HESLB yajipanga ‘kuwaliza’ wanafunzi vyuo vikuu

HESLB yajipanga ‘kuwaliza’ wanafunzi vyuo vikuu

NI KINYAAA NA UKAKASI KUSIKIA HABARI KAMA HIZI. MTU KAFIKA MWAKA WA NNE UNATAKA KUMPOKONYA MKOPO! TATIZO VIONGOZI WETU HAWAJAWAI KUONA REACTION ZA WANANCHI.
 
Well said Mkuu! Nashukuru kwakunielewe mimi sio mwandishi mzuri wa kile ninachowaza. Ila umegusia jambo zuri sana Vyama vyetu vya siasa vyote hakuna chama chenye itikadi yoyote ile ndio maana kila mtu anahama anavyotaka kwani hakuna wanachoamini. Kwa wenzetu vyama ni kama dini huwezi hama hama tu kila mtu atakushangaa!
Vyama vya siasa vinatokana na social classes.Matabaka katika jamii.

Uingereza huko tulikorithi hizi habari, kuna wafanyakazi walikuwa na Labour, kuna mabwanyenye walikuwa na Conservatives. Ukimsoma Karl Marx na historia ya Industrial Revolution utaona mgongano kati ya wafanyakazi na mabwanyenye waliomiliki viwanda, mgongano huu ndio umezalisha vyama vya siasa organically.

Sisi wote tunatoka tabaka moja la wakulima na wafanyakazi. Tofauti za kitabaka ndiyo kwanza zinaanza kujitokeza sasa. As a result, vyama vya kisiasa vinakuwa overly artificial.

Watu hawana elimu za kuelewa msingi ya social classes ya vyama vya siasa.

Matokeo yake vyama vya siasa vimeanzishwa kuzunguka watu zaidi, sio kuzunguka mirengo ya kisiasa.

Hata public policy inapowekwa, watu wanakosa misingi ya kiitikadi, wanaelewa elea tu.

Katika mfumo kama huo ambao umekosa misingi ya kuelewa vyema tunakotaka kwenda, misingi ya kuelewa tunataka kujenga jamii gani, ni rahisi sana kuchanganyikiwa.

Hatujui tunataka kwenda wapi, tutajuaje njia ya kutufikisha tusikokujua?
 
Nampenda Magufuli kwa moyo wangu wote hasa kuhusu suala la ufisadi lakini katika hili la mikopo hajui anachofanya na itamgharimu sana kisiasa. Pengine kwa vile ana katiba na tume ya uchaguzi vinavyomruhusu kushinda tena na tena yeye na chama chake lakini pia akumbuke kuwa anaowaongoza ni binadamu na binadamu wana ukomo kudadadeki. Kwa nini wanafunzi wote wanaostahili wasipate mikopo kama ilivyokuwa huko nyuma? Kwa nini tunabaguana katika suala muhimu kama elimu? Hii ni hatari sana tena mno. Please stop this nonsense NOW before it's too late!
 
Hahaha jipe moyo,au haujaangalia tv leo?Mkurugenzi Mkuu wa bodi kaweka kila kitu hadharani yaani mwaka huu lazima uisome namba,na wavimbe wapasuke ngenge,acha muisome namba wee lalala mmeichagua wenyewe.
nahisi huyu jamaa kipofu na kiziwi wa akili
 
Nampenda Magufuli kwa moyo wangu wote hasa kuhusu suala la ufisadi lakini katika hili la mikopo hajui anachofanya na itamgharimu sana kisiasa. Pengine kwa vile ana katiba na tume ya uchaguzi vinavyomruhusu kushinda tena na tena yeye na chama chake lakini pia akumbuke kuwa anaowaongoza ni binadamu na binadamu wana ukomo kudadadeki. Kwa nini wanafunzi wote wanaostahili wasipate mikopo kama ilivyokuwa huko nyuma? Kwa nini tunabaguana katika suala muhimu kama elimu? Hii ni hatari sana tena mno. Please stop this nonsense NOW before it's too late!
Nashindwa kuelewa kabisa...ni serikali haina fedha au ni kwamba kila kiongozi kwenye idara yake aonekane anafanya kazi..lakini mwisho wa siku tunaumia sana, sante magu tunyooshe baba
 
Hiyo ndio Tanzania shida yetu kubwa ni USWAHILI mpaka kwenye mambo ya msingi hiyo ndo sababu nasema naipenda Tanzania
 
Mkurugenzi mtendaji wa bodi acha uswahili unahitaji kutafakari zaidi hadi nyuma ya
 
Andamaneni si mlizoea kuandamana JPM hajaribiwi,tangu JPM kaingia madarakani sijawahi kuona maandamano yeyote hongera sana JPM umerudisha nidhamu.
Mkuu yale uliyokuwa unayaona yalikuwa hawajayapiga marufuku, haya yamepigwa pin hadi 2020 utayaanzaje kwa mfano
Mh. Rais Magufuli.. hii Bodi ya mikopo, ni jipu limeiva, limepasuka, na bado linarudia rudia jipu hili.. plse, do all you can, tumbua na kunyofoa kiini cha HELSB... sbb huwezi hakiki mwanafunzi wa mwaka wa pili, tatu na nne wakati walishapewa mikopo miaka yote..

