina mke kabisa kaka..ila haeleweki, na nimepata wasiwasi kuwa huenda ameathirika..”
“Ndio maana nikakwambia ungekuja nae hapa..ili mjue afya zenu kwa pamoja”
“Dokta, usipende kutania katika vitu serious bana..hivi unahisi ningekuja nae hapa halafu ikawa kama hivi mimi sina halafu yeye anao..unafikiri pangekalika hapa?”
“Ok haya bana..kila mtu ana jinsi anavyopokea matukio..anyway, nikutakie siku njema..ila zingatia nilichokuambia.” dokta alimaliza akaagana na Hisham kisha Hisham akaondoka.
Moja kwa moja mpaka kituo cha Angaza kilichokuwa mjini. Akafika na kwenda kupima tena..Hapa pia aliambiwa hajaathirika. Baada ya hapo akarudi tena ile maabara ya mwanzo..hapa akiwa na uhakika zaidi kuwa hajaathirika. Ilikuwa imebaki nusu saa tu kabla kituo hiki kufungwa. Hakukuta foleni yoyote. Akaingia moja kwa moja mpaka kwa Daktari ambaye alimlaki vizuri.
“Oooh boss..naona umerudi..”
“Yaah..nilisahau kitu muda ule..nikarudi nyumbani..kufika huko nako nikakutana na mambo meengi saana..ndio yakanichelewesha, ila nimekuja kucheki afya..naomba unipime kipimo kikubwa”
“Ok boss..hakuna shaka” Dokta akachukua damu ya Hisham na kufanya vipimo.. Majibu ya hapa pia yalionesha HAJAATHIRIKA.
“Yule malaya..kesho mapeema kabisa naenda nae kupima.. Ole wake sasaaa..nimkute kaathirika, atajamba cheche anye moto..Ni lazima anieleze huu mkakati wa kuniambukiza ukimwi ameutoa wapi” Hisham alijisemea mwenyewe moyoni akiwa kwenye gari lake kurudi nyumbani.
★★★★★★★★★★★★★★★★
“Mama, Khatib kanipigia simu kasema anataka kuonana na mimi..hivi yupo njiani anakuja Tanga” Hamida alimweleza Nana, mara tu alipokata simu ya Khatib.
“Anataka nini?” Aliuliza Nana ambaye bado alikuwa na hasira sana kwa familia nzima sasa.
“Kanambia anataka tuonane ili tuzungumze kuhusu maisha yetu na mtoto wetu..tena kanambia nijitahidi iwe leo maana anakuja huku kwa ajili yangu tu”
“Baradhuli mkubwa.. Analazimisha muonane leo ana 'appointment'?.. Sheenzi saana.. Hakuna kwenda kokote, tena mjibu mwambie sina muda wa kuonana na wewe unachoma mafuta yako bure..” Nana alifoka..hakutaka kabisa mwanae yule wa pakee aendelee kuwa na uhusiano na Khatib tena.
“Mama, ila mi naona nikamsikilize tu kwanza anataka kuongea nini..maana ana mwanawe huku unajua” Hamida hakutaka kukubaliana na mamaake.
“Kumbe na wewe ushaanza kuwa mpuuzi..” Nana ambaye sasa alikua amemshikia kiuno mwanae huku akimwangalia usoni katika hali ya kukasirika.
“Hebu lete hiyo simu nimjibu mimi..” Aliongeza Nana na kukwapua simu ambayo Hamida alikua ameishikilia..
“Jamani mamaa...kwanini unafanya hivyoo? Si bora umuache tu..mwenyewe nimchune hela zake..” Hamida alilalama akitaka kuchukua simu ambayo ilikuwa mikononi mwa Nana kwa wakati huu, tayari Nana alishaanza kuandika sms kwa ajili ya kumtumia Khatib.
“Unasemaje weewee..??! Pumbaav..kumbe ni hizo hela zake ndio zinakufanya uchanganyikiwe? Tena komaa..kwani hapa huli ukashiba? Huvai? Nisije nikakusikia tena ukiongea hayo maneno..nitakata pua yako hiyo” Nana aliamua kuwa mkali..kisha akamalizia kuandika ile sms na kuituma kwa Khatib.
*************************
“Sheikh..Khatib amenipa taarifa kuhusu yule mwenzie..amemwambia hana muda wa kuonana nae leo..na yeye (Khatib) yuko njiani anaelekea huko aonane nae yeye..Maana amenambia Mzee J4 hatoweza kuonana nae leo” Mama Mdharuba alikuwa akimpa taarifa Sheikh Lesangwa..
“Ok, ngoja nilifanyie kazi..nitakujuza”
“Sawa sheikh”
Zikapita dakika tano kisha Lesangwa akampigia simu Mama Mdharuba akimwambia amwambie Khatib ampigie simu Hamida sasa hivi.
*****
Baada tu ya kupewa taarifa Khatib alipiga simu kwa Hamida..simu ikapokelewa..
“Haloo..umeshafika baba Abdul? Maana mimi ndo nataka nikaoge nije, kama bado nambie tutaonana wapi ili nitangulie?” Kabla Khatib hajaongea chochote, Hamida aliongea yote haya mara tu baada ya kupokea simu.
★★★★★★★★★★★★★★★★
Don't Miss Episode 20

Maoni, Ushauri:-
+255718274130
mdharuba@gmail.com

Story nyingi pia kupitia Instagram..follow now🏃🏃👇
@jk.stories
 
Mdharuba ahsante, but unachelewesha sana hadi tunapoteza mtiririko wa hadithi
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom