HESLB yajipanga ‘kuwaliza’ wanafunzi vyuo vikuu

HESLB yajipanga ‘kuwaliza’ wanafunzi vyuo vikuu

hili la mikopo linaleta utata kila kukicha...
rupia ziko kweli??
 
SWALI LANGU LA MSINGI NI KUWA;WAKATI WANACHUO WAKIJAZA DODOSO HELA YA BOOM KWA FIRST SEMESTER ZITATOLEWA AMA NDO MPAKA UHAKIKI UISHE??NI ZOEZI LA MWEZI MMOJA KWA MAELEZO YA BODI THAT MEANS NI NOVEMBER MPAKA DECEMBER,VIPI BOOM LA PILI???
ilo dodoso mbona mm silioni kwenye web yao
 
NI KINYAAA NA UKAKASI KUSIKIA HABARI KAMA HIZI. MTU KAFIKA MWAKA WA NNE UNATAKA KUMPOKONYA MKOPO! TATIZO VIONGOZI WETU HAWAJAWAI KUONA REACTION ZA WANANCHI.
Hahaha, Wananchi gani labda? Labda kama sio Watanzania.
 
Serikali kwann mnafanya hivi?? Kumbukeni kama nyinyi muna uwezo wakusomesha watoto wenu bila mikopo lakini kuna wazazi wenzenu wanaishi maisha duni ikiwa urithi wa mtoto ni elimu kweli elimu tutaipata??? Wanaondelea kupata mkopo vipi Leo muwafutie mikopo kwan hapo mwanzo hamkuyaona haya,??? Tulio maliza diploma kwenda degree hatuna haki ya kupata mkopo wakt hapo awali walikua wanapata hata sisi tunaishi maisha duni elimu yenyewe ya kuungaunga nyie wnyw baadh yenu wametoka diploma kwenda degree, tambueni mnatukomoa sisi wanafunz na kuumiza wazazi wetu, kila lenye mwanzo lina mwisho wake.
 
Matairaa hamkosag piaaa
Mmeshikiliaaa uchamaa tu kat mamboo yanazd kuaa tatzooo
Iyoo ixhu ipooo
Mkuu kifaa chako hakina "S"? Una hoja nzuri toka huko juu lakini unaharibu kwa kuweka "X" inapostahili "S". Lugha ya Kiswahili haina herufi 'X'
 
Ni muda wa kuona umuhimu wa Bima za Elimu haiwezekani uweze kulipa Bima Gar lako halfu mtoto mpaka anafika form six hana bima ya Elimu makampun yapo ila tatizo uelewa wetu mfano nawa Alliance Life Insuarance wana bima.nzur za elimu
27a4624f1601fa288aa602aaa357f0b3.jpg
 
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB), imetangaza mpango wa kupitia upya na kusitisha mikopo wanafunzi wote inaodai kuwa walipewa mikopo lakini hawakidhi vigezo vipya vya utolewaji wa mikopo hiyo.

Abdul-Razaq Badru, mkurugenzi wa HESLB akizungumza katika ukumbi wa Idara ya Habari – MAELEZO jijini Dar es Salaam amewambia waandishi wa habari kuwa bodi hiyo lazima ipitie upya majina ya wanafunzi waliopewa mikopo hata kama wapo katika mwaka wao wa mwisho wa masomo.

Badru ametaja wanafunzi wanaostahili kupata mikopo kuwa ni yatima, walemavu au wenye wazazi wasiojiweza pamoja na wale wanaosoma masomo ambayo ni miongoni mwa vipaumbele vya taifa.

“Kwa vigezo hivi, muombaji anayesoma fani za sayansi za tiba na afya, ualimu wa Sayansi na Hisabati, uhandisi (Viwanda, Kilimo, Mifugo Mafuta na Gesi) au yatima, mlemavu na mwenye wazazi wenye hali duni au wasiojiweza ndiye anayestahili kupata mkopo.

HESLB tutahakiki upya wanufaikaji wa mikopo waliopo mwaka wa pili, tatu na hata wale wa mwaka wa nne ili kuondoa kila asiye na sifa na kwa wale wa mwaka wa kwanza waliokosa mikopo na wanadhani wanazo sifa wakate rufaa kuanzia Novemba Mosi,” amesema Badru.

Wakati HESLB ikijiandaa kufanya hivyo, Kilonzo Mringo, Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFMSO) amesema iwapo bodi ya mikopo itafanya hivyo, wanafunzi wengi watashindwa kuendelea na masomo.

“Mpaka sasa IFM wanafunzi wengi wana sifa na wamenyimwa mikopo, wengine wameamua kusitisha masomo yao na wengine wanasoma kwa kuja chuo wiki moja, nyingine wanaenda kutafuta fedha. Hali ni mbaya, wakiamua kupunguza tena idadi ya wanaopata mikopo basi chuo kitabaki kitupu,” amesema Mringo.

Eliudi Kasunzu, Waziri wa Mikopo katika Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) ameiambia MwanaHALISI Online kuwa hawapingi zoezi la uhakiki lakini wanaishangaa HESLB kuhakiki wanaopata mikopo ambao ni wachache na kuacha kuhakiki wengi walionyimwa.

“Hatuoni mantiki ya kutuhakiki tena kwa kuleta dodoso wanafunzi wajaze, fomu za maombi wanazo huko ofisini kwao wakihitaji kuhakiki basi waziangalie na si kutuingiza kwenye usumbufu wa kujaza dodoso wakati hivi karibuni wamefanya uhakiki wa idadi ya wanufaikaji.

“Hata vigezo walivyoweka mwanzo hawazingatii, tuna orodha kubwa ya wanafunzi yatima, walemavu na wanaosoma masomo yanayotajwa kuwa ni vipaumbele vya taifa lakini bado wamenyimwa mkopo halafu wanataka wachache waliopata wawapunguze zaidi,” amesema.

Boniface Emmanuel, Waziri Mkuu wa DARUSO yeye amesema anadhani kitendo cha HESLB kutaka kuhakiki wanafunzi wanaoendelea na masomo ni mbinu ya kuchelewesha kuwapa fedha zao za kujikimu.

“Kama mtu aliomba mkopo mwaka mmoja, miwili au mitatu iliyopita na akaonekana kwa bajeti na uchambuzi wa wakati huo ana vigezo vya kupata mkopo, iweje umuhakiki mwaka huu? Nadhani wanatafuta kisingizio cha kuchelewa kulipa fedha za kujikimu za awamu zijazo kwa kisingizio cha uhakiki,” amesema Boniface.
Hv haya maswala wanatuigizia wapo serious....
 
Hakikisha una app ya m-bet, meridian bila kusahau kusave bookmark mkekabet.com Hawa jamaa ni waaminifu sana Pesa yao haichelewi wala haina dodoso haina rufaa, haina priority
 
Back
Top Bottom