Cha msingi sana ni kudili na wanaoanza vyuo, wafuate vigezo kwa umakini mkubwa... sio ambao tayari walikuwa wana mikopo, hii itawafukuzisha vyuo wengi kwa kukosa ada, boom etc.. ni hatari sana hii
 
Laana ya kuirudisha ccm madarakani itatafuna wengi sana!
Kwa makosa yaliyofanyika tutarajie majuto makubwa hasa kwa wale waliokuwa wakiitikia kibwagizo cha ule wimbo wao maarufu!
Hivi huyo Abdulrazak Badru, Mujahidini amefikaje hapo na kupewa jukumu zito kama hilo? hebu fuatilieni kuona hata majina ya waliopewa mikopo hilo ni jibu kuweni macho yasije yale ya NSSF ya Dau Kujirudia. Wapi uzoefu wake, wapi elimu yake, hivi alishamaliza hata Masters yake maana tulikua nae darasa moja na hakumaliza shule.

Wazungu wanassema, Garbage In, Garbage Out
 
Huyu nae ni kijakazi wa Mbowe?

Taarifa ya Mwananchi online hii hapa:

Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) imesema itaanza uhakiki wa taarifa za wanafunzi wanufaika wanaoendelea na masomo ili kujiridhisha kama wanasifa sitahiki na ambao watakuta hawana sifa watasitishiwa mkopo.

Mkurugenzi wa mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru amesema zoezi hilo litaanza Jumanne na wanafunzi wote watatakiwa kujaza dodoso ambalo litatolewa ambalo litawekwa kwenye mtandao wa bodi hiyo.

"Lengo letu ni kujiridhisha kama wanaonufaika wote kweli wanamahitaji sanjali na kuhakiki orodha yetu upya, katika hilo wale ambao hadhi zao zitaonesha kuwa sio wahitaji watapoteza sifa za kendelea kunufaika na mkopo," alisema Badru.
Lile li dodoso na kimbizana ya muda ya chuo inaboa sana, unakatwa mkopo ukiwa mwaka wa Pili siku upo kazini yanaanza kukukata mpaka ulipoishia inaboa
Mkuu mimi bado hainiingii akilini hiki kinachofanyika hata raisi anakijua kabisa na watajitetea wao waliahidi elimu bure hadi form 4 na si mpaka chuo
 
Eti nauliza hizo dodoso zinaendana na mkataba wa awali wa mkopo wa bodi ambao hujazwa mara 1???
 
Kitu kikubwa amechosema nikuwa wanaangalia vipaumbele vya serikali katika sera ya elimu ya 2014, na mpango wa uchumi 2015/2025.Kwahiyo kwa wanaondelea na masomo pia wanaweza kusimamishiwa mkopo endapo wataona kuwa mnufaika hayupo katika vipaumbelee vyao.Pia kasema mkataba wa maombi yamkopo unawapa mamlaka ya kusitisha mkopo endapo wataona mnufaika hastahili kuendelea kupata mkopo kama atakuwa nje ya vipaumbele vyao.
Ila ukitafakari sana utaona serikali haitaki kupeleka vijana chuo wanamaliza hakuna kazi ndyo maana kutwa wapo na vipaumbele
Tunasubiri TANZANIA YA VIWANDA tunaletewa TANZANIA YA UHAKIKI.kwani nani kawapa mikopo hao wanafunzi?
 
Nampenda Magufuli kwa moyo wangu wote hasa kuhusu suala la ufisadi lakini katika hili la mikopo hajui anachofanya na itamgharimu sana kisiasa. Pengine kwa vile ana katiba na tume ya uchaguzi vinavyomruhusu kushinda tena na tena yeye na chama chake lakini pia akumbuke kuwa anaowaongoza ni binadamu na binadamu wana ukomo kudadadeki. Kwa nini wanafunzi wote wanaostahili wasipate mikopo kama ilivyokuwa huko nyuma? Kwa nini tunabaguana katika suala muhimu kama elimu? Hii ni hatari sana tena mno. Please stop this nonsense NOW before it's too late!
Mpeee tenaaa 2020 akomeshee mafisad kaka
 
Back
Top Bottom