Hii ndiyo ofisi ya Rais wa wanyonge

Hii ndiyo ofisi ya Rais wa wanyonge

Duh
Hiyo meza unajua bei yake wewe?

Hiyo simu unajua bei yake wewe.

Hiyo printer unajua bei yake wewe?

Hatunasema Rais awe na ofisi ya gharama saaana hapana, awe na ofisi ya kawaida tuu ina iwe imepangwa vizuri.

Kweli hiyo ni arrangement ya ofisi ya Rais? Hivi waloajiriwa kwa ajili ya kumsaidia kazi Rais wanalipwaje mishahara kwa kumuachia Rais afanye mpaka kazi za kupanga ofisi?

Rais wetu anawaza mipango mikubwa mikubwa sio aanze kujisumbua kwa kupanga panga vimeza kazi ambayo hata mlinzi wake anaweza kuifanya.
sipati picha ofisi ya secreatry itakuwaje?
 
Habari za asubuhi wanajamvi.

Jana zilisambaa picha nyingi zikimuonesha RAIS watu akiwa Ofisini akiongea na Simu aliyopigiwa na Rais Wa China, Picha hizo zilionesha Ofisi iliyojaa mafaili ambayo inayotumiwa na Rais wa Tanzania IKULU CHAMWINO, DODOMA.

Niseme hapa kuwa kiukweli Rais wetu ni Rais wa Wanyonge kwani Ofisi yake ni kama hizi za wakuu na walimu wakuu wa Shule za Msingi Zilizoko Tanzania.

Nachelea kusema kuwa hii inaonesha ni namna gani Rais wetu sio wa vitu vikubwa na ni Rais wa Wanyonge.

Hongera Rais Wetu.

View attachment 1651282
Hujaona anajenga kasri kubwa kuliko hekalu la Mfalme Suleiman kuwa Ikulu ya "wanyonge"?
 
TUNATAKA PESA KITAA! MAMBO GANI HAYA YA KUTULETEA PICHA YA RAIS AKIWA OFISINI. HAPO NDIYO MNAZIDI KUTUPANDISHA HASIRA DHIDI YA SERIKALI. ALAA!
 
Habari za asubuhi wanajamvi.

Jana zilisambaa picha nyingi zikimuonesha RAIS watu akiwa Ofisini akiongea na Simu aliyopigiwa na Rais Wa China, Picha hizo zilionesha Ofisi iliyojaa mafaili ambayo inayotumiwa na Rais wa Tanzania IKULU CHAMWINO, DODOMA.

Niseme hapa kuwa kiukweli Rais wetu ni Rais wa Wanyonge kwani Ofisi yake ni kama hizi za wakuu na walimu wakuu wa Shule za Msingi Zilizoko Tanzania.

Nachelea kusema kuwa hii inaonesha ni namna gani Rais wetu sio wa vitu vikubwa na ni Rais wa Wanyonge.

Hongera Rais Wetu.

View attachment 1651282
Dalili za nchi masikini duniani hakuna cha uyonge hapo
 
Mnasifiaga ujinga mpaka nnashangaa hiv mna familia kweli? Inamaana hizi akili ndio mnazotumia kuongoza familia zenu? Duuh kuna familia zinaongozwa na vituko
 
Kuna siku gazeti moja la magaharibi lilimfanyia mahojiano Nyerere.

Waandishi wale waliandika si tu mahojiano, bali pia hata mandhari ya nyumbani kwa Nyerere.

Wakasema Nyerere ni mtu simple sana.

Nyumbani kwake wafanyakazi wake wanavaa kawaida sana.

Hata juisi waliyokaribishwa wageni haikuwa na ubaridi.

Watu wa Ikulu waliona ile makala, wakawa wanaisifia sana jinsi ilivyomsifia Nyerere alivyokuwa si mpenda makuu.

Akaja mzee mmoja, nguli wa habari, Press Secretary wa Nyerere, Paul Sozigwa.

Akaisoma ile habari, akasema mnachekelea nini? Mwalimu Nyerere kadhalilishwa kwenye habari hii.

Wamesema hajui hata kuwa na watumishi wasafi wanaoweza kuandaa juisi ya baridi.

Sasa na hapa tunaweza kusifia humility wakati rais hajui hata kupanga mafaili kwenye meza!
 
Duh! Ofisi kama ya Mwalimu mkuu wa Secondary. Hata kubana matumizi sio hivo.
 
Nimeongea Na Waziri Wa Ardhi Atutafutie Kiwanja Sehemu
Pesa Tutakazoziokoa Geita Kwa DED, Tumjengee Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Ofisi Nzuri Sana Tena Ya Kisasa
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Nasema Uongo Ndugu Zangu
 
Duh! Ofisi kama ya Mwalimu mkuu wa Secondary. Hata kubana matumizi sio hivo.
Unajua Hata Kama Ni Samaki Unachakata Itaozea Mkononi Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Katika hiyo picha kosa kubwa la kwanza ni shati la oversize
 
Kuna siku gazeti moja la magaharibi lilimfanyia mahojiano Nyerere.

Waandishi wale waliandika si tu mahojiano, bali pia hata mandhari ya nyumbani kwa Nyerere.

Wakasema Nyerere ni mtu simple sana.

Nyumbani kwake wafanyakazi wake wanavaa kawaida sana.

Hata juisi waliyokaribishwa wageni haikuwa na ubaridi.

