HESLB yajipanga ‘kuwaliza’ wanafunzi vyuo vikuu

HESLB yajipanga ‘kuwaliza’ wanafunzi vyuo vikuu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB), imetangaza mpango wa kupitia upya na kusitisha mikopo wanafunzi wote inaodai kuwa walipewa mikopo lakini hawakidhi vigezo vipya vya utolewaji wa mikopo hiyo.

Abdul-Razaq Badru, mkurugenzi wa HESLB akizungumza katika ukumbi wa Idara ya Habari – MAELEZO jijini Dar es Salaam amewambia waandishi wa habari kuwa bodi hiyo lazima ipitie upya majina ya wanafunzi waliopewa mikopo hata kama wapo katika mwaka wao wa mwisho wa masomo.

Badru ametaja wanafunzi wanaostahili kupata mikopo kuwa ni yatima, walemavu au wenye wazazi wasiojiweza pamoja na wale wanaosoma masomo ambayo ni miongoni mwa vipaumbele vya taifa.

“Kwa vigezo hivi, muombaji anayesoma fani za sayansi za tiba na afya, ualimu wa Sayansi na Hisabati, uhandisi (Viwanda, Kilimo, Mifugo Mafuta na Gesi) au yatima, mlemavu na mwenye wazazi wenye hali duni au wasiojiweza ndiye anayestahili kupata mkopo.

HESLB tutahakiki upya wanufaikaji wa mikopo waliopo mwaka wa pili, tatu na hata wale wa mwaka wa nne ili kuondoa kila asiye na sifa na kwa wale wa mwaka wa kwanza waliokosa mikopo na wanadhani wanazo sifa wakate rufaa kuanzia Novemba Mosi,” amesema Badru.

Wakati HESLB ikijiandaa kufanya hivyo, Kilonzo Mringo, Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFMSO) amesema iwapo bodi ya mikopo itafanya hivyo, wanafunzi wengi watashindwa kuendelea na masomo.

“Mpaka sasa IFM wanafunzi wengi wana sifa na wamenyimwa mikopo, wengine wameamua kusitisha masomo yao na wengine wanasoma kwa kuja chuo wiki moja, nyingine wanaenda kutafuta fedha. Hali ni mbaya, wakiamua kupunguza tena idadi ya wanaopata mikopo basi chuo kitabaki kitupu,” amesema Mringo.

Eliudi Kasunzu, Waziri wa Mikopo katika Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) ameiambia MwanaHALISI Online kuwa hawapingi zoezi la uhakiki lakini wanaishangaa HESLB kuhakiki wanaopata mikopo ambao ni wachache na kuacha kuhakiki wengi walionyimwa.

“Hatuoni mantiki ya kutuhakiki tena kwa kuleta dodoso wanafunzi wajaze, fomu za maombi wanazo huko ofisini kwao wakihitaji kuhakiki basi waziangalie na si kutuingiza kwenye usumbufu wa kujaza dodoso wakati hivi karibuni wamefanya uhakiki wa idadi ya wanufaikaji.

“Hata vigezo walivyoweka mwanzo hawazingatii, tuna orodha kubwa ya wanafunzi yatima, walemavu na wanaosoma masomo yanayotajwa kuwa ni vipaumbele vya taifa lakini bado wamenyimwa mkopo halafu wanataka wachache waliopata wawapunguze zaidi,” amesema.

Boniface Emmanuel, Waziri Mkuu wa DARUSO yeye amesema anadhani kitendo cha HESLB kutaka kuhakiki wanafunzi wanaoendelea na masomo ni mbinu ya kuchelewesha kuwapa fedha zao za kujikimu.

“Kama mtu aliomba mkopo mwaka mmoja, miwili au mitatu iliyopita na akaonekana kwa bajeti na uchambuzi wa wakati huo ana vigezo vya kupata mkopo, iweje umuhakiki mwaka huu? Nadhani wanatafuta kisingizio cha kuchelewa kulipa fedha za kujikimu za awamu zijazo kwa kisingizio cha uhakiki,” amesema Boniface.
 
Ukimnyima mkopo mwanafunzi wa mwaka wa mwisho akashindwa kuendelea utarudisha vipi pesa ulizo mpa awali? Huu si ni mkopo? Acheni ya wenzenu, acha vijana mlio wakuta wamalize masomo na mje na ya kwenu..... ndo JK alisema ukiwa kiongozi mpya ............
 
Wawaangamize tu ili mabadiliko yakweli yapatikane.Maana wale uvccm waliopo vyuoni hakika watahamasisha mabadiliko yakweli.Mimi naomba mtukufu aendelee kukandamiza ili huko vijijini kwetu watu wapate elimu ya uraia bila kuelimishwa na Zitto,Mbowe,Lissu au Mbatia.Watoto wao wenyewe watawafikishia elimu ya uraia.
 
Mwaka wa pili,mwaka wa tatu eti wasiokuwa na vigezo acheni kutuyumbisha tutachoka na sisi
usijisumbue vigezo vipya ni kwaajili ya mwaka wa kwanza tuu... aliyepost ni kijakazi wa Mbowe
 
Serikali imeshindwa kuboresha elimu,awamu ya kikwete,kikwete alifanya mambo ya hovyo lakini huyu mtukufu wa sasa anafanya mambo ya hovyo zaidi ya awamu iliyopita,tuendelee kusubiri tanzania ya viwanda vya kufyatua
 
Mh. Rais Magufuli.. hii Bodi ya mikopo, ni jipu limeiva, limepasuka, na bado linarudia rudia jipu hili.. plse, do all you can, tumbua na kunyofoa kiini cha HELSB... sbb huwezi hakiki mwanafunzi wa mwaka wa pili, tatu na nne wakati walishapewa mikopo miaka yote..

Cha msingi sana ni kudili na wanaoanza vyuo, wafuate vigezo kwa umakini mkubwa... sio ambao tayari walikuwa wana mikopo, hii itawafukuzisha vyuo wengi kwa kukosa ada, boom etc.. ni hatari sana hii
 
Kuna vidio niliyonayo huyo mkurungenzi akiyazungumzia hayo,sema nashindwa kuipandisha jukwaani naomba mtu ani PM namba yake ili nimtumie aiweke jukwaani.
 
Andamaneni si mlizoea kuandamana JPM hajaribiwi,tangu JPM kaingia madarakani sijawahi kuona maandamano yeyote hongera sana JPM umerudisha nidhamu.
 
Hivi huo uhakiki wanawatembelea majumbani kuangalia hali za familia zenu au wanapitia zile fomu tulizokuwa tunajaza miaka ile?
 
Laana ya kuirudisha ccm madarakani itatafuna wengi sana!
Kwa makosa yaliyofanyika tutarajie majuto makubwa hasa kwa wale waliokuwa wakiitikia kibwagizo cha ule wimbo wao maarufu!
 
Back
Top Bottom