Unaweza ukawaza kuhusu kutengeneza ndege za auna hiyo sababu kwenye mawazo ya yaliyo ndani ya kichwa cha mjinga kila kitu kinawezekana. Tumeshawaza na sasa tumeanza kuimba nyimbo za uchumi wa viwanda bila hata kuwa ma aina ya hiyo elimu wala mikakati na fitna zake na tunaamini inawezekana.
Ni ngumu sana kushindana pasipo kuwa na taarifa za kutosha. Kwa wale waliosoma Intelligence Analysis watanielewa nikisema hivi; nasikitishwa sana na aina ya mikakati tuliyo nayo katika kuijenga nchi yetu, nasikitishwa na vipaombele, nasikitishwa na wataalamu wetu na zaidi nasikitishwa na uduni tulio nao katika matumizi ya Takwimu. Tulijiandaa kwa muda mrefu na kwa ghalama binafsi kuwa sehemu ya mfumo wa nchi usio na biaseness ili tuijenge na kuipeleka nchi next level but who knows you and who cares imetufikisha hapa. Kila uongozi mpya unapoingia madarakani inakuwa kama vile nchi ndiyo kwanza imepata uhuru. Kila mtawala atataka ajenge na kuwapa kipaombele matajiri wake, wanausalama wake, na wanataaluma wake, marafiki zake n.k
Nchi ilhaina kabisa consistence and yet unatarajia kusimama sambamba na nchi kama Bophuthatswana (Botswana), Namibia, Kenya, Zambia, na nyinginezo nyingi. Kiwanda gani utakijenga katika nchi ya aina hii? Huna business connections, huna Diplomatic approaches, unabadirika badirika kwenye musimamo na kauli zako halafu unadanganya unataka kuipeleka nchi next level, labda utaweza maana hata nje ya mstari ikawa next level kwa tafsiri za watu wa aina hii.
Tukubali tu kwamba tumeumia. Nashindwa kuamini kwamba wale waliomo ndani ya mfumo wote ni academician tu na hatuna watu waliopata kusoma kozi Intelligence Analysis.
Tuliopo benchi tunapata hasira sana tuonapo viongozi na wataalam wa nchi wanavyo jikanyaga kanyaga bila kwenda mbele mithili ya mtu anayechanganya maji na udongo wa kutengenezea matofali ya udongo.
Acha tuendelee kuwa watazamaji tu. Taifa ni lao sisi wengine ni kama wapangaji tu ndani ya hili taifa, cha muhimu ni kulipa kodi na kyfuata sheria na masharti basi.