Hii ndio Kanda ya Kaskazini

Hii ndio Kanda ya Kaskazini

Nani alie kwambia wasukuma ni wavivu? Kwa taarifa yako msukuma ndio anaweza kuwa mtu mwenye pesa zaidi ya makabila yote, usukumani kuna diamond, dhahabu, ng'mbe, mbuzi, mchele nk.Fanya tathmini pembuzi ndugu.huko uchagani kuna nini zaidi ya ndizi na kahaw na mlima kmnjr, hivi kuna kijana wa kitanzania anaewaza akatafute maisha moshi?sijawahi muona ila wachaga tu kukimbia kwao mnaongoza mkifuatiw na wamakonde japo wana ardhi kubw.Ukweli ni kwamba moshi hakuna rasilimali chochevu kama mkoa wa mby, Morogoro, Njombe, Rukwa, pwani nk.Hata miundombinu iliojwngw huko imejengwa na serikali unasifia utazani wewe ni mkenya, kikwete alileta mfumo wa kiwaondoa katika kujipendelea kielimu, shule za kata zimekata mzizi wa fitina na takwimu zinaonesha wasukuma ndio wengi vyuoni kuliko makabila yote, miaka kumi inayo watatawala kila sekta na wengi wao husoma zaidi sayansi kwa sababu wanaakili kuliko wachaga.

Darasa la chuo kikuu wanafunzi tulikua 80, nusu ni wachaga
 
Habari Wakuu!

Kanda ya kaskazini inajumuisha Mikoa mitatu ambayo ni mkoa wa Arusha( na Manyara), Tanga na Kilimanjaro. Mikoa hii ni moja ya mikoa iliyobarikiwa karibu kila kitu. Nathubutu kusema kanda ya kaskazini ni zaidi ya nchi ya maziwa na asali. je si kanda ya kaskazini yenye mali asili nyingi kupita kanda yoyote ile. Mali asili zilizopo huko huweza kuingia katika top ten kiulimwengu.

Nikianza na Rasilimali watu. Kanda hii kuna makabila mbalimbali yenye mila na destu zao. Wapo Wachaga, Wapare, Wamasai, Wasambaa, wadigo, wazigua, wabondei, Wameru, Wambulu, wambugu n.k. Kila kabila linavijikabila ndani yake. Hakuna sifa yoyote kiulimwengu ambayo watu wa kanda hii hawana. Kama ni wanawake wazuri hii ndio kanda iliyobarikiwa kuliko kanda zingine. Watoto kutoka Tanga, Watoto kutoka Manyara ndio usiseme kabisa.

Kwa habari ya elimu kanda hii wanatisha. Karibu kila familia kuna zaidi ya watoto wawili wenye shahada. Kila ukoo unawatu wenye shahada mbili au hata tatu. hii tafsiri yake ni kuwa watu kutoka huko wapo vizuri kielimu. Tofauti na kanda nyingine au hata nchi nyingine ambazo unaweza kukuta kwenye familia hakuna hata mwenye elimu ya kidato cha sita. Kutokana na watu kuwa na elimu katika kanda hii ndio maana hata maendeleo yao si haba.

Kwa habari za miundo mbinu kama barabara, reli, viwanja vya ndege, bandari n.k. Kanda ya kaskazini imesheheni. Kuna kiwanja kimoja cha ndege cha kimataifa(KIA) ambacho kinaruhusu ndege kutoka mataifa ya nje kufika kanda hiyo. Pia vipo viwanja vya ndege vidogo vidogo. Ipo bandari ya Tanga ambayo Kanda hii inaweza kupokea meli kutoka sehemu yoyote duniani. barabara ya lami kiasi wamejitahidi ukilinganisha na kanda zingine na nchi zingine. Reli nayo ipo. Nini kimebakia kwenye habari ya miundo mbinu. Jibu ni hakuna.

