HESLB yajipanga ‘kuwaliza’ wanafunzi vyuo vikuu

HESLB yajipanga ‘kuwaliza’ wanafunzi vyuo vikuu

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB), imetangaza mpango wa kupitia upya na kusitisha mikopo wanafunzi wote inaodai kuwa walipewa mikopo lakini hawakidhi vigezo vipya vya utolewaji wa mikopo hiyo.

Abdul-Razaq Badru, mkurugenzi wa HESLB akizungumza katika ukumbi wa Idara ya Habari – MAELEZO jijini Dar es Salaam amewambia waandishi wa habari kuwa bodi hiyo lazima ipitie upya majina ya wanafunzi waliopewa mikopo hata kama wapo katika mwaka wao wa mwisho wa masomo.

Badru ametaja wanafunzi wanaostahili kupata mikopo kuwa ni yatima, walemavu au wenye wazazi wasiojiweza pamoja na wale wanaosoma masomo ambayo ni miongoni mwa vipaumbele vya taifa.

“Kwa vigezo hivi, muombaji anayesoma fani za sayansi za tiba na afya, ualimu wa Sayansi na Hisabati, uhandisi (Viwanda, Kilimo, Mifugo Mafuta na Gesi) au yatima, mlemavu na mwenye wazazi wenye hali duni au wasiojiweza ndiye anayestahili kupata mkopo.

HESLB tutahakiki upya wanufaikaji wa mikopo waliopo mwaka wa pili, tatu na hata wale wa mwaka wa nne ili kuondoa kila asiye na sifa na kwa wale wa mwaka wa kwanza waliokosa mikopo na wanadhani wanazo sifa wakate rufaa kuanzia Novemba Mosi,” amesema Badru.

Wakati HESLB ikijiandaa kufanya hivyo, Kilonzo Mringo, Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFMSO) amesema iwapo bodi ya mikopo itafanya hivyo, wanafunzi wengi watashindwa kuendelea na masomo.

“Mpaka sasa IFM wanafunzi wengi wana sifa na wamenyimwa mikopo, wengine wameamua kusitisha masomo yao na wengine wanasoma kwa kuja chuo wiki moja, nyingine wanaenda kutafuta fedha. Hali ni mbaya, wakiamua kupunguza tena idadi ya wanaopata mikopo basi chuo kitabaki kitupu,” amesema Mringo.

Eliudi Kasunzu, Waziri wa Mikopo katika Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) ameiambia MwanaHALISI Online kuwa hawapingi zoezi la uhakiki lakini wanaishangaa HESLB kuhakiki wanaopata mikopo ambao ni wachache na kuacha kuhakiki wengi walionyimwa.

“Hatuoni mantiki ya kutuhakiki tena kwa kuleta dodoso wanafunzi wajaze, fomu za maombi wanazo huko ofisini kwao wakihitaji kuhakiki basi waziangalie na si kutuingiza kwenye usumbufu wa kujaza dodoso wakati hivi karibuni wamefanya uhakiki wa idadi ya wanufaikaji.

“Hata vigezo walivyoweka mwanzo hawazingatii, tuna orodha kubwa ya wanafunzi yatima, walemavu na wanaosoma masomo yanayotajwa kuwa ni vipaumbele vya taifa lakini bado wamenyimwa mkopo halafu wanataka wachache waliopata wawapunguze zaidi,” amesema.

Boniface Emmanuel, Waziri Mkuu wa DARUSO yeye amesema anadhani kitendo cha HESLB kutaka kuhakiki wanafunzi wanaoendelea na masomo ni mbinu ya kuchelewesha kuwapa fedha zao za kujikimu.

“Kama mtu aliomba mkopo mwaka mmoja, miwili au mitatu iliyopita na akaonekana kwa bajeti na uchambuzi wa wakati huo ana vigezo vya kupata mkopo, iweje umuhakiki mwaka huu? Nadhani wanatafuta kisingizio cha kuchelewa kulipa fedha za kujikimu za awamu zijazo kwa kisingizio cha uhakiki,” amesema Boniface.
BODI YA MIKOPO NI JIPU TENA LINA FUNZA
 
Hawa jamaa vipi hivi hivyo vigezo walivyoviweka ili MTU kupata mkopo mbona havina mantiki,mfano wanasema yatima ndio apewe mkopo mfano mtoto wa Marehem Wilson Kebwe aliekuwa mkurugenzi wa jiji DSM apewe mkopo kwa sababu ni yatima? Au mtoto wa Bakhresa su mtoto wa Manji apewe mkopo kwa sababu anasoma masomo yanayowekewa kipaumbele kwa mfano sayansi ya tiba ,ualimu wa sayansi na nyingineyo? Sioni mantiki hapo .
 
Mh. Rais Magufuli.. hii Bodi ya mikopo, ni jipu limeiva, limepasuka, na bado linarudia rudia jipu hili.. plse, do all you can, tumbua na kunyofoa kiini cha HELSB... sbb huwezi hakiki mwanafunzi wa mwaka wa pili, tatu na nne wakati walishapewa mikopo miaka yote..

