Si tumenunua ndege za kutosha tu na zingine tano (Bombadier 3 na Boing 2) zipo njiani kutua nchini. tatizo liko wapi? Siyo lazima kila kitu utengeneze wewe mwenyewe ndo uonekane tajiri Hata china inanunua ndege toka Marekani. Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa "comparative advantage" kwamba gharama ya kuzaliwa mwenyewe inapokuwa kubwa basi unaamua kuagiza toka nje badala ya kutengeneza mwenyewe na kinyume chache. Pia tupo katika open Economy, hivyo siyo lazima kutengeneza wenyewe kila kitu kama gharama ya kuzalisha wenyewe kwa sasa inaonekana kubwa kubwa kuliko kununua toka nje.
Lakini ukweli mchungu ni kwamba hata David Ricardo alivyokuwa anaazungumzia Comparative Advantage aliingalia dunia katika nyanja finyu mnoo: Wachumi wanasema aliliangalia katika "A Two Country Model" kwamba nchi zitazalisha tu kile ambacho inahitaji na kiko ndani ya uwezo wake, vile vyote ambavyo nchi haina itaagiza kwa mtu nchi yenye nacho.
NB 1: Ikumbukwe kwamba dhana nzima ya Compatarive Advantage Theory ni kuweza kufanya biashara ya kimataifa iwe na utulivu ili kuzuia kadhia za kisiasa kama Vita zilizosababishwa na sera za Kibepari kama Protectionism. Hivyo aliandika kwamba nchi izalishe kidogo tu ili kuzuia msuguano duniani ambao ulijengwa na Absolute Advantage Theory ya bwana Adam Smith. Kama umesoma vizuri utakuja ona kwamba mataifa makubwa yalishindana sana na kutaka kuuza tu huku wanatunisha misuli na kuminya kijeshi nchi ndogo zisiuze ile ziendelee kuwa masikini ya wao wapate faida.
Mwisho wa haya yote ilikuwa ni Vita na maanguko ya kiuchumi kama Economic Depression,
Hivyo Compartive Advantage ilikuwa kama Immediate Response kwa hali iliyotawala dunia wakati huo.
NB 2: Mchumi
Paul Krugman anasema kwamba kutokana na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia kuna baadhi ya nchi zinaweza kuzalisha bidhaa nyingi kwa bei ndogo na kuzipeleka kwenye soko la dunia kwa bei ndogo pia hivyo kufanya bidhaa za nchi nyingine kutouza. Uchumi wa Masoko wa karne ya 21 una kitu kinaitwa Choice of Variety, bidhaa za aina moja zipo nyingi sana hivyo wewe unaamua ununue bidhaa gani na kwa bei gani. Nchi kama Uchina na India wanatumia Cheap Labour kuzalisha teknolojia kubwa kwa bei ndogo, kiasi kwamba wakizipeleka kwenye soko la dunia zinauza sana na zinaharibu masoko ya nchi kama Marekani na Umoja wa Ulaya. Mfano hapa Afrika kuna kipindi simu za Nokia zilikuwa zinauza sana lakini zikaletwa Tecno zenye uwezo ule ule na za bei ndogo na Uchina anauza sanaa.
Hapa bado utasema
Comparative Advantage inafanya kazi wakati Choice of Variety ndiyo inafanya kazi ????
NB 3: Dunia aliyoizungumzia David Ricardo kwenye Comparative Advantage ni ile yenye amani heshima na ushindani safi.
Kwamba wewe hutazalisha kile mwenzako anacho kwasababu unaweza kuingia gharama nzito kama ulivyosema hapo juu lakini kubwa hapa ni kwamba ukizalisha unaweza kusababisha Vita ya Kibiashara isiyo na Msingi wowote ule (Economic War and Trade War); Katika hili pitia Vita ya Kiuchumi baina ya British Empire na Imperial Germany. Walipigana kwasababu walikuwa wanazalisha bidhaa za aina moja na wanaharibiana masoko, wakati upande wa pili Uingereza ili kuzuia vita na mataifa mengine walitengeneza kitu kinaitwa MONOPOLY COMPANIES kama Multi- National Corporations. Ambazo kwa namna moja au nyingine hata kama nchi haizalishia inaweza kumiliki hisa kwenye hayo makampuni na kunufaika kisiasa.
Lakini Kibaya sasa ni kwamba hapa hakuna
Comparative Advantage kwasababu Makampuni Makubwa (Monopoly Companies) kama
Pfizer,
Monsanto na
Syngenta yanazalisha bidhaa ambazo nchi masikini inazalisha na hivyo kuua uchumi kabisa.
Leo hii kuna
World Trade Organization ambayo inajaribu kufanya biashara ya dunia iwe na amani na Ushindani lakini haiwezekani kwasababu haina mamalaka ya kuingilia uchumi wa nchi kama Uchina na kuwapangia nini wazalishe. Ndiyo maana anashusha fedha yake thamani na kuwauimiza wenzake, kinyume kabisa na WTO Rules. Donald Trump analalamika sana kwamba "There is an unbalanced Trade between America and China"
Hapa mkuu utasemaje kuna Comparative Advantage dunia ya leo ???
NB 4: Hivyo mimi nasema kwasababu dunia inabadilika na inakuwa ya kimafia inabidi na sisi tuinue uchumi kwa njia hizo hizo. Hatuwezi kutegemea kwamba tununue tu kile tunahitaji au tutengeneze kile tunahitaji kwasabubu Comparative Advantage Theory inasema, ni lazima tutaumia sanaaaaa. Wazungu hawafuati hizo WTO Rules na wanatushurutisha sisi tuzifuate ili watunyonye. (Haiwezekani)
NB 5: Mwisho kabisa ambacho nadhani umekisahau na nataka ukikumbuke ni kwamba Comparative Advantage ni nadharia tu ya kutufanya tuelewe Uchumi vizuri na ina uhalisia mdogo sana. Katika vitendo kama wewe umesoma shule miaka ya 80 utakuja kukumbukwa kwamba hii Sera ya Comparative Advantage inasababisha kitu kinachoitwa Over-Specialization ambapo nchi inakuwa inategemea bidhaa moja tu AS A SOURCE OF HARD CURRENCY mwisho wa siku ukitokea ushindani basi uchumi wa nchi unatetereka.
Miaka baada ya Uhuru Tanzania tulikuwa tunategemea sana Zao la Mkonge kama bidhaa ya kusafirisha nje,
Lakini bahati mbaya sana tulipata upinzani tokea kwa nchi kama India na watu walivyoanza na mifuko ya plastiki basi nchi ikateteleka sanaaa. USSR ilianguka miaka ya 80 hadi 90 kwasababu ilikuwa inategema Mafuta na Gas as a Source of Hard Currency, kumbe dunia inabadilika na ushindani ukaanza kutokea nchi kama Saudi Arabia: Tunajua nini kilitokea.
HITIMISHO:
Hatuwezo kucheza na sera za karne ya 19 na 20 kwenye huu Ulimwengu mbaya wa Karne ya 21.
Tusipocheza kama ngoma ya dunia inavyotaka tucheze basi tutaendelea kutengeneza Baiskeli tu tukidanganya kwamba ndizo tunazihitaji hizo kwa sasa. Huku tukipeleka mabilioni ya pesa zetu nje kuagiza bidhaa halafu tunajitia moyo na kusema "Comparative Advantage".....Its just too futile.
CC:
izzo ,
Consigliere ,
Dragoon