Huduma za kijamii kama Zahanati, Hospitali, Shule, Vyuo vya ufundi, Vyuo vikuu, Umeme, huduma za kibenki, Makanisa, Misikiti, Vyombo vya habari n.k. Ipo hospitali kubwa ya KCMC ambayo ni moja ya hospitali kongwe na bora katika nchi hii. Kila wilaya kuna Zahanati kama si hospitali ndogo. Vyuo vya ufundi (VETA) Karibu kila kata kama si wilaya vipo. Vyuo Vikuu vinavyotoa kozi mbalimbali vipo. Kanda hii ndio kanda pekee yenye shule nyingi kuliko kanda yoyote hapa duniani na hata baadhi ya mikoa ya nchi fulani barani Afrika. Usishangae katika kata moja kukawa na shule za msingi hata 10, Shule za sekondari tano. Hii ni kusema kuwa wanayohaki kupata elimu wengi. Umeme upo karibu kila kijiji. Vyombo vya habari zikiwemo Redio kadha wa kadha. Huduma za kibenki kila wilaya na hata baadhi ya kata kuna vituo vya kutolea pesa. Huduma za mawasiliano ipo, kila mtandao unashika vizuri. Hakuna tabu ya kufanya miamala ya simu.\

Wasomi na Wataalamu katika kanda hii ni wengi sana. Ndio kanda pekee inayoongoza kwa kuwa na wasomi wengi na wataalamu wengi. Wanasheria, Madaktari, Waalimu, Wahandisi, Wakandarasi, Wanasiasa, Wachungaji, Wahasibu, wataalamu wa mambo ya fedha, Wataalamu wa mawasiliano na kompyuta, Madereva, Makanika n.k. kwenye nchi hii kila fani niliyoitaja hapo wengi wao wanatoka Kanda ya kaskazini.

Rasilimali kama Mbuga za wanyama, Madini, Mlima Kilimanjaro, Bwawa la Nyumba ya Mungu, Mapango ya ambani, Bahari ya Hindi, Maziwa na mito, Ardhi kubwa yenye Rutuba, Tabia ya nchi nzuri, Miti ya matunda n.k. Kilichokosekana hapa ni Gesi na mafuta tuu. lakini hayo mengine yapo kanda ya kaskazini.

Wasanii na watu maarufu. Kanda ya kaskazini ndio kanda pekee yenye wasanii lukuki wanaoeleweka. Wasanii wengi na watu maarufu wengi hutoka kanda hii. Wengi hutoka TANGA, ARUSHA NA MOSHI. Hivyo ni kusema Kanda hii ni moja ya kanda iliyobarikiwa kupita zote.

Ndio Kanda pekee ambayo watu wake wanapenda kwao na kujivunia kwao. Ni watu ambao hawasiti kujitambulisha popote pale. Mtu hata asipoulizwa hujikuta akisema kuwa kwetu ni Moshi, mara home ARA chuga, ooh kwetu Tanga. Hii huifanya kanda hii kuonekana inaubaguzi na umimi kutokana na hulka ya majigambo.

Matajiri na Wafanya biashara wakubwa. Hakuna ubishi kuwa kanda ya kaskazini inaongoza kwa kuwa na watu wenye mpunga na jala la kufa mtu. Atakayebisha ni yule asiyeijua nchi hii vizuri au ambaye hajatembea mikoa mingi katika nchi hii. Karibu kila kata kwenye majiji makubwa hapa nchi huwezi kukuta matajiri kumi bora wa kata hiyo alafu usikute watano wanatoka kanda ya kaskazini. Si Dar es Salaam, si Mbeya, si Mwanza popote pale lazima matajiri wanne au watano katika kata hizo lazima watoke huko kaskazini. Kanda hii inaheshimu pesa sana. Watu wake hawaoni aibu kufanya hata ni shughuli ya kuuza nyanya bila kujali mtu huyo kaenda shule au hajaenda. Wanachoangalia je kuna mpunga basi.