Cha msingi sana ni kudili na wanaoanza vyuo, wafuate vigezo kwa umakini mkubwa... sio ambao tayari walikuwa wana mikopo, hii itawafukuzisha vyuo wengi kwa kukosa ada, boom etc.. ni hatari sana hii
[/QUOT
Mh. Rais Magufuli.. hii kBodi ya mikopo, ni jipu limeiva, limepasuka, na bado linarudia rudia jipu hili.. plse, do all you can, tumbua na kunyofoa kiini cha HELSB... sbb huwezi hakiki mwanafunzi wa mwaka wa pili, tatu na nne wakati walishapewa mikopo miaka yote..

Cha msingi sana ni kudili na wanaoanza vyuo, wafuate vigezo kwa umakini mkubwa... sio ambao tayari walikuwa wana mikopo, hii itawafukuzisha vyuo wengi kwa kukosa ada, boom etc.. ni hatari sana hii
Hivi ww kwa akili yako mbovu unadhani bodi wanafanya vitu from vacuum?huyo unayemwambia awatumbue ndiye kawaagiza.Au hukuelewa maana ya "msinidrive!msinidrive!"
 
Mimi Nadhani Serikali ingetangaza moja kwa moja kwamba imejitoa kwenye suala la kuwakopesha wanafunzi wote ili wazazi wajue moja, kuliko kuleta usumbufu usio na maana.

By the way, huu ni mkopo siyo msaada kwa sababu mwanafunzi lazima arudishe huko mbeleni. nionavyo mimi serikali haina mpango tena wa kuwekeza kwenye elimu, maana unapoanza kubagua wanafunzi kwa fani wanazosoma ni sawa na kudhani mkono wa kushoto hauna msaada kwenye mwili wa binadamu kwa sababu tu mkono wa kulia upo.

Fani zote ni muhimu na zinategemeana sana katika kuleta maendeleo.

Binafsi napinga aina yoyote ya kuwabagua watu kwa rangi, kabila, dini, vyama, utaifa na sasa huu ubaguzi wa kisasa eti fani unayosomea.
 
Bodi ya mikopo ya elimu ya juu imejaa ubabaishaji tu, kama ilivyo kwa kuhani mkuu. Kuna wanafunzi walipata boom la semester ya pili ya mwaka jana wakati wakiwa likizo kunako mwezi wa saba mwishoni. Kama si ujuha ni nini?
 
Unafiliria kwa kutumia kiungo gani kudhani haya yanafanyika bila rais kujua?
 
usijisumbue vigezo vipya ni kwaajili ya mwaka wa kwanza tuu... aliyepost ni kijakazi wa Mbowe
Hahaha jipe moyo,au haujaangalia tv leo?Mkurugenzi Mkuu wa bodi kaweka kila kitu hadharani yaani mwaka huu lazima uisome namba,na wavimbe wapasuke ngenge,acha muisome namba wee lalala mmeichagua wenyewe.
 
Lissu ulisema haya mapema, usipoguswa leo utaguswa kesho watu wakabaki wanatumbua macho tu..uliomba ushirikiano watu wakabaki kukodoa macho tu.

Leo ametufikia hatujui pakushika, najua umekaa kwenye meza unatushangaa tu. Ngoja turudi nyumbani make pesa inakusanywa na kutunzwa kwa ajili ya kutushonea vazi la taifa na siyo kutukopesha sisi taifa la kesho.
 
Mh. Rais Magufuli.. hii Bodi ya mikopo, ni jipu limeiva, limepasuka, na bado linarudia rudia jipu hili.. plse, do all you can, tumbua na kunyofoa kiini cha HELSB... sbb huwezi hakiki mwanafunzi wa mwaka wa pili, tatu na nne wakati walishapewa mikopo miaka yote..

Cha msingi sana ni kudili na wanaoanza vyuo, wafuate vigezo kwa umakini mkubwa... sio ambao tayari walikuwa wana mikopo, hii itawafukuzisha vyuo wengi kwa kukosa ada, boom etc.. ni hatari sana hii
Kwa hiyo wewe unadhani haya yote yanayoendelea yeye hayajui na hayana baraka zake?
 
Tatizo la hii nchi ni kubwa sana, shida inakuja pale tunapojadili na kutoa majibu ya muda mfupi. Hii ni nchi ambayo haijui iko katika mrengo gani! Hatujui ni wajamaa au wabepari. Hili ni tatizo kubwa sana kama tupo ujamaa kila kitu kinajulikana namna inavyotakiwa ni kiwa na maana serikali ndio mkurugenzi wa kila kitu ndani ya nchi. Kama ni ubepari maana yake serikali ni msimamizi tu. Mfano kigezo cha mzazi maskini ni kipi? na mzazi tajiri au mwenye uwezo ni kipi? Na hapa ndipo unapozalisha ufisadi. Mfano wenzetu ukifikisha miaka kumi na nane wewe na mzazi mmemalizana inabaki kati ya wewe(18yo) na serikali. Kama mzazi ni tajiri haimzuiii mtoto kukopa pesa kwaajili ya elimu yake kwan atakayefaidika ni yeye na si mzazi. Nitaendelea kurudia kuwa bila kuweka mfumo sahihi tutaendelea kuchanganyana hivi hvi.
 