Watu wa Ikulu waliona ile makala, wakawa wanaisifia sana jinsi ilivyomsifia Nyerere alivyokuwa si mpenda makuu.

Akaja mzee mmoja, nguli wa habari, Press Secretary wa Nyerere, Paul Sozigwa.

Akaisoma ile habari, akasema mnachekelea nini? Mwalimu Nyerere kadhalilishwa kwenye habari hii.

Wamesema hajui hata kuwa na watumishi wasafi wanaoweza kuandaa juisi ya baridi.

Sasa na hapa tunaweza kusifia humility wakati rais hajui hata kupanga mafaili kwenye meza!
Katika karne ya 21 kwenye nchi maskini kama Tanzania, unazungumzia eti kiongozi kusifiwa tena na Wazungu??? Sisi hatutaki kiongozi wa sifa za kitoto --- tunataka huduma za mawasiliano, barabara, maji, umeme, afya, shule na SGR.

Niongeze volume, au???
 
Habari za asubuhi wanajamvi.

Jana zilisambaa picha nyingi zikimuonesha RAIS watu akiwa Ofisini akiongea na Simu aliyopigiwa na Rais Wa China, Picha hizo zilionesha Ofisi iliyojaa mafaili ambayo inayotumiwa na Rais wa Tanzania IKULU CHAMWINO, DODOMA.

Niseme hapa kuwa kiukweli Rais wetu ni Rais wa Wanyonge kwani Ofisi yake ni kama hizi za wakuu na walimu wakuu wa Shule za Msingi Zilizoko Tanzania.

Nachelea kusema kuwa hii inaonesha ni namna gani Rais wetu sio wa vitu vikubwa na ni Rais wa Wanyonge.

Hongera Rais Wetu.

View attachment 1651282
Samahani kwa kuwa a bit irrelevant, hivi hili neno "nachelea" maana yake nini hasa na linatumikaje?
 
Kama ni kweli hapa Jiwe yupo ofisini, ni vyema pia tukaamini kwa nini kama nchi hatusongi. Katika ulimwengu wa kidigitali kama huu tuliopo bado kiongozi mkuu wa nchi unamjazia mafaili lundo namna hiyo? Kwamba hanan wasaidizi wa kuyasoma kisha wao kwenda kum brief? Kila faili alisome yeye. Poor my dear donor country
Unajua Job Descriptions za President wa JMT???

Tuanze hapo Mr Much Know
 
Samahani kwa kuwa a bit irrelevant, hivi hili neno "nachelea" maana yake nini hasa na linatumikaje?
1. chelea = sita (kufanya jambo fulani)

Nachelea kusema kwamba Kiswahili ni lugha bora ila wazawa wengi wanakimbilia Kiingereza. (Means jambo zito ambalo usingependa kusema moja kwa moja; sasa unajifichia kwenye "nachelea" ili kuzuia mathalani unwarranted reactions za wasikilizani)

2. chelea = dekeza

Mchelea (mdekeza) mwana kulia, hulia yeye.
 
Habari za asubuhi wanajamvi.

Jana zilisambaa picha nyingi zikimuonesha RAIS watu akiwa Ofisini akiongea na Simu aliyopigiwa na Rais Wa China, Picha hizo zilionesha Ofisi iliyojaa mafaili ambayo inayotumiwa na Rais wa Tanzania IKULU CHAMWINO, DODOMA.

Niseme hapa kuwa kiukweli Rais wetu ni Rais wa Wanyonge kwani Ofisi yake ni kama hizi za wakuu na walimu wakuu wa Shule za Msingi Zilizoko Tanzania.

Nachelea kusema kuwa hii inaonesha ni namna gani Rais wetu sio wa vitu vikubwa na ni Rais wa Wanyonge.

Hongera Rais Wetu.

View attachment 1651282
kutoka ...wakaribu.

Kuhusu fail huo ni utaratibu wake kila siku lazima apitie, hizo fail zimeweka muda sio muda na kila juu ya file Kuna sticker iliyoandikwa Kama ni documents za ardhi, madini, utalii, uwekezaji, maji na kadharika.

Tuache kulishana matango pori kwa kuongea uongo, hiyo meza ni 370000/=, sio million+ Kama wanavyosema wengi.

Arrangements ya fails inapangwa vizuri akishamaliza kupitia yote, Kisha zinarudishwa kwenye shelves. Hawezi kupitia fails wakati huo huo apange mwenyewe, hiyo haipo. hivyo wasaidizi wake mnawaonea bure mnaposema wanapokea mishahara ya bure.

Tukumbuke hata alivyokuwa waziri hesabu za samaki, pesa nyingi na point zilikaa kichwani sembuse kuzipitia hizo fail?

Kuna watu wanasema hata Kama ni kubana matumizi hiyo ni too much, siwashangai maana binadamu ndivyo tulivyo vingejaa vitu vya thamani Sana tungeongea kuwa ni matumizi mabaya ya pesa.

Binadamu hatuna jema hata kidogo.

Angalizo:

ogopa Sana MUNGU na technology, nyuma ya keyboard ni mbaya Sana tupunguze ukali wa maneno kwenye comments zetu.

Mnapaswa kujiongeza kwanini wizara ya aliyekuwa naibu waziri wa healthy imeanzishwa kwa purpose ipi.

Tu-comment kwa hoja na lugha rafiki kwa kila mtu.
 
Back
Top Bottom