Hii ndiyo ofisi ya Rais wa wanyonge

Hii ndiyo ofisi ya Rais wa wanyonge

Habari za asubuhi wanajamvi.

Jana zilisambaa picha nyingi zikimuonesha RAIS watu akiwa Ofisini akiongea na Simu aliyopigiwa na Rais Wa China, Picha hizo zilionesha Ofisi iliyojaa mafaili ambayo inayotumiwa na Rais wa Tanzania IKULU CHAMWINO, DODOMA.

Niseme hapa kuwa kiukweli Rais wetu ni Rais wa Wanyonge kwani Ofisi yake ni kama hizi za wakuu na walimu wakuu wa Shule za Msingi Zilizoko Tanzania.

Nachelea kusema kuwa hii inaonesha ni namna gani Rais wetu sio wa vitu vikubwa na ni Rais wa Wanyonge.

Hongera Rais Wetu.

View attachment 1651282
Hiyo picha inaeleza mengi sana yasiyokuwa mazuri.

Kutoa sifa kwa mwonekano huo ni kutojua maana ya kuwa na ofisi. Mnataka kuifanya Tanzania iwe na mwonekano wa jalalani?
 
Kuweka haya mapicha ni kazi ya kitengo maalum Cha habari, wanaitwa "spin doctors"kunapokuwepo na mambo yasio mazuri yanaoyoendelea nchini. Kama kuminywa kwa demokrasia, kuhonga na kuvuruga vyama vya upinzani, wakosoaji kutishiwa maisha, TRA kufunga na kuchukua pesa za watu binafsi, furaha imetoweka kwenye mioyo ya Watanzania.

Hiki kitengo huleta taarifa Ili iwafanye wananchi wasiendelee kujadili uozo unaoendelea hapa nchini na hii technic hutumiwa hata na vyombo vya habari na watu binafsi.

Diamond kapiga sing na koffie, song limebamba dunia nzima, Wakenya wakaona wivu, wakaona watupie clip ya Koffie akimpiga mnenguaji wake, tukio limetokea miaka minne iliyopita, kwanini sasa hivi liongelewe, kwanini halikuongelewa mwezi wa Tisa, kumi?
Song la whaaa limetoka!? Mara paaaaap, clip ya Koffie hiyo!!!
Wewe ni 'mtaalam' wa haya mambo.
 
Yani kwa lugha nyingine tunasema hiyo ofisi ni chafu, hayo ma document yamepangwa hovyo sana hapo wakati naamini kuna watu wanalipwa mishahara na wamesomea kazi ya utunzaji wa ofisi

Kwa ninavomfahamu Magufuli hasomi files zote hizo kwa siku moja au tatu, ameweka tu hapo kwa ajili ya jambo lake
Ninakubaliana na mawazo yako haya.

Hawa watu ni washamba sana, wanadhani watu wote ni wajinga kama wao.

Hivi kati ya hao "wanyonge" ambao ndio walengwa wa propaganda kama hizi hakuna watu werevu wa kujua kuwa haya ni maigizo?

Kuwa "mnyonge" sio kuwa mpumbavu au mjinga.
 
Jiwe amejua "kuwafurahisha"
So mmeamini hio ni ofisi yake kuu!?

Ningekua Mimi ni JPM ningewafurahisha zaidi,ningekaa kwenye kiti cha plastic,maana watanzania wepesi sana akili zao
 
Hajakataza watu kupiga picha. Amekataza watu kurushiana document za Serikali na ambazo ni confidential, kwenye mitandao ya whatsup. Hawa viongozi naomba tuwe tunawasikiliza vizuri wanapokuwa wanaongea ili kusudi inapofikia kwenye hatua ya kuwatuhumu, tuwatuhumu kwa tuhuma zilizo sahihi!
Mkuu Makanyaga , tuhuma ni tuhuma tu. Hakuna tuhuma sahihi au zisizo sahihi.
Kutojulikana usahihi wa tuhuma ndio utuhuma wenyewe.
 
Mbona mnamjaza sifa sana? Ndio maana huwa anawazingua, hebu nioneshe picha hapa ya Mwalimu wa shule ya msingi, sekondari mwenye ofisi kama hiyo.