Ni wakati sasa kuwe na sheria za:-

1.Ukimteua mtu, na kumtengua, inabidi uelezee sababu za kina kwa nini unamtengua na kwa nini tusikuchukulie wewe uliyemteua huyu unayemtengua kama mzembe kwa kumteua mtu ambaye hujamfanyia uchunguzi wa kutosha na unakuja kumtengua.

2. Ukimpitisha mtu kwa kazi, mkopo, kupandishwa cheo etc halafu mtu akaonekana hajafikisha vigezo baada ya kupitishwa, wewe uliyempitisha uwajibishwe kwanza kabla ya yeye kuwajibishwa.

Mtu ka[ataje mkopo bila kufikisha vigezo kama hakuna uzembe uliotokea hapo kati katika waliompitisha?
 
Tatizo la hii nchi ni kubwa sana, shida inakuja pale tunapojadili na kutoa majibu ya muda mfupi. Hii ni nchi ambayo haijui iko katika mrengo gani! Hatujui ni wajamaa au wabepari. Hili ni tatizo kubwa sana kama tupo ujamaa kila kitu kinajulikana namna inavyotakiwa ni kiwa na maana serikali ndio mkurugenzi wa kila kitu ndani ya nchi. Kama ni ubepari maana yake serikali ni msimamizi tu. Mfano kigezo cha mzazi maskini ni kipi? na mzazi tajiri au mwenye uwezo ni kipi? Na hapa ndipo unapozalisha ufisadi. Mfano wenzetu ukifikisha miaka kumi na nane wewe na mzazi mmemalizana inabaki kati ya wewe(18yo) na serikali. Kama mzazi ni tajiri haimzuiii mtoto kukopa pesa kwaajili ya elimu yake kwan atakayefaidika ni yeye na si mzazi. Nitaendelea kurudia kuwa bila kuweka mfumo sahihi tutaendelea kuchanganyana hivi hvi.
Umeongea vitu vya msingi sana.

Hasa hizo habari za mrengo.

Nilishauri kutumia principle ya "To each according to his need, from each according to his ability" nikaja kujistukia hiyo ni principle ya kijamaa na kikomunisti zaidi.

Lakini nikashindwa kujua kama hii principle kuwa ya kijamaa zaidi ina tatizo Tanzania ama la.

Kwa sababu Tanzania hatujui ni nchi ya kijamaa au kibepari.

Kimsingi Tanzania bado ni nchi ya kijamaa na kanuni hiyo inasimama bado.

Lakini ukiangalia Azimio la Zanzibar lilivyolibadili la Arusha na soko huria lilivyokuwadiwa kiasi kwamba kuna mambo Tanzania tumekuwa mabepari kuliko Marekani, inabidi ujiulize swali hilo ulilouliza.

Tanzania inafuata mrengo gani?

Kwa sababu leo kuna utitiri wa vyama vinavyozunguka personalities, ukiuliza wanavyama chama chako kinafuata itikadi gani ya kisiasa, wanaanza kusema majina ya watu, Magufuli mbaya, Mbowe fisadi etc.
 
Umeongea vitu vya msingi sana.

Hasa hizo habari za mrengo.

Nilishauri kutumia principle ya "To each according to his need, from each according to his ability" nikaja kujistukia hiyo ni principle ya kijamaa na kikomunisti zaidi.

Lakini nikashindwa kujua kama hii principle kuwa ya kijamaa zaidi ina tatizo Tanzania ama la.

Kwa sababu Tanzania hatujui ni nchi ya kijamaa au kibepari.

Kimsingi Tanzania bado ni nchi ya kijamaa na kanuni hiyo inasimama bado.

Lakini ukiangalia Azimio la Zanzibar lilivyolibadili la Arusha na soko huria lilivyokuwadiwa kiasi kwamba kuna mambo Tanzania tumekuwa mabepari kuliko Marekani, inabidi ujiulize swali hilo ulilouliza.

Tanzania inafuata mrengo gani?

Kwa sababu leo kuna utitiri wa vyama vinavyozunguka personalities, ukiuliza wanavyama chama chako kinafuata itikadi gni ya kisiasa, wanaanza kusema majina ya watu, Magufuli mbaya, Mbowe fisadi etc.
Well said Mkuu! Nashukuru kwakunielewe mimi sio mwandishi mzuri wa kile ninachowaza. Ila umegusia jambo zuri sana Vyama vyetu vya siasa vyote hakuna chama chenye itikadi yoyote ile ndio maana kila mtu anahama anavyotaka kwani hakuna wanachoamini. Kwa wenzetu vyama ni kama dini huwezi hama hama tu kila mtu atakushangaa!
 
Back
Top Bottom