Hii hali ya kuwa kuna waajiriwa wana maisha mazuri kuliko wafanyabiashara kibao ni kitu watu huwa hawataki kukubali ila ukweli hauwezi kubadilika.

Hii hali ya kuwa kuna waajiriwa wana maisha mazuri kuliko wafanyabiashara kibao ni kitu watu huwa hawataki kukubali ila ukweli hauwezi kubadilika.

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,451
watanzania wengi wapo brainwashed kutetea biashara ndio njia pekee ya kutoboa na mifano lazima iwe ile ya kina MO na Bakhresa,

Ni kweli biashara ndio sekta inayotajirisha zaidi lakini haimaanishi watu wenye ajira wana maisha mabaya.

kuna waajiriwa wengi wana maisha mazuri ya uhakika kuzidi wafanyabiashara kibao.

Unapoangalia wafanyabiashara wachache waliotoboa jua kuna wengi zaidi wanafunga biashara kila siku, wanazihudumia biashara badala ya biashara kuwahudumia, Wameshindwa kurejesha mikopo wanapoteza hadi nyumba za urithi, biashara iliyofanikiwa miaka 10 ghafla inapata upinzani mkali na kufilisika, n.k.

Hitimisho: HATA KAMA UMEAJIRIWA JITAHIDI UWE NA BIASHARA !😊 WAPO WANAOFANIKIWA !
 
Kati ya wasomi 20 ni wawili tu ndio wanaopata ajira

Kwa hio hawa wengine wafanye nini haswwa
 
Karibu kila mtanzania kawa brainwashed kutetea biashara pekee ndio njia ya kutoboa, hata ukutana na mtu ambae biashara imemfilisisha atakwambia Biashara ni tamu 😂 lakini muda huo yupo bize kuwaambia watoto wake someni mje mpate kazi,
Ukiwa katika ajira una lenga kupata mshiko,
Ukiwa umejiajiri una lenga kupata mshiko,

Na kote unaweza kupata maisha mazuri tu ya hadhi yake
Ila when it comes to utajiri, penye fursa ya kupata utajiri ni kwenye biashara

Na angle ya biashara unaweza kuifanya hata ukiwa umeajiriwa, ukawa na biashara zako zinakuingizia mapato

Hivyo unaweza kuajiriwa na bado ukawa una miliki biashara zako kadhaa

Sasa mleta mada hapo unaweza kuweka heading yako vizuri,, unamaanisha maisha mazuri kwa kulinganisha muajiriwa asiyejishughulisha na biashara yoyote vs mfanyabishara...!??
 
Ukiwa katika ajira una lenga kupata mshiko,
Ukiwa umejiajiri una lenga kupata mshiko,

Na kote unaweza kupata maisha mazuri tu ya hadhi yake
Ila when it comes to utajiri, penye fursa ya kupata utajiri ni kwenye biashara
Umesahau kuandika point muhimu biashara haina huruma, watu wanafunga biashara kila siku, kuhudumia biashara bila faida yoyote, kufilisika hadi mali za urithi kupigwa mnada, n.k.

biashara inatajirisha lakini pia inacharaza kupitiliza
 
Hata Kama umeajiriwa jitahidi uwe na biashara .

Kwakuwa ukifa familia yako inaweza kuendeleza biashara zako Ila haiwezi kuendeleza ajira yako

Pia ukipata changamoto yoyote ile Kama Afya , ulemavu n.k ukiwa tayari Una biashara unaweza Ku-survive

Biashara sio lazima uwe na products zinazoshikika , no , waweza kuwa na Nyumba kadhaa unapangisha, mashamba ya kilimo n.k zote hizo ni biashara.
Kutegemea ajira Kama chanzo kikuuu pekee cha kipato ni hatari sana.

Kuhusu kuishi maisha vizuri ni mpangalio wako mwenyewe na jinsi yatafsiri hayo maisha mazuri.
 
Ni kitu muhimu kuwa na biashara hata kama umeajiriwa, Kina Marehemu Mengi, Vunja Bei, Marehemu Ally Mafuriki nao waliwahu kuwa waajiriwa

Unaishi nchi ipi mkuu, watoto wa waajiriwa wengi tu wanapigiwa pasi sehemu ambazo wazazi au ndugu zao wapo.

Nenda jeshini, mahakamani, TRA, n.k. ajira zikitangazwa watu kibao tu wanawekwa kwasababu wazazi au ndugu zao wamo.

Shida inakuja labda mtu awe hana elimu au kasomea fani nyingine au mtu wa kumweka hana ushawishi.
 
Back
Top Bottom