Majambazi, mafisadi na wahujumu uchumi. Ndio kanda pekee inayoweza kutoa Mafisadi, majambazi na wahujumu uchumi kushinda kanda yoyote hapa nchini. Ujambazi wa kimataifa pia umefanya na watu wa kanda hii. Si ajabu mtu kutoka Arusha akienda Kenya kupiga tukio la kijambazi. Hii imepelekea kanda hii kuogopwa na kutokuaminiwa kabisa na kanda zingine hasa kwenye ishu za pesa. Ndio Kanda pekee ambayo hawataki mchezo na mali zao. Si rahisi umdhulumu mtu kutoka kanda hii. Ukisikia kesi ya kuku ng'ombe anauzwa ili kuendesha kesi basi huko kaskazini ndio mtindo.

Ndio Kanda pekee ambayo hawakatai watoto. Na si rahisi kuchukua damu yao.

Ndio kanda pekee inayojiona Superior kuliko kanda zingine. Mtu kutoka huku hata kama hajaenda shule huwezi kumuendesha na kumdharau eti kisa wewe umeenda shule au unavijipesa.

Ikumbukwe kwamba mtu yeyote anaweza kuwa kanda ya kaskazini iwe kwa damu au kuzaliwa huko.

Nawasilisha!
Mimi nimekaa Moshi karibu miaka sita sijaona chuo cha VETA kwenye kila kata
 
Nasema wanyantuzu ni wakush sawa na wachaga tuu uangalie mambo yao kwa makini
 
Hivi Haya mambo bado tu.Eti kanda!!Hizo mada za bwenini kwenu unazileta hapa.
 
Kujinadi kwa wito wa ukabila,ukanda, rangi ya mwili nk ni wito wa "kijahiliya" ni wito wa kijinga. Sijui mtu ananufaika na nini akijinadi kwa wito wa namna hiyo.
Labda hujamuelewa mtoa mada mkuu mkuu,
Binafsi sijaona ubaya wa uzi huu
Ni kama kuwashindanisha watoto wako wanaosoma shule tofauti za viwango sawa kwa mtihani mmoja
Just kuwapa changamoto sio kiwatenganisha
 
Mnachokifanya sasa hao jamaa wa kaskazini walikifanya miaka ya 60 na 70's

Huu ni ushindani mzuri sio kurogana tuuu

Keep the fire burning!
Naona watu na Kanda yao "keep the fire burning" hivi hiki kiingereza watu wa kaskazini ndo huwa mnamezeshwa na watalii sio "nikiona mtu anajisifia anakotoka namwona waheed kabsa,,, jisifie kwa kile ulichokifanya wewe na kwa trend inavyoenda mnaenda kupoteza crown kwa kuendekeza ulevi usiofaa,, maendeleo yaliyopo kaskazini mengi yalifanyika miaka ya nyuma kipindi tunafuata sukari moshi,, kwa sasa upepo umebadilika na Hali hii baada ya miaka 15 tu sijui nani anajisifia eti Kanda gan unatokea,,, huu ujinga uwatoke na pombe muache mnapata hepatitis kijinga tu mtu Ana hela anakuja Ana liver failure,, sasa unadhan sisi tutaweka liver mpya shauri ya pombe yao
 
Kila kanda tz inakitu cha pekee cha kumzidi kanda nyingine

HIV UNAWEZA KUFANANISHA UWEPO WA MADINI KANDA HIYO NA KANDA YA ZIWA??

HV UNAWEZA KUFANANISHA UWEPO CHAKULA KWA WINGI KANDA HIYO NA YA NYANGA ZA JUU KUSINI??

BINAFSI NAONA MMETEKA KWENYE UTALII TUU COZ YA MLIMA NA MBUGA ZA WANYAMA

Kama uoto wa arusha mbona haifiki kwa mtwara

MLICHO JALIWA KINGINR mnapenda sifa kuliko wa haya HVUKITOA WACHAGA KABILA GANI LINAWASOMI KAMA ULIVYO SEMA??
 
Ili nchi iwe imara kabisa kisiasa na kiuchumi ni lazima pawe na mamlaka za kikanda na kila kanda iwe inasimamia maendeleo yake kwa kasi.
 
Back
Top Bottom