Unajua bei ya hiyo meza hapo? Si chini ya mil pamoja ni hiko kiti hapo
Kwa hiyo unataka mwalimu wa shule ya msingi awe na ofisi kama ya Rais?
 
Habari za asubuhi wanajamvi.

Jana zilisambaa picha nyingi zikimuonesha RAIS watu akiwa Ofisini akiongea na Simu aliyopigiwa na Rais Wa China, Picha hizo zilionesha Ofisi iliyojaa mafaili ambayo inayotumiwa na Rais wa Tanzania IKULU CHAMWINO, DODOMA.

Niseme hapa kuwa kiukweli Rais wetu ni Rais wa Wanyonge kwani Ofisi yake ni kama hizi za wakuu na walimu wakuu wa Shule za Msingi Zilizoko Tanzania.

Nachelea kusema kuwa hii inaonesha ni namna gani Rais wetu sio wa vitu vikubwa na ni Rais wa Wanyonge.

Hongera Rais Wetu.

View attachment 1651282
Wewe sema tu wanyonge furniture za ofisi nzima unaweza kujenga nyumba ya adabu capripoint ,njiro,shanty town au mbweni jkt.
 
Alishawahi kus
Hiyo meza unajua bei yake wewe?

Hiyo simu unajua bei yake wewe.

Hiyo printer unajua bei yake wewe?

Hatujasema Rais awe na ofisi ya gharama saaana hapana, awe na ofisi ya kawaida tuu ina iwe imepangwa vizuri.

Kweli hiyo ni arrangement ya ofisi ya Rais? Hivi waloajiriwa kwa ajili ya kumsaidia kazi Rais wanalipwaje mishahara kwa kumuachia Rais afanye mpaka kazi za kupanga ofisi?

Rais wetu anawaza mipango mikubwa mikubwa sio aanze kujisumbua kwa kupanga panga vimeza kazi ambayo hata mlinzi wake anaweza kuifanya.
Huyo anayelala na mafaili hadi kitandani ndio unataka apangiwe ofisi? Usikute hapo aliwaambia wajaze mafaili mezani ili apige picha aonekane yuko bize
 
kutoka ...wakaribu.

Kuhusu fail huo ni utaratibu wake kila siku lazima apitie, hizo fail zimeweka muda sio muda na kila juu ya file Kuna sticker iliyoandikwa Kama ni documents za ardhi, madini, utalii, uwekezaji, maji na kadharika.

Tuache kulishana matango pori kwa kuongea uongo, hiyo meza ni 370000/=, sio million+ Kama wanavyosema wengi.

Arrangements ya fails inapangwa vizuri akishamaliza kupitia yote, Kisha zinarudishwa kwenye shelves. Hawezi kupitia fails wakati huo huo apange mwenyewe, hiyo haipo. hivyo wasaidizi wake mnawaonea bure mnaposema wanapokea mishahara ya bure.

Tukumbuke hata alivyokuwa waziri hesabu za samaki, pesa nyingi na point zilikaa kichwani sembuse kuzipitia hizo fail?

Kuna watu wanasema hata Kama ni kubana matumizi hiyo ni too much, siwashangai maana binadamu ndivyo tulivyo vingejaa vitu vya thamani Sana tungeongea kuwa ni matumizi mabaya ya pesa.

Binadamu hatuna jema hata kidogo.

Angalizo:

ogopa Sana MUNGU na technology, nyuma ya keyboard ni mbaya Sana tupunguze ukali wa maneno kwenye comments zetu.

Mnapaswa kujiongeza kwanini wizara ya aliyekuwa naibu waziri wa healthy imeanzishwa kwa purpose ipi.

Tu-comment kwa hoja na lugha rafiki kwa kila mtu.
Hiyo kutumia lugha staha ni kwa wote hata wanaccm au ni kwa wapinzani tu hasa cdm??
 
Habari za asubuhi wanajamvi.

Jana zilisambaa picha nyingi zikimuonesha RAIS watu akiwa Ofisini akiongea na Simu aliyopigiwa na Rais Wa China, Picha hizo zilionesha Ofisi iliyojaa mafaili ambayo inayotumiwa na Rais wa Tanzania IKULU CHAMWINO, DODOMA.

