Hii ndege ni hatari sana ikitokea vita

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,783
Hii ni ndege ya Mrusi aina ya SU-35, iko vizuri sana.
Ila na huyu rubani anajiweza aisee, mhhh!!!

Najiuliza siku ndege kama hii ikivaa silaha nzito na itumike si watu wataumia sana ???

Warusi na bajeti finyu lakini bado wanaendelea kufanya makubwa kama haya.

Najiuliza tu maswali mengi sana,

Hivi na lini sisi tutakuwa na ndoto ya kurusha vitu kama hivi angani ???

Hawa wazungu wana nini cha ziada ambacho sisi hatuna ???

Tokea Uhuru tatizo la maji tu halijaisha; Kwanini lakini ???

CC: Bukyanagandi , Dotworld , Dragoon , Vladimirovich Putin , Maalim Shewedy
 
Hats JWTZ wanaweza hiyo wako ngerengere kawaida sana hiyo.
 
Hats JWTZ wanaweza hiyo wako ngerengere kawaida sana hiyo.

Nafahamu mkuu marubani wazuri lazima wapo hapa nchini kwetu,
Lakini swali la msingi hapa ni hili tu:
kwanini kila siku tutake kununua na kurusha ndege za Wachina, Warusi na Wamarekani ???
Kwanini tusiwaze hata siku moja kutengeneza ndege zetu hata za Abiria na Mizigo tu ???
Tulikuwa na ndoto za kutengeneza magari, lakini leo zile ndoto hazipo, kwanini ???
 
za nini mkuu, kwani tuna mpango wa kupigana na nchi gani? hicho sio kipaumbele kabisa.

Kwasasa nakubaliana na wewe ndege vita siyo Kipaumbele,
Lakini hata za Abiria na mizigo hatuna maono nazo pia ???
Hivi tungekuwa tumewekeza kwenye elimu kwa spidi ile ile ya Mwalimu unahisi leo hii tungekuwa wapi ???

NB: Mbona India wanarusha hadi vyombo nje ya dunia ???
 
Kuna watakao kuja na kukubeza at unatukuza wazungu ati ata sisi tunanyungo za asili. Weusi tulilogwa na nani sijui

Mambo mazuri na mafanikio hayani Rangi au Utaifa,
Hata kama wakibeza ukweli utabaki kwamba hawa wazungu wametushinda sana.
Hivyo kama kuna mazuri ya kuiga basi tuige na sisi tuendeleee: Wachina wanaiga sana na wamepiga hatua kali.
 
Katika ndege ambazo mrusi alitulia ni hizi zinazo tengenezwa na Sukhoi(Su) ingawa kuna makampuni kama MIG nayo yanatengeneza hizi ndege...moja ya "Signature " ya ndege za mrusi ni kufanya "Cobra Maneuver "Hakika inapendeza!
 
Moja ya "Signature" za ndege za Mrusi hasa hizo za Sukhoi

Ni State of the Art aisee!
Wakomunisti na ubaya wao wote lakini walifanya kazi sana kuendeleza Urusi.
Hii kitu tokea mwaka 1988 mpaka leo inadunda kwa kishindo.....
 
Katika ndege ambazo mrusi alitulia ni hizi zinazo tengenezwa na Sukhoi(Su) ingawa kuna makampuni kama MIG nayo yanatengeneza hizi ndege...moja ya "Signature " ya ndege za mrusi ni kufanya "Cobra Maneuver "Hakika inapendeza!

Hivi tuseme ukweli tu,
Umoja wa Kisovieti ungekuwepo mpaka leo unadhani wangukuwa wapi kiteknolojia ???
Maana hizi ndege zote za sasa hivi MiG na Sukhoi zote zilitengenezwa miaka ya Sabini na Themanini hivi.

Sasa kama vile viwanda vya ndege vilivyokuwa Ukraine, Poland na Georgia vingekuwa chini ya Usimamizi moja basi sijui kama leo hii NATO angekuwa na Ubavu wa kupiga hata makelele mengi hivi.

Kinachonifanya niwaze ni kwamba Mrusi bado ana nguvu sana japo anatumia silaha zilizotengenezwa zamani na Umoja wa Kisovieti. Walichofanya wakina Vladmir Putin na wenzake ni kuviboresha (Upgrade) hivi vifaa. Lakini ukiangalia Marekani anatengeneza silaha mpya kila uchwao na ana bajeti kubwa sana lakini bado anasumbuliwa sana Urusi.

NB: Kuwekekeza kwenye Elimu kunalipa sana kuliko hata kuwekeza kwenye Miundombinu.( Education is just sustainable my friend)
 
Maendeleo ya Wazungu na sisi ni sawa na mbingu na.ardhi!

Hujakosea mkuu,
Japo maendeleo ya Wazungu ambayo mimi ninayaonea wivu ni maendeleo ya watu wake (Kielimu na Kiustaraabu)
Kifupi ni uwezo wao wa kujituma na kujitambua kwamba ni nini wanahitaji na kwa wakati upi na wafanyaje kukipata.
Kama maendeleo ya vitu (Ndege, Reli, Flyovers na Maghorofa) hata Uarabuni wanayo lakini hayanivutii kabisa. (Maendeleo ya vitu vya kununua kutoka nje huwa hayadumu; yanakufanya uwe mtumwa na udumae akili)
 
Nafahamu mkuu marubani wazuri lazima wapo hapa nchini kwetu,
Lakini swali la msingi hapa ni hili tu:
kwanini kila siku tutake kununua na kurusha ndege za Wachina, Warusi na Wamarekani ???
Kwanini tusiwaze hata siku moja kutengeneza ndege zetu hata za Abiria na Mizigo tu ???
Tulikuwa na ndoto za kutengeneza magari, lakini leo zile ndoto hazipo, kwanini ???
Kwanza tutengeneze baiskeli, tben pikipiki, then motokaa.....mambo ya ndege tusubiri kwanza
 
Back
Top Bottom