Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 39,883
- 61,610
Zamani tulikuwa tukijenga nyumba zetu, tutaweka bustani ndogo ndogo za mbogamboga na mtunda, mabanda ya mifugo midogo midogo ili utakapo hitaji chochote iwe ni rahisi kupata hapo ulipo.
Nyakati hizi hatujui ni pepo gani ametuingia, tumehama katika hizo bustani na ufugaji mdogo mdogo, na kukimbilia kwenye uoteshaji wa bustani za maua, ukoka n.k na wakati mwingine kusiliba eneo lote kwa siment au vitofali ili tusioteshe chochote. Huku ukigharamia bili za maji za kunyweshea maua yasiokuwa na faida.
Sasa, hii ni akili au kukengeuka?