Hii ndio Kanda ya Kaskazini

Hii ndio Kanda ya Kaskazini

Tunachofanya sasa ni kutapakaa Tanzania yote huku vijana tukipambana mashuleni, vyuoni. Tutasomana tu

Mimi kiasili ni mtu wa Tabora. Naelewa ninachokiandika. Kanda ya kaskazini wanazombinu nyingi za kuendelea kuwa juu kwa karne nyingi zaidi. Wakati nyie mnawaza hayo wenzenu wameshatapakaa nchi za nje miaka mingi iliyopita. Sasa ikiwa nyie bado mnawaza kujenga vyoo vya nyumba, sijui kula mboga za kondeni wenzenu walitoka huko miaka ya 60.

Naongea haya ili niwatie hasira mutafute maendeleo ili taifa letu liendelee. Kwa kifupi huko bado sana
 
Me kukubali juu kusini coz kule kun wanaume imara na weny akili kulipga jesh la kijerman leny watu 300 kwa mkuki mkwawa noma sana


Kwa hilo kweli tuwape hongera sana. Lakini dunia hairudi nyuma Mkuu. Dunia inaenda mbele. Nyie mnajivunia watu waliokufa poleni sana. wenzako wanajivunia vilivyohai
 
Kanda hii hakuna kitu kinachukiwa kama chama cha mapinduzi yanii kuna watu huku wanaamini kabisa CCM ni alama ya umasikini na ujinga Sijui kwanini!??Yani ukiwa ccm wanakuona Wewe ni Madifi ( muulize mchaga madifi ni nini)
We usitamke tena hilo jina, maana yake ni mbolea.
 
Habari Wakuu!

Kanda ya kaskazini inajumuisha Mikoa mitatu ambayo ni mkoa wa Arusha( na Manyara), Tanga na Kilimanjaro. Mikoa hii ni moja ya mikoa iliyobarikiwa karibu kila kitu. Nathubutu kusema kanda ya kaskazini ni zaidi ya nchi ya maziwa na asali. je si kanda ya kaskazini yenye mali asili nyingi kupita kanda yoyote ile. Mali asili zilizopo huko huweza kuingia katika top ten kiulimwengu.

Nikianza na Rasilimali watu. Kanda hii kuna makabila mbalimbali yenye mila na destu zao. Wapo Wachaga, Wapare, Wamasai, Wasambaa, wadigo, wazigua, wabondei, Wameru, Wambulu, wambugu n.k. Kila kabila linavijikabila ndani yake. Hakuna sifa yoyote kiulimwengu ambayo watu wa kanda hii hawana. Kama ni wanawake wazuri hii ndio kanda iliyobarikiwa kuliko kanda zingine. Watoto kutoka Tanga, Watoto kutoka Manyara ndio usiseme kabisa.

Kwa habari ya elimu kanda hii wanatisha. Karibu kila familia kuna zaidi ya watoto wawili wenye shahada. Kila ukoo unawatu wenye shahada mbili au hata tatu. hii tafsiri yake ni kuwa watu kutoka huko wapo vizuri kielimu. Tofauti na kanda nyingine au hata nchi nyingine ambazo unaweza kukuta kwenye familia hakuna hata mwenye elimu ya kidato cha sita. Kutokana na watu kuwa na elimu katika kanda hii ndio maana hata maendeleo yao si haba.

Kwa habari za miundo mbinu kama barabara, reli, viwanja vya ndege, bandari n.k. Kanda ya kaskazini imesheheni. Kuna kiwanja kimoja cha ndege cha kimataifa(KIA) ambacho kinaruhusu ndege kutoka mataifa ya nje kufika kanda hiyo. Pia vipo viwanja vya ndege vidogo vidogo. Ipo bandari ya Tanga ambayo Kanda hii inaweza kupokea meli kutoka sehemu yoyote duniani. barabara ya lami kiasi wamejitahidi ukilinganisha na kanda zingine na nchi zingine. Reli nayo ipo. Nini kimebakia kwenye habari ya miundo mbinu. Jibu ni hakuna.

Huduma za kijamii kama Zahanati, Hospitali, Shule, Vyuo vya ufundi, Vyuo vikuu, Umeme, huduma za kibenki, Makanisa, Misikiti, Vyombo vya habari n.k. Ipo hospitali kubwa ya KCMC ambayo ni moja ya hospitali kongwe na bora katika nchi hii. Kila wilaya kuna Zahanati kama si hospitali ndogo. Vyuo vya ufundi (VETA) Karibu kila kata kama si wilaya vipo. Vyuo Vikuu vinavyotoa kozi mbalimbali vipo. Kanda hii ndio kanda pekee yenye shule nyingi kuliko kanda yoyote hapa duniani na hata baadhi ya mikoa ya nchi fulani barani Afrika. Usishangae katika kata moja kukawa na shule za msingi hata 10, Shule za sekondari tano. Hii ni kusema kuwa wanayohaki kupata elimu wengi. Umeme upo karibu kila kijiji. Vyombo vya habari zikiwemo Redio kadha wa kadha. Huduma za kibenki kila wilaya na hata baadhi ya kata kuna vituo vya kutolea pesa. Huduma za mawasiliano ipo, kila mtandao unashika vizuri. Hakuna tabu ya kufanya miamala ya simu.\

