Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 653
- 1,058
Basi sometime huwa natoka huku Idukilo naenda hadi jijini Mwanza na siku zingine naenda Shinyanga hata Simiyu. Kwa kabiashara kangu ka kukopesha vihela na kununua mazao na biashara nyingine sometime na madini ya Mwadui basi wafanyakazi wa Selikali wamekuwa marafiki zangu sana. Basi juzi nikiwa Mwanza nikabahatika kukaa na wakurugenzi kama wa wilaya nne kutoka Mwanza, Shinyanaga na Simiyu ambao walikutana pale Mipa Hoteli kwa mambo yao na mie nikawa nawasikiliza manake mmoja ni rafiki yangu.
Niliwasikia wakilalamika zaidi kuwa kwa sasa Rais hateui kabisa wajumbe wa bodi kwa baadhi ya mashirika ya umma na wakawa wanadai pengine mpaka uchaguzi upite ili wale ambao hawatapa nafasi wapewe nafasi kwenye bodi. Walitaja taasisi kama kumi hivi ambazo hazina bodi. Mwingine hadi akafikia kusema eti JK alipondwa kuwa hakuwa anateua uongozi kwenye mashirika lkn awamu hii wamezidi.
Wakurugenzi wenyewe wakadai maofisini mwao wafanyakazi wamekuwa wakikaimu tu nafasi za ukuu wa vitengo lkn vyeo hawapewi. Mmoja akasema Halmashauri yake wakuu wa vitengo wote wanakaimu na wengine ni zaidi ya miaka miwili na hawapewi na anavyoona hata kura hawatampa Rais. Mwingine akasema hata huko kwenye taasisi watumishi wanakaimu tu na wengi wana hasira sana ukizingatia mishahara kupanda ndiyo hola.
Mmoja wa Wakurugenzi ambaye naye anasema wakuu wa vitengo wanne wanakaimu akasema CCM haitegemei kura za watumishi wao na hivyo haki zao kwenye ajira zitatatolewa kwa matakwa tu ya wenye mamlaka na sio vinginevyo.
Zaidi ya yote hata vyama vya kuwatetea wafanyakazi kwa sasa vimewekwa mfukoni na Ikulu na hata wakilalamika vipi malalamiko yao yataishia Tinde tu hayatafika Dodoma wala Dar.