Hii ndio sababu iliyonifanya niache kuvaa nguo za ndani (vest na boxer)

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,718
10,214
Maisha ni fumbo kubwa lililojaa somo kubwa iwapo tu utasimama thabiti na ukiwa na msimamo chanya na kuwa mtu unayependa kujifunza kupitia na magumu unayoyapitia.

Nilipoingia kwenye biashara na kuanza kushika vijihela ambavyo nilikuwa sijawahi kuvishika kabla, basi na tabia mpya zikaanza. Wanawake, Pombe na nyama choma ndio yakawa maisha yangu.

Mwalimu wangu wa biashara (Mentor/ Guru) akawa ananikaripia na kunigombeza sana kutokana na tabia zangu hizi mpya. Akaniambia hizi ni tabia zinazofungua mlango wa kuniingiza kwenye ufukara.

Wakati nakatazwa niachane na tabia zangu mbaya performance ya biashara nayo ikashuka, usiku nikawa kama popo, nahangaika kwenye makumbi ya starehe na wanawake.

Nikaja kupata msichana ambaye nikahisi ndiye atakayekuja kuwa mke wangu. Akawa free kuja kwangu muda atakao na mimi nikawa free kwenda kwake, tulikuwa tumebadilishana funguo.

Sasa ikatokea siku moja nimekula supu Break Point ya Makumbusho zamani zile, nikashusha na bapa kubwa la Konyagi. Nikazima simu nikaona sehemu salama ya mimi kujificha bila kusumbuliwa na Guru ni kwenda nyumbani kwa demu wangu.

Kule nikapata muda mzuri sana wa kulala, pombe ziliponiisha, mida ya saa 11 jioni, nikaingia bafuni kuoga. Baada ya kuoga nikavaa fresh, bahati mbaya nikadondoshea ufunguo wa gari pembeni ya kitanda.

Nilipovuta kitanda ili niifikie funguo kwa urahisi nikakutana na mfuko wa nylon ile iliyopigwa marufuku. Nikaingiwa na roho ya udadisi nikasema niufungue. Mle ndani nikakuta kuna boxer zangu 2 na vest moja, karatasi imeandika majina yangu matatatu, na majina yote ya mama yangu na tarehe yangu ya kuzaliwa.

Kulikuwa na mayai viza yameandikwa kwa kiarabu kwa wino mwekundu. Pia kulikuwa na kafatasi ina michoro michoro na maandishi ya kiarabu.

Kulikuwa na hirizi mbili, moja kubwa nyekundu na nyingine ndogo nyeusi. Nikakibeba kifuko kile, nikakipiga picha na kumtumia mamsapu kwa WhatsApp.

Tangu siku hiyo sivai kabisa nguo za ndani.
 
Back
Top Bottom