Wasomi na Wataalamu katika kanda hii ni wengi sana. Ndio kanda pekee inayoongoza kwa kuwa na wasomi wengi na wataalamu wengi. Wanasheria, Madaktari, Waalimu, Wahandisi, Wakandarasi, Wanasiasa, Wachungaji, Wahasibu, wataalamu wa mambo ya fedha, Wataalamu wa mawasiliano na kompyuta, Madereva, Makanika n.k. kwenye nchi hii kila fani niliyoitaja hapo wengi wao wanatoka Kanda ya kaskazini.

Rasilimali kama Mbuga za wanyama, Madini, Mlima Kilimanjaro, Bwawa la Nyumba ya Mungu, Mapango ya ambani, Bahari ya Hindi, Maziwa na mito, Ardhi kubwa yenye Rutuba, Tabia ya nchi nzuri, Miti ya matunda n.k. Kilichokosekana hapa ni Gesi na mafuta tuu. lakini hayo mengine yapo kanda ya kaskazini.

Wasanii na watu maarufu. Kanda ya kaskazini ndio kanda pekee yenye wasanii lukuki wanaoeleweka. Wasanii wengi na watu maarufu wengi hutoka kanda hii. Wengi hutoka TANGA, ARUSHA NA MOSHI. Hivyo ni kusema Kanda hii ni moja ya kanda iliyobarikiwa kupita zote.

Ndio Kanda pekee ambayo watu wake wanapenda kwao na kujivunia kwao. Ni watu ambao hawasiti kujitambulisha popote pale. Mtu hata asipoulizwa hujikuta akisema kuwa kwetu ni Moshi, mara home ARA chuga, ooh kwetu Tanga. Hii huifanya kanda hii kuonekana inaubaguzi na umimi kutokana na hulka ya majigambo.

Matajiri na Wafanya biashara wakubwa. Hakuna ubishi kuwa kanda ya kaskazini inaongoza kwa kuwa na watu wenye mpunga na jala la kufa mtu. Atakayebisha ni yule asiyeijua nchi hii vizuri au ambaye hajatembea mikoa mingi katika nchi hii. Karibu kila kata kwenye majiji makubwa hapa nchi huwezi kukuta matajiri kumi bora wa kata hiyo alafu usikute watano wanatoka kanda ya kaskazini. Si Dar es Salaam, si Mbeya, si Mwanza popote pale lazima matajiri wanne au watano katika kata hizo lazima watoke huko kaskazini. Kanda hii inaheshimu pesa sana. Watu wake hawaoni aibu kufanya hata ni shughuli ya kuuza nyanya bila kujali mtu huyo kaenda shule au hajaenda. Wanachoangalia je kuna mpunga basi.

Majambazi, mafisadi na wahujumu uchumi. Ndio kanda pekee inayoweza kutoa Mafisadi, majambazi na wahujumu uchumi kushinda kanda yoyote hapa nchini. Ujambazi wa kimataifa pia umefanya na watu wa kanda hii. Si ajabu mtu kutoka Arusha akienda Kenya kupiga tukio la kijambazi. Hii imepelekea kanda hii kuogopwa na kutokuaminiwa kabisa na kanda zingine hasa kwenye ishu za pesa. Ndio Kanda pekee ambayo hawataki mchezo na mali zao. Si rahisi umdhulumu mtu kutoka kanda hii. Ukisikia kesi ya kuku ng'ombe anauzwa ili kuendesha kesi basi huko kaskazini ndio mtindo.

Ndio Kanda pekee ambayo hawakatai watoto. Na si rahisi kuchukua damu yao.

Ndio kanda pekee inayojiona Superior kuliko kanda zingine. Mtu kutoka huku hata kama hajaenda shule huwezi kumuendesha na kumdharau eti kisa wewe umeenda shule au unavijipesa.

Ikumbukwe kwamba mtu yeyote anaweza kuwa kanda ya kaskazini iwe kwa damu au kuzaliwa huko.

