Hints za Rais Samia kuhusu Mafuta na Gesi Tanzania

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Contents za Rais

1. Kwa muda wote ambao nimekuwa Serikalini, tangu nikiwa Waziri, nimekuwa nasikia habari ya mradi huu wa LNG huko Lindi. Kuna wakati nikiwa Makamu wa Rais nilijaribu kuona kama naweza kusaidia kulisukuma mbele lakini lilikuwa zito kidogo na lina mambo mengi. Nilipopata nafasi hii ya kuiongoza nchi yetu, nikaazimia kwamba lazima tuutekeleza huu mradi.


2. Huu ni mradi mkubwa na wa kimkakati kwa nchi yetu. Tumekuwa ni miradi ya aina hii kwa miaka ya hivi karibuni, ikiwemo wa SGR na Bwawa la Umeme Rufiji. Mradi wa LNG una umahsusi wake kwamba sio mradi wa matumizi ya pesa bali ni mradi unaotuletea mtaji na mapato. Tutakapoukamilisha utabadilisha taswira ya uchumi wa nchi yetu.


3. Nimefarijika kwamba Wizara imekwishaliweka kwenye miliki ya Serikali eneo la mradi na kwamba kuna mpango pia wa kuanzisha Eneo Maalum la Kiuchumi (Special Economic Zone) kwenye eneo la mradi wa LNG ili kuvutia viwanda na uwekezaji mwingine. Huku ndio kufikiri kuzuri.

4. Serikali imejipanga kutoa kipaumbele maalumu kwa wakandarasi na watoa huduma wa ndani katika mradi huu. Fursa ni nyingi zikiwemo ajira rasmi na zisizo rasmi katika kipindi cha ujenzi na uendeshaji wa mradi. Hivyo basi, niwasihi Watanzania kuanza kufanya maandalizi ili kupata fursa za kushiriki katika Mradi huu.
 
Huu mradi mbona unaharakishwa sana.wananchi tuelezwe kilichomo kwenye mkataba na kama tukiona hakina manufaa bora huo mradi usitishwe .Tumeona miradi mingi inaanzishwa na kusifiwa na hawa viongozi uchwara kuwa utaleta mageuzi lakini mwisho wake Hamna kitu. Gesi ya mtwara tumeona hasara yake,migodi ya dhahabu kanda ya ziwa wanufaika ni hawa wawekezaji uchwara na viongozi wetu mafisadi.Au ndio kupigwa mnada kwa Nchi kama alivyotuambia jobu ndugai?Maana Ngorongoro tayari iko kwenye mnada.Wananchi tusikubali huu uhuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi Sana Cha muhimu ni keki yetu ilindwe vyema na wahusika..
Fanyeni mchakato mfufue na mradi wa Bandari ya Bagamoyo na Kuchimba chuma Liganga/Mchuchuma.
 
Ni hivihivi tuliletewa matumaini na gesi ya mtwara na kwamba kila nyumba itaunganishwa na gesi ila mpaka leo tunaona manyoya. Kwa nini viongozi wa pwani wanapenda kuuza rasilimali za nchi badala ya kujenga nchi?
 
Back
Top Bottom