HESLB yajipanga ‘kuwaliza’ wanafunzi vyuo vikuu

HESLB yajipanga ‘kuwaliza’ wanafunzi vyuo vikuu

Usiwaze kwa kutumia makalio inawezekana hata maana ya mkopo haujui ngoja nikupe ufafanuzi,mkopo huwa ni ada ambayo mwanafunzi analipiwa na serikali moja kwa moja shuleni na si mwanafunzi kupewa,kwa ahadi za magufuli aliahidi elimu bure hadi form 4 yaani hakuna mwanafunzi atakayesoma shule za serikali alafu akaambiwa alipie pesa ya ada au michango yoyote ile kazi ya wazazi itakuwa ni kuwapa watoto wao uniform na madaftari lakini hii si kweli maeneo mengi bado wanafunzi wanachangishwa na baadhi ya shule hazina walimu gazeti la mwananchi liliwahi kuripoti kule tanga shule ina mwalimu mmoja tu anayelazimika kufundisha kuanzia darasa la kwanza hadi la saba,pitia shule za vipaji maaalumu kama Moshi tech,Musoma Tech,Tanga Tech,Ifunda n.k ujionee hali ilivyo mbaya kiufupi serikali imeamua kutoa bora elimu na si elimu bora.

Turudi kwenye mikopo vyuoni huku ndo jipu kabisa unakuta mtu amepewa mkopo wa shilingi mia tano yaani kwenye ada ambayo mtu alitakuwa alipe milioni moja na nusu serikali inamlipia shiling mia tano hii inamfanya mtoto wa maskini atafute milioni moja elfu arobaini na tisa na mia tano ili alipe ada aendelee na masomo bila hivyo arudi kijijini kulima kwa hali hii wataendelea kusoma matajiri tu.
Nimekushambulia nikijua unawatetea wao.

Nilidhani unatukejeli tunaoomba mkopo.
 
Naumia sana tu ila siumii na kujutia kwa wakati mmoja kama ninyi ambao mlimpa kura bwana yule!
Mwanao atakaponyimwa kwa wakati mmoja utamsoma tu
Mimi Nadhani Serikali ingetangaza moja kwa moja kwamba imejitoa kwenye suala la kuwakopesha wanafunzi wote ili wazazi wajue moja, kuliko kuleta usumbufu usio na maana.

By the way, huu ni mkopo siyo msaada kwa sababu mwanafunzi lazima arudishe huko mbeleni. nionavyo mimi serikali haina mpango tena wa kuwekeza kwenye elimu, maana unapoanza kubagua wanafunzi kwa fani wanazosoma ni sawa na kudhani mkono wa kushoto hauna msaada kwenye mwili wa binadamu kwa sababu tu mkono wa kulia upo.

Fani zote ni muhimu na zinategemeana sana katika kuleta maendeleo.

Binafsi napinga aina yoyote ya kuwabagua watu kwa rangi, kabila, dini, vyama, utaifa na sasa huu ubaguzi wa kisasa eti fani unayosomea.

Lissu ulisema haya mapema, usipoguswa leo utaguswa kesho watu wakabaki wanatumbua macho tu..uliomba ushirikiano watu wakabaki kukodoa macho tu.

Leo ametufikia hatujui pakushika, najua umekaa kwenye meza unatushangaa tu. Ngoja turudi nyumbani make pesa inakusanywa na kutunzwa kwa ajili ya kutushonea vazi la taifa na siyo kutukopesha sisi taifa la kesho.

Tatizo la hii nchi ni kubwa sana, shida inakuja pale tunapojadili na kutoa majibu ya muda mfupi. Hii ni nchi ambayo haijui iko katika mrengo gani! Hatujui ni wajamaa au wabepari. Hili ni tatizo kubwa sana kama tupo ujamaa kila kitu kinajulikana namna inavyotakiwa ni kiwa na maana serikali ndio mkurugenzi wa kila kitu ndani ya nchi. Kama ni ubepari maana yake serikali ni msimamizi tu. Mfano kigezo cha mzazi maskini ni kipi? na mzazi tajiri au mwenye uwezo ni kipi? Na hapa ndipo unapozalisha ufisadi. Mfano wenzetu ukifikisha miaka kumi na nane wewe na mzazi mmemalizana inabaki kati ya wewe(18yo) na serikali. Kama mzazi ni tajiri haimzuiii mtoto kukopa pesa kwaajili ya elimu yake kwan atakayefaidika ni yeye na si mzazi. Nitaendelea kurudia kuwa bila kuweka mfumo sahihi tutaendelea kuchanganyana hivi hvi.

NI KINYAAA NA UKAKASI KUSIKIA HABARI KAMA HIZI. MTU KAFIKA MWAKA WA NNE UNATAKA KUMPOKONYA MKOPO! TATIZO VIONGOZI WETU HAWAJAWAI KUONA REACTION ZA WANANCHI.

Una upungufu wa taarifa, tatizo unalolazimisha kuliziba kwa hisia na mapenzi ya chama.
 
usijisumbue vigezo vipya ni kwaajili ya mwaka wa kwanza tuu... aliyepost ni kijakazi wa Mbowe
Huyu jamaa nahisi sehemu kulipotakiwa kuwa na kichwa aliwekewa jiwe, Unabishana na mkurugenzi wa HESLB aliefanya press conference na akatoa maelezo hayo....."Kuna watu ni wachawi mpaka kwa nafsi zao".
 
kule kukabidhiana waliko kabidhiana wakubwa na mmoja akapanda chopa akapelekwa kwao Msoga, hili halikuwemo....?, serikali mnatukosesha amani wazazi, kila uchao ni MABADILIKO kana kwamba leo ndio kwanza suala hili limeanza.
 
SWALI LANGU LA MSINGI NI KUWA;WAKATI WANACHUO WAKIJAZA DODOSO HELA YA BOOM KWA FIRST SEMESTER ZITATOLEWA AMA NDO MPAKA UHAKIKI UISHE??NI ZOEZI LA MWEZI MMOJA KWA MAELEZO YA BODI THAT MEANS NI NOVEMBER MPAKA DECEMBER,VIPI BOOM LA PILI???
Hilo nalo muhim
 
Andamaneni si mlizoea kuandamana JPM hajaribiwi,tangu JPM kaingia madarakani sijawahi kuona maandamano yeyote hongera sana JPM umerudisha nidhamu.
Mdanganye, nipe uzoefu wako hapa duniani ambapo serikali ya mabavu iliwashinda wananchi! Msitake kutuharibia amani yetu. Elimu ya mtu usiichezee kabisa. Mtu amehustle hadi kufika hapo alipo. Hata paka ukimkimbiza sana hugeuka kuwa simba.
 
Tulichagua elimu bule mpaka ya kidato cha NNE mambo ya chuo kikuu nani anayaleta humu?
 
Hivi huyo Abdulrazak Badru, Mujahidini amefikaje hapo na kupewa jukumu zito kama hilo? hebu fuatilieni kuona hata majina ya waliopewa mikopo hilo ni jibu kuweni macho yasije yale ya NSSF ya Dau Kujirudia. Wapi uzoefu wake, wapi elimu yake, hivi alishamaliza hata Masters yake maana tulikua nae darasa moja na hakumaliza shule.

Wazungu wanassema, Garbage In, Garbage Out
Acha ukumya wewe falya kwanini utukane dn za watu pimbi wewe halafu jamii forums ya siki hz haina adabu kabisa
 
Back
Top Bottom