Nawasilisha!
Kaandike kitabu, Kuna kanda zikiamua kufungulia mapori na hifadhi zao wakazifanya zichimbwe na madini na kukata mbao hiyo kasakazini itasubiri sana
 
Mkuu wenzako tukipost tunafanya uchunguzi kwanza. Huko Kigoma wanatoka wasanii wangapi na ni wasanii wa aina gani? Hivi unadhani Chato itajengwa kwa miaka kumi 😀😀😀😀😀. Hivi unadhani mtu mmoja anaweza kujenga mkoa mzima😛😛😛😛.
Hivi unadhani kanda hiyo ilianza mwaka 2015🙂🙂🙂. Nyie shikeni vyombo vyote lakini mkumbuke ni kwa miaka kumi tuu na mbaya zaidi ni kuwa imebaki saba😉😉😉. Eti wasomi ni watumwa wa wanasiasa ndio ulivyofunishwa hivyo na unavyowafundisha watoto wenu huko ndio maana hawaendi shule. Pole sana. Zipo kanda zinaua waume zao na wake zao ili zipande cheo kichawi😛😛.

Mheshimiwa anapapenda kwao lakini hawezi kujenga kwao yeye pekee. Mnatakiwa mumsaidie sio kumtegemea yeye tuu. Mimi nitaendelea kujidanganya lakini ukweli unaujua. Zote ni kanda za nchi yetu. Wengine wamejaliwa ujinga, uchawi na imani za kishirikina. Wamejaliwa kutegemea ndio maana wewe mwenyewe unakiri kuwa mheshimiwa anajenga kwao. Wewe unajenga wapi? Lazima Watanzania tubadilike.
Umeeleweka mkuu afu msomi anakuwa mtumwa wa mwanasiasi kama hajitambui yaani mlinda tumbo yule anayeona thamani ya elimu yake huwez muendesha kihivyo utaachwa mwanasiasa unapiga kelele we na serikali miaka kumi ikiisha unaenda kwako msomi anabaki kwenye nafasi yake
 
Ukisikia madini; yaani almasi, dhahabu umeongelea lake zone. Thamani ya hivi vitu kama vingetumika kikamilifu hiyo kanda ya ziwa na Tanzania kiujumla tungekua mbali zaidi ya unavyo weza fikiria. Hapo nimeongelea madini tu tafadhali.
Madini yenyewe mmempa akasia yanawasaidia nini?.
 
Si kweli wanaume wa kanda maalumu ndo hushobokea wanawake wa kule had kero kuu. Mi shakutana na wengi na vile hamko romantic basi ni kero tupu
Hongera kwa kuwapa haki yao waliyohitaji na wewe ukafurahia ndo maana ushakutana nao hao wengi
 
kumbe hata ww ni wa huko hongera sanaa sema inasikitisha nyie wasichana wa huko badala ya kufanya kazi kwa bidii mnasubiri kuwapoteza wamme zenu sema BTW rafiki yangu 2tanataniana tu mwisho wa siku hakuna kanda iliyo bora, hakuna watu walio bora, hakuna utamaduni ulio bora pia wenzetu wanasema east and west home is best, hivyo tusiishi kikanda ni hatari sanaa mm nipo kaskazini hapa japo siyo wa huku ni Arusha natazama vivutio vya utalii mwanachama alivyo taja hapo juu kama kina wema sepetu nashukuru nimekuwa na moments nzuri huku kaskazini
Pamoja na kuwa anaweza muua mume wake lakin wakati anatafuta na yy hakulala pia jua alipambana,nikwambie tu mwanamke ambaye anakaa nyuma ya meza tu hatathubutu kuua mume wake maana kuzisimamia mali sio mchezo lazima ulikuwa na akili yakutafuta pia huwez endeleza kitu ambacho hujui mwanzo wa misingi yake
 
Nani alie kwambia wasukuma ni wavivu? Kwa taarifa yako msukuma ndio anaweza kuwa mtu mwenye pesa zaidi ya makabila yote, usukumani kuna diamond, dhahabu, ng'mbe, mbuzi, mchele nk.Fanya tathmini pembuzi ndugu.huko uchagani kuna nini zaidi ya ndizi na kahaw na mlima kmnjr, hivi kuna kijana wa kitanzania anaewaza akatafute maisha moshi?sijawahi muona ila wachaga tu kukimbia kwao mnaongoza mkifuatiw na wamakonde japo wana ardhi kubw.Ukweli ni kwamba moshi hakuna rasilimali chochevu kama mkoa wa mby, Morogoro, Njombe, Rukwa, pwani nk.Hata miundombinu iliojwngw huko imejengwa na serikali unasifia utazani wewe ni mkenya, kikwete alileta mfumo wa kiwaondoa katika kujipendelea kielimu, shule za kata zimekata mzizi wa fitina na takwimu zinaonesha wasukuma ndio wengi vyuoni kuliko makabila yote, miaka kumi inayo watatawala kila sekta na wengi wao husoma zaidi sayansi kwa sababu wanaakili kuliko wachaga.
Mkuu wewe ndo umetaja wasukuma na wavivu, bila kujali kabila yoyote akiwa mvivu hajitumi na akili mgando hawezi kufanikiwa, maana maendeleo ni udhubutu.