Niseme hapa kuwa kiukweli Rais wetu ni Rais wa Wanyonge kwani Ofisi yake ni kama hizi za wakuu na walimu wakuu wa Shule za Msingi Zilizoko Tanzania.

Nachelea kusema kuwa hii inaonesha ni namna gani Rais wetu sio wa vitu vikubwa na ni Rais wa Wanyonge.

Hongera Rais Wetu.

View attachment 1651282
Tumezoea kwa viongozi wengine kuna bendera ndogo ya taifa hapo mezani!
 
Kuna siku gazeti moja la magaharibi lilimfanyia mahojiano Nyerere.

Waandishi wale waliandika si tu mahojiano, bali pia hata mandhari ya nyumbani kwa Nyerere.

Wakasema Nyerere ni mtu simple sana.

Nyumbani kwake wafanyakazi wake wanavaa kawaida sana.

Hata juisi waliyokaribishwa wageni haikuwa na ubaridi.

Watu wa Ikulu waliona ile makala, wakawa wanaisifia sana jinsi ilivyomsifia Nyerere alivyokuwa si mpenda makuu.

Akaja mzee mmoja, nguli wa habari, Press Secretary wa Nyerere, Paul Sozigwa.

Akaisoma ile habari, akasema mnachekelea nini? Mwalimu Nyerere kadhalilishwa kwenye habari hii.

Wamesema hajui hata kuwa na watumishi wasafi wanaoweza kuandaa juisi ya baridi.

Sasa na hapa tunaweza kusifia humility wakati rais hajui hata kupanga mafaili kwenye meza!
unaona watu mpaka wanadai juice ya baridi,hiyo ni dalili ya kitu gani????

leo hii wewe unashangaa kwanini ofisi haiko kwenye mpangilio,ila siku ukiona imepangwa utaanza kuhoji pia kwanini inapangwa sana wakati jamaa hata hatembelewi.
 
Mkuu Makanyaga , tuhuma ni tuhuma tu. Hakuna tuhuma sahihi au zisizo sahihi.
Kutojulikana usahihi wa tuhuma ndio utuhuma wenyewe.
Makanyaga akienda akaiba kwenye duka la mhindi Kariakoo, halafu mhindi aliyeibiwa akaja kwako anakutuhumu wewe kuwa ndiye uliyemwibia, hizo zitakuwa ni tuhuma sahihi kwako si ndiyo?
 
Hiyo ni ofisi ya Katibu wake na picha hiyo imepigwa Februari. Msidanganywe. By the way kwa nini Rais wa China ampongeze kwa ushindi leo na si Jana?
 
Uzalendo wa kweli unaanzia kwenye HAKI... ukishindwa kusimamia haki unakosa uzalendo wala utumishi uliotukuka.

Mamlaka ya nchi inaanzia kwa wananchi... wananchi wanapata nafasi hiyo adimu ya kikatiba kupitia uchaguzi. Unapoharibu uchaguzi basi umevunja katiba kwa kuwanyima wananchi kusimika watawala wa haki wanaowataka wao...na kwa kufanya hivyo wewe unakosa uzalendo...maana msingi wa uzalendo ni Haki.
 
Habari za asubuhi wanajamvi.

Jana zilisambaa picha nyingi zikimuonesha RAIS watu akiwa Ofisini akiongea na Simu aliyopigiwa na Rais Wa China, Picha hizo zilionesha Ofisi iliyojaa mafaili ambayo inayotumiwa na Rais wa Tanzania IKULU CHAMWINO, DODOMA.

Niseme hapa kuwa kiukweli Rais wetu ni Rais wa Wanyonge kwani Ofisi yake ni kama hizi za wakuu na walimu wakuu wa Shule za Msingi Zilizoko Tanzania.

Nachelea kusema kuwa hii inaonesha ni namna gani Rais wetu sio wa vitu vikubwa na ni Rais wa Wanyonge.

Hongera Rais Wetu.

View attachment 1651282
tumepoteza mwelekeo aisee,maendeleo sio uduni au uzuri wa ofisi zetu.after all hapo alipo pengine ni nyumbani kwake sasa unategemea home kwake ofisi iweje?
 
I don't believe that is the office of the president of Tanzania. It was used for the purpose of sending certain messages to people. They cannot leave his office to be in such shambles.
 
Back
Top Bottom