Gembe
JF-Expert Member
- Sep 25, 2007
- 2,483
- 156
wakati Rais Kikwete anaingia madarakani alijibebesha mizigo tisa,Je ni ipi kati ya aliyojibebesha wakati anazindua bunge la Jamhuri ya muungano pale Dodoma ambao ameweza kuufikisha panapotakiwa
Ifuatayo ni mizigo hiyo tisa
Mzigo wa kwanza alioamua kukijitwisha ni ule wa kukiri na kueleza bayana kwamba tatizo la kuwapo kwa rushwa kubwa (grand corruption) ni jambo ambalo atakabiliana nalo kwa nguvu zake zote, akianzia na hatua ya kupitia mikataba yote ambayo serikali inaingia na taasisi za kigeni.
Kwa kukiri kwake kwamba, rushwa kubwa inayohusisha viongozi ni tatizo ambalo halina budi kushughulikiwa kikamilifu, Kikwete alihitimisha hoja ambazo zimekuwa zikitolewa na wananchi na asasi mbalimbali za ndani na nje kuhusu kuwapo kwa rushwa hiyo ambayo serikali ya awamu ya tatu haikuwahi kuiweka bayana na kukubali kuwapo kwake.
Katika hilo, aliwatadharisha viongozi wote katika serikali yake kuwa waaminifu na kutojiingiza katika mtego wa kupokea rushwa kubwa kwa tamaa ya kupata utajiri wa haraka haraka na akahitimisha kwa kusema; "Tusijekulaumiana mbele ya safari".
Mzigo wa pili ambao aliahidi kuubeba kwa kufikia hata hatua ya kuitisha mdahalo au mjadala wa kitaifa ulikuwa ni ule alioupa jina la Mpasuko wa Zanzibar wa kati ya Wapemba na Waunguja, hoja ambayo Mwalimu Nyerere katika ile hotuba yake ya mwaka 1995 aliugusia.
Mzigo wa tatu unaoelekeana na huo alioahidi kuushughulikia pia ni ule wa matatizo yaliyopo katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao alifikia hatua ya kuahidi kuunda wizara itakayokuwa Ofisi ya Makamu wa Rais itakayopitia masuala yote yanayoleta chokochoko na kuzusha malalamiko kutoka pande zote mbili.
Mzigo wa nne ni ule wa mmomonyoko wa maadili ya kitaifa, umoja na mshikamano wetu ambao huo aliamua kurejea katika falsafa zilizobuniwa na Serikali ya Awamu ya Kwanza katika kuupatia ufumbuzi kabla haujawa tatizo kubwa.
Katika hilo, Kikwete alieleza haja ya kurejeshwa tena kwa Shule za Sekondari za Kitaifa moja katika kila wilaya au mkoa ambazo zitakuwa zikichukua wanafunzi kutoka mikoa yote ya Tanzania na pia akarejea umuhimu wa kurejeshwa kwa Jeshi la Kujenga Taifa mambo ambayo kimsingi yalisaidia sana katika kujenga misingi ya umoja na utaifa wa Tanzania.
Kikwete alijitwika mzigo wa sita wa kukabiliana na tatizo la udini ambalo pia limeanza kulinyemelea taifa kama alivyowahi kuonyesha Baba wa Taifa pia. Katika hilo, Rais alilielezea hilo kwa tahadhari kwa kuzitaka shule zinazoanzisha na mashirika ya dini (zisizo za seminari) kujenga utaratibu wa kuwachukua wanafunzi wenye imani tofauti lengo likiwa kutoa fursa sawa ya Watanzania wote kielimu.
Mzigo wa saba aliuzungumzia na kutoa maelekezo ya namna atakavyoukabili ni ule unaohusu miiko ya uongozi na hususan ile inayohusiana na kuzingatia maadili ya utendaji na hususan uaminifu. Katika hilo, Kikwete aliahidi kukabiliana ipasavyo na viongozi wote wenye uchu ya kupata utajiri wa haraka haraka hata kufikia hatua ya kuliibia taifa kwa lengo la kujilimbikizia mali, nia ikiwa ni kupata utajiri wa haraka haraka kwa njia zisizo halali.
mzigo wa nane ni wa kuokoa raslimali maji na uhifadhi wa mazingira kwa kuhakikisha kwamba analifanya hilo kama mkakati mahususi kabisa wa kulinusuru taifa hili kukabiliwa na mgogoro mkubwa wa ukosefu wa maji katika kipindi cha miaka 10 ijayo iwapo hatua za dharura na mahususi hazitachukuliwa.
mzigo wa tisa ambao Kikwete aliuzungumzia ulikuwa ni ule wa kukabiliana na pengo kubwa kati ya matajiri na maskini, jambo ambalo limekuwa likipigiwa sana kelele na watu wengi akiwamo Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Katika hilo, Kikwete alisema serikali yake haitawapokonya mali matajiri, bali itawajengea maskini uwezo wa kujikwamua kimapato.
Naomba kuwasilisha
Kwa hisani ya Fikra Pevu