Siamini UTABIRI wa yeyote binaadam chini ya jua, ila projections kwa kutumia scietific causation au sequencing events yes. Yeyote ambaye si mjumbe wa Mungu hawezi kufanya utabiri, binadamu anaweza kufanya UBASHIRI ambao hii ni elimu inayoendana na mafunzo ya vitabu, maneno na matukio haliyopita. Je Joshua ni nabii? Kaletwa na nani? Kwa ushahidi gani? Anatumia nyaraka(suhfi) gani? Kwanini video iwe posted baada ya tukio? Kwani aseme ndege itapata ajali wakati wa take-off? Kuna take off inayochukua zaidi ya saa 1? Kuna take off inayoebdelea ktk umbali wa 35000ft? Bado mwataka kuzipeleka likizo tu akili zenu? Haya, yamekwisha haya. Kila mtu na uwezo wake wa kuyapokea yapitayo duniani. Endelea mkuu.
Huyo Joshua hana lolote. Anachota tu akili za watu ambao ama hawana akili au ni wavivu wa kufikiri.
Hana ujuzi wowote wala uwezo wowote ule wa kutabiri tukio lolote lile to a tee. Tabiri zake nyingi, kama siyo zote, huwa ni za jumla jumla mno kiasi cha mtu yeyote yule kuweza kutabiri.
Kuhusu hii ajali, yaani ukisikiliza huo utabiri wake utaishia kucheka tu. Eti anakwambia kuna nchi ya Asia, lakini hataitaja jina, ambayo itapatwa na ajali ya ndege na kuua watu 200 na kitu.
Hahahaa, sasa huo nao eti ni utabiri. Utabiri my azz. Hivi katika mwaka ni ajali ngapi za ndege huwa zinatokea? Jibu ni karibu kila mwaka lazima huwa kuna ajali za ndege hapa duniani!
Na ni ndege ngapi zenye uwezo wa kubeba watu mia mbili na kitu? Jibu ni nyingi tu.
Na bara la Asia lina nchi ngapi? Jibu ni nyingi tu. Sasa kwa nini hakutaja hata nchi, achilia mbali airline yenyewe?
Sasa hapo kuna utaalamu gani? Mimi ningemwona wa maana kama angekuwa ana nail huo utabiri wake with pin point accuracy - yaani anatoa specifics halafu tukio linatokea kweli kama alivyotabiri.
Lakini huu upuuzi wa kutoa utabiri wa jumla jumla hata mimi naweza kuutoa. Naweza kabisa kusema kabla mwaka huu haujaisha kutatokea ajali ya ndege ndogo katika moja ya nchi za Afrika Mashariki na Afrika ya Kusini na itaua watu zaidi wa 10.
Na kweli, mwezi na nane au wa tisa Precision au SA Airways inadondoka na kuua watu 15, bingo, nami ntakuwa nimeingia kwenye unabii. Hahahahaaaa.......kaazi kweli kweli.
Na hapo wala nitakuwa situmii uwezo wowote wa ajabu bali ni common sense tu na law of averages, basi. Sasa huyo Joshua ni lini kawahi kutoa utabiri na specifics za nguvu na ikaja kweli kutokea.
Hebu ona huo utabiri wake ambao watu wajinga wanadhani kuwa ndo alikuwa anaitabiria hiyo ndege ya Malaysia. Utabiri wenyewe eti aliufanya July 2013. Yaani hakuna specifc info hata kiduchu. Kilichopo ni mi broad generalities tu.
Halafu, iweje utabiri wake usiwe na time limit? Hebu fikiria, eti utabiri aliufanya mwaka jana mwezi wa saba, majuzi ndege imepotea eti watu ndo wanaona alikuwa anaitabiria hiyo ndege. Ina maana utabiri wake ni open-ended?
Ain't nobody in their right mind got time for that.