Tarehe 4 februari 1993 niliikanyaga Dar Es Salaam kwa mara ya kwanza. Na kilichonipeleka Dar ni masomo ya Sekondari katika shule ya Sekondari Azania. Nilipomaliza masomo yangu ya O-level, nilichaguliwa kuendelea na masomo katika shule ya Sekondari Tambaza. Na kisha Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.
Kipindi hicho majengo marefu Dsm yalikuwa machache sana. Nadhani jengo refu zaidi lilikuwa ni lile la Kitega Uchumi cha Bima (Posta), Jengo la NASACO, Faculty of Social Science, Hall 2 na Hall 5 yote ya UDSM, Jengo zilipo studio za Channel Ten (zamani lilikuwa linaitwa ghorofa la CTN na baadae Ghorofa la Ushirika.
Kipindi kile usafiri ulikuwa ni mabasi ya UDA (Kwa sehemu kubwa) na Chai maharage (KIA) kwa routes ndefu kama ya Kariakoo Chanika au Kisarawe.
Nilikuwa na ndugu yangu anaishi Pugu Kajiungeni. Asilimia kubwa kuanzia Mwisho wa Lami hadi Pugu Kajiungeni yalikuwa ni mapori tu. Enzi hizo ukiwa Kipawa, ghorofa la CTN unaliona. Kwa sasa jiji la Dar limebadilika mno. Zuri na uzuri wake ni wa kuvutia.
Kwa sasa nimehamia Arusha kikazi. Nina miaka zaidi ya minne sasa.
HOJA YANGU NI IPI?
Hoja yangu ni hii hapa..Kwa tathmini yangu, Arusha inabidi ijengwe kwa zaidi ya miaka 20 ili iifikie Dar ya mwaka 1995. Wakati huo Arusha ikijengwa, Dar iwe imesimama hata tofali moja halijengwi.