Historia batili: Riwaya mpya na JK episode 02

Historia batili: Riwaya mpya na JK episode 02

ushawah kupga hata cm kuulzia nin tatzo? Au ni malalamiko ya hapa jukwaani tu kutafta ujiko? How much u paid 4 da st0ry?

Haina haja ya kupiga simu kwa sababu we' mwenyewe unatuambia sababu ya wewe kutotokea.Siku ya siku unatuachia manyoya ilhali uliahidi mwenyewe.
Ninavyolalamika hapa jukwaani nawakilisha malalamiko ya wote waliokereka na siyo kutafuta ujiko.
Kama vipi toa kitabu tununue,kwa utamu wa story usituendeshe kama unavyotaka.
 
Alianza ooh... nasoma, course ngumu sijui mnajua SUA kimefanyaje.
Mwalimu mzima anashindwa kujieleza anajikanyaga tu.
Hadithi ni yako si ungesema tu naishia hapa kwa maamuzi yangu binafsi.
Sasa unataka upigiwe simu, vituko!!!
 
Dah mbona mmefikia pabaya? Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Ni bora tuvumiliane maana hakuna anayejua la mwenzake.
 
kwa nini usipeleke hii riwaya yako kule jukwaa la matangazo madogo madogo?
 
Mdharuba nilijuwa utachemka Tu hivyo sishangai .hizi kazi wanaziweza wenyewe watu weupe ss wa afrika huwa tuna kopi. Mfano hai shigogo kipindi kile na riwaya yake raisi anampenda mke wangu hunaikumba hiyo riwaya basi na yeye alikuwa anakopi kama wewe. Acheni kukopi
 
Mdharuba nilijuwa utachemka Tu hivyo sishangai .hizi kazi wanaziweza wenyewe watu weupe ss wa afrika huwa tuna kopi. Mfano hai shigogo kipindi kile na riwaya yake raisi anampenda mke wangu hunaikumba hiyo riwaya basi na yeye alikuwa anakopi kama wewe. Acheni kukopi

sawa mkuu umeeleweka! Ntaacha kuk0pi!


Nzi akiacha ujinga wake pia anaweza akatengeneza asali.
 
Alianza ooh... nasoma, course ngumu sijui mnajua SUA kimefanyaje.
Mwalimu mzima anashindwa kujieleza anajikanyaga tu.
Hadithi ni yako si ungesema tu naishia hapa kwa maamuzi yangu binafsi.
Sasa unataka upigiwe simu, vituko!!!

unajua kubembeleza ukiwekwa ndani! Wewe wife material kbsa... Ntakupm
 
acha ujinga kwani ulilazimishwa kuweka humu?si ungebandika tangazo kule matangazo madogomadogo kuwa unauza story kama ulikuwa unataka fedha kwa kijistory chako!ebo tutolee upunguwani wako hapa

ukianza kutumia akili yako vzr badala ya matuc unaweza kug0mbea hata ubunge viti maalum pale kwenye kta yenu kupitia UWT, ndugu dullyjr
 
Kumbe mdharuba mtata mbona unawatukana wadau wakati kipindi kile ulikuwa unaenda vizuri walikupa shavu nawe ukaota vipembe ukawa mtamu kidogo.leo hii wadau wanakukataa na wanakukosoa baada ya kuona umebadilika umekuwa mtu wa blaablaaa .ww unapaniki unawapa shiti .vipi bhana toa rugha mzuri wadau wa takuherewa tu nao binadamu kama ww ..kama story imeisha funguka ni easy tu MDharuba
 
Kumbe mdharuba mtata mbona unawatukana wadau wakati kipindi kile ulikuwa unaenda vizuri walikupa shavu nawe ukaota vipembe ukawa mtamu kidogo.leo hii wadau wanakukataa na wanakukosoa baada ya kuona umebadilika umekuwa mtu wa blaablaaa .ww unapaniki unawapa shiti .vipi bhana toa rugha mzuri wadau wa takuherewa tu nao binadamu kama ww ..kama story imeisha funguka ni easy tu MDharuba

Nimepata nyepesi kuwa jamaa kaiba sehem yani copy and paste sasa huko kumekwama ndo mana

CC😡story za eddy
 
hahhahhaaaa sio kweli banaaaa... unazingua asee...
 
I will be back soon...
 

Attachments

  • mdharuba.jpg
    mdharuba.jpg
    45.5 KB · Views: 315
Kitabu cha historia batili kipo tayari,,, baada ya uchaguzi nitawaeleza wapi pa kukipata
 
STORY: HISTORIA BATILI
MTUNZI: Mdharuba, J.K.

EPISODE 26
2⃣6⃣
★★★★★★★★★★★★★
Tujikumbushe ILIPOISHIA....

