Hili la kutoteua bodi na kutowapandisha vyeo watumishi litawagharimu Selikali ya CCM uchaguzi huu

Tila-lila2

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
653
1,058
Basi sometime huwa natoka huku Idukilo naenda hadi jijini Mwanza na siku zingine naenda Shinyanga hata Simiyu. Kwa kabiashara kangu ka kukopesha vihela na kununua mazao na biashara nyingine sometime na madini ya Mwadui basi wafanyakazi wa Selikali wamekuwa marafiki zangu sana. Basi juzi nikiwa Mwanza nikabahatika kukaa na wakurugenzi kama wa wilaya nne kutoka Mwanza, Shinyanaga na Simiyu ambao walikutana pale Mipa Hoteli kwa mambo yao na mie nikawa nawasikiliza manake mmoja ni rafiki yangu.

Niliwasikia wakilalamika zaidi kuwa kwa sasa Rais hateui kabisa wajumbe wa bodi kwa baadhi ya mashirika ya umma na wakawa wanadai pengine mpaka uchaguzi upite ili wale ambao hawatapa nafasi wapewe nafasi kwenye bodi. Walitaja taasisi kama kumi hivi ambazo hazina bodi. Mwingine hadi akafikia kusema eti JK alipondwa kuwa hakuwa anateua uongozi kwenye mashirika lkn awamu hii wamezidi.

Wakurugenzi wenyewe wakadai maofisini mwao wafanyakazi wamekuwa wakikaimu tu nafasi za ukuu wa vitengo lkn vyeo hawapewi. Mmoja akasema Halmashauri yake wakuu wa vitengo wote wanakaimu na wengine ni zaidi ya miaka miwili na hawapewi na anavyoona hata kura hawatampa Rais. Mwingine akasema hata huko kwenye taasisi watumishi wanakaimu tu na wengi wana hasira sana ukizingatia mishahara kupanda ndiyo hola.

Mmoja wa Wakurugenzi ambaye naye anasema wakuu wa vitengo wanne wanakaimu akasema CCM haitegemei kura za watumishi wao na hivyo haki zao kwenye ajira zitatatolewa kwa matakwa tu ya wenye mamlaka na sio vinginevyo.

Zaidi ya yote hata vyama vya kuwatetea wafanyakazi kwa sasa vimewekwa mfukoni na Ikulu na hata wakilalamika vipi malalamiko yao yataishia Tinde tu hayatafika Dodoma wala Dar.
 
Siku nyingine ukitaka kudanganya angalia unaowadanganya wana umri na elimu, la sivyo utaumbuka. Nimesoma mpaka mwisho nikaona makosa mengi ambayo yamekosa mpangilio ambayo yametengeneza hali ya kuonekana ni uongo.

Kwa kuandika hivi maana yake umewaanika watu kitendo ambacho mwenye akili hawezi kufanya na hivyo kufanya ulichoandika kuwa ni uongo.

Kwa kuwa umewaanika watu, watakapoulizwa juu ya hiki ulichoandika na wakakana kusema haya uliyoandika na wakakutaja, hivyo utakuwa unejianika kwa kusema uongo.
Jifunze namna nzuri ya kudanganganya siku nyingine
 
Kiwango chako cha elimu tafadhali!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani nyie wakuu hapo juu kalo MWILAPWA na thetallest mbona mnang'ang'ana na elimu ya mleta mada badala ya kujibu hija zake. Kwani yeye kasema ana elimu gani, yeye kajielezea aliyoyasikia na kueleza kwanini aliweza kusikia (vibiashara vyake vinamfanya kujuana na wakurugenzi wa wilaya) Sasa mambo ya kuhoji elimu yake yanaanzia wapi.

Jikiteni kwenye hoja yake wakuu. Je mishahara imepanda ya watumishi? Je wajumbe wa bodi wameteuliwa? Msiishie kumuataki elimu yake badala ya kuataki hoja zake
 
Siku nyingine ukitaka kudanganya angalia unaowadanganya wana umri na elimu, la sivyo utaumbuka. Nimesoma mpaka mwisho nikaona makosa mengi ambayo yamekosa mpangilio ambayo yametengeneza hali ya kuonekana ni uongo.

Kwa kuandika hivi maana yake umewaanika watu kitendo ambacho mwenye akili hawezi kufanya na hivyo kufanya ulichoandika kuwa ni uongo.

Kwa kuwa umewaanika watu, watakapoulizwa juu ya hiki ulichoandika na wakakana kusema haya uliyoandika na wakakutaja, hivyo utakuwa unejianika kwa kusema uongo.
Jifunze namna nzuri ya kudanganganya siku nyingine
Hamna hata uwongo hapo. Kukataa lazima watakataa tu kwa sababu walichokuwa wanaongea hakiwezi kukupendezesha wewe na wenye mamlaka.
 
Kwani nyie wakuu hapo juu kalo MWILAPWA na thetallest mbona mnang'ang'ana na elimu ya mleta mada badala ya kujibu hija zake. Kwani yeye kasema ana elimu gani, yeye kajielezea aliyoyasikia na kueleza kwanini aliweza kusikia (vibiashara vyake vinamfanya kujuana na wakurugenzi wa wilaya) Sasa mambo ya kuhoji elimu yake yanaanzia wapi.

Jikiteni kwenye hoja yake wakuu. Je mishahara imepamda ya watumishi? Je wajumbe wa bodi wameteuliwa? Msiishie kumuataki elimu yake badala ya kuataki hoja zake
eti bhana! Sasa darasa langu la nne nililofika pale Idukilo Primaly School mwaka 1995 linawahusu nini?
 
Hao wafanyakazi wa serikali ambao awamu iliyopita walikuwa wakijifanya watu wa system, Kikwete aliwaambia haitaji kura zao na akapita kwa kifupi hawana effect yoyote
 
Back
Top Bottom