Mkuu swala lakuwa na dhahabu nakubaliana nalo na ingetakiwa kanda ya ziwa ipige maendeleo makubwa kwa sababu ya hayo madini, but unfortunately hali huko ndo mbaya kuliko inavotakiwa, rasilimali za madini hazijaweza kuisadia Africa, hususani Tanzania kujikwamua maana inaendeshwa na mabepari ka Acacia kwa hyo return kwa community ni mdogo, hayo madini hayawwzi kuondoa umaskini kusikochukuliwa hatua madhubuti maana madini hayagusi wananchi moja kwa moja ka shughuli nyingine za uchumi.

Hyo ya wachaga kukimbia kwao ni akili ya kwenda kutafta fursa sehemu nyingine ili kujipanua hata mataifa makubwa yanaleta makampuni yao kuwataftia wananchi wao fursa kuondoa u maskini, ndo mana nchi hii miradi mingi inafanywa na wageni hyo yote ni fursa hata wewe usikae sehemu moja eti kisa kwenu usiangalie fursa nyingine huo ni uzembe, watu wana search green pasture.

Mkuu shule za kata zimekataje mzizi wa fitina wakati ndo zimesaidia kuondoa ujinga kwa Watanzania wengi. Kumrudisha nyuma aliyetangulia sio solution dawa ni wewe kujikwamua ili upige hatua, mi tangia nimeanza shule darasni waliokuwa wengi walikuwa wachaga, wahaya wanyakyusa sana sana mkuu kwa wingi.
Miaka kumi waweza kutawala lakini itategemea umeijengea vipi jamii yako kuhusu kuwa na mwamko wa elimu na Ku grab different opportunities.
 
Kweli wanapenda kushoboka sana hafu wanakosa sauti sema wanawake wakule wana akili wanawafundisha maisha na kutoa ushamba, ujue ili mwanaume asimame anahtaji mwanamke anayejielewa. Sasa wao ndo wanaoa hao kwa wingi Dada zao nani atawaoa.
Kanda maalumu miaka niliyokuwa Mimi wanawake walikuwa wachache sana kuliko wanaume ndo maana wengi wanaolewa haraka, sasa kanda ya mikoa ya Manyara, Arusha, Kil, na Tanga kuna uhaba wa wanaume na nguvu za kiume ndo maana wale wa kanda maalumu wanapendwa sana Chezea kijana ameanza kunywa michuzi ya samaki tangu mdogo, kula kichuri na vimolo utaachwaje hujaridhika?
 
Ukisikia madini; yaani almasi, dhahabu umeongelea lake zone. Thamani ya hivi vitu kama vingetumika kikamilifu hiyo kanda ya ziwa na Tanzania kiujumla tungekua mbali zaidi ya unavyo weza fikiria. Hapo nimeongelea madini tu tafadhali.
Ni kweli hzo rasilimali zingetunika effectively nchi yetu isingekuwa maskini tatizo hyo buashara inaendeshwa na mabepari, ndo maana Raisi alikuja na mpango wakupitia upya mikataba ya madini
 
Hongera kwa kuwapa haki yao waliyohitaji na wewe ukafurahia ndo maana ushakutana nao hao wengi
Ni kweli shakutana nao wengi ni mabest na Mimi huwapa changamoto za hapa na pale mkuu. Maana wananipenda mwenyewe tu automatically
 
Kanda maalumu miaka niliyokuwa Mimi wanawake walikuwa wachache sana kuliko wanaume ndo maana wengi wanaolewa haraka, sasa kanda ya mikoa ya Manyara, Arusha, Kil, na Tanga kuna uhaba wa wanaume na nguvu za kiume ndo maana wale wa kanda maalumu wanapendwa sana Chezea kijana ameanza kunywa michuzi ya samaki tangu mdogo, kula kichuri na vimolo utaachwaje hujaridhika?
Si kweli mkuu shobo zao tu ujue yakuwapenda, maana kanda maalumu wanakutana na wakorofi wenzao wanatulizwa kwa mpira hawafuruki ng'o hyo nyingine ya vichuri ni case kubwa sana loh
 
Kanda maalumu miaka niliyokuwa Mimi wanawake walikuwa wachache sana kuliko wanaume ndo maana wengi wanaolewa haraka, sasa kanda ya mikoa ya Manyara, Arusha, Kil, na Tanga kuna uhaba wa wanaume na nguvu za kiume ndo maana wale wa kanda maalumu wanapendwa sana Chezea kijana ameanza kunywa michuzi ya samaki tangu mdogo, kula kichuri na vimolo utaachwaje hujaridhika?
Kuhusu wanawake kuwa wengi ni kweli na nafikiri ni sehemu zote ila kwingine umedanganya mkuu
 
Back
Top Bottom