Khatib ni kijana wa miaka 27 anayefahamika sana kutokana na ukarimu wake aliojijengea katika jamii. Licha ya kuwa ni kijana anayejulikana kuwa alitokea familia ya kitajiri, akiwa anamiliki yard ya magari mkoani Morogoro, lakini hii inaonekana kama ni HISTORIA BATILI tu. Ukweli hauko hivyo.!! Anamiliki pia Hoteli kubwa inayojulikana kwa jina la Euler Hotel iliyopo Msamvu Morogoro. Utajiri wake ni wa siri, kitu kilichowatia shaka watu wengi sana. Kwenye jamii alikuwa akijulikana kama mmiliki wa yard ya magari tu. Lakini utajiri wake ulionekana ni zaidi ya hapa.
Anashawishiwa kumuoa Sauda na baada ya miaka miwili katika ndoa Sauda anauawa kikatili kwa kuwekewa sumu na Khatib!!.. Anafanikiwa kumhonga Dr. Mwinyi na kutoa majibu feki pia kuhusu kifo cha Sauda..Hii ni baada ya Sauda kuonekana ameanza kufuatilia kwa karibu juu ya mienendo ya Khatib.

Pia, msichana Alice, ambaye alikuwa akitumika vibaya chini ya Afisa Usalama (Ahmed) bila yeye kujua, alijikuta akishawishika kufuatilia juu ya utajiri wa Khatib. Hatimaye Khatib anamshtukia na kumtuma Noor (ambaye alijulikana kama babaake mdogo) akafanye mahojiano na Alice.. Alice anajikuta anazidiwa kiakili na kutaka kutamka jina la aliye nyuma yake. Kabla ya kutaja jina hilo, Ahmed ambaye alipachika kifaa maalum kwa Alice kwa ajili ya kufuatilia mienendo yake, bila yeye mwenyewe (Alice) kujua, anaamua kumpiga risasi ya kichwa Alice kabla hajataja jina la aliye nyuma yake ambaye ni yeye Ahmed. Noor anapigwa na butwaa, lakini anaishia kufikishwa kituoni usiku huohuo. Khatib anaongea na mkuu wa kituo kwa kuwa anajuana nae, Noor anatoka bila hata kuandikisha maelezo yoyote. Lakini akiwa hajui nani aliyekuwa nyuma ya Alice.

Pamoja na yote hayo, Khatib ni muumini mzuri sana wa imani ya nguvu za giza (Ushirikina) ambapo anamtumia Sheikh Lesangwa, mtaalam ambaye anafahamiana zaidi na mamaake, ili kulinda siri zao na 'status' yake (Khatib) isishuke. Ila sukari inaingia shubiri pale ambapo Mzee J4 ambaye ni mjomba wa Marehemu Sauda ambaye kwa kutumia jini lake Sayyeed, anajua kila kinachoendelea kuhusu utajiri wa Khatib na historia yake ya kweli. Mzee J4 anakaribia kumuendesha Khatib atakavyo baada ya kumfahamu vizuri. Anampa masharti yake, na Khatib anaahidi kuyatekeleza huku mama yake (Mama Mdharuba) akiwa hataki kabisa hicho kitu kiendelee kutokea. Anamshauri Khatib aachane na habari za Mzee J4, asimsikilize, asimpatilize kwa ayasemayo, lakini Khatib anakuwa mbishi. Lakini baadae anakuja kugundua kuwa mama yake alikuwa sahihi. Mipango ya kumpoteza Mzee J4 (ambaye jini lake Sayyeed linampa habari zote zinazotokea kila kona) inaanza.

Ilikuwa Jumatatu jioni ambapo Khatib alikuwa akiongoza msafara uliokuwa ukielekea Mbeya kwa ajili ya kwenda kuuzika mwili wa marehemu Nira. Aliyefariki kwa UKIMWI baada ya kuambukizwa na mke wa Hisham, bi Regina ambaye anaamua kutoroka kwa mumewe kabla ya adhabu ya kifo iliyokuwa inamsubiri. Mama Mdharuba anampigia simu mwanawe na kumtaka ageuke haraka aende Tanga kwenda kuonana na Mzee J4 kabla ya kesho (Jumanne) saa 7 mchana.. Hayo yakiwa ni maelekezo kutoka kwa Sheikh Lesangwa. Na hiyo ndiyo njia pekee ya kumuangusha Mzee J4, ni lazima kukutana nae jumanne kabla ya saa 7 mchana.. Khatib anachanganyikiwa.. Hapo ageuke asiende kumzika swahiba wake, mfanyakazi wake wa siku nyingi. Tena akiwa yeye tu (Khatib) ndiye anayepajua huko kwao na yeye anajulikana.. Hakuna mtu mwingine katika msafara ule alipafahamu au yeye kufahamika huko. Khatib anamjia juu mamaake kwa kumlaumu kuwa anajipangia tu mambo na Sheikh Lesangwa bila yeye kumshirikisha... Mamaake anamjibu kwa kumwambia "Viwili vinachagulika mwanangu, ulinde 'status' yako, ama uende kumzika rafiki yako".

Je, nini kitaendeleaa..??!!!
Tulia hapohapo.. Naileta.

Je, unataka story hii kuanzia Episode 1 hadi hapa?? Bofya hapa..

HEKIMA ZA MDHARUBA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom