HESABU kitu cha ajabu

HESABU kitu cha ajabu

Chrysanthemum

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
1,933
Reaction score
7,000
Ulifanya ACSEE ukapita vizuri. Maths ukapata A😎
Kwa sababu wewe na hesabu mlikuwa kama mapacha waliozaliwa siku moja, ukaamua kuingia university uchukue Statistics, Pure Mathematics na kila course yenye namba ndani yake. 😂

Ukasema:
“Mimi si fala bana. Dunia inahitaji kujua uwezo wangu.” 😂
Semester ya kwanza ikaenda vizuri tu.
Semester ya pili ndiyo Mungu akaanza kukufundisha humility. 🥲

Kijana wa wenyewe akaanza kunywa dawa za ulcers. 🥵
Usingizi ukawa unaupata kwa msaada wa sleeping pills. 😭
Ukikaa anawaza derivatives.
Ukioga anawaza probability.
Ukilala anaota matrices. 😂😭

SECOND YEAR:
Hapo sasa ndipo degree inaanza kukutengeneza upya. 😂

Lecturer anaingia class, anaanza kuongea kama ana-communicate na viumbe wa sayari nyingine. 👽
Unaangalia board…
Unaangalia lecturer…
Unaangalia notes…
Unaangalia rafiki yako…

Kila mtu ana uso wa:
"Bro… tunaelewa kweli?” 😭😂
Unaamua kuuliza swali.
Lecturer anakasirika:

“I have already explained this!” 😤

Na moyoni unasema:
“Professor, hata wewe sijui kama umeelewa unachotufundisha.” 😂

Nilipofanya ACSEE nilikuwa na A ya Maths, nikaingia university nikachukua kila kitu kilichokuwa na hesabu ndani yake kwa sababu nilijiona mimi ndiye BABA WA MATHEMATICS. 😂😂
Mwaka wa kwanza haujaisha…
Miwani tayari.
Machoni unaona equation hata ukiangalia kuku.

Na ukifika Level 3 Calculus…
Hapo sasa siyo tena education. Ni spiritual warfare. 😭😂
Calculus Level 3 inaweza kukufanya uanze kufikiria:
“Labda nilizaliwa kwa ajili ya kilimo.” 😂😂
Probability nayo usiichezee.
Inaweza kukufanya upungue kilo bila hata kwenda gym. 😭😂

Nadhani wanafunzi wa Engineering nyinyi mliona mengi kwenye lecture halls. 😂😭
Ukisikia mtu anasema:
“Ninateseka na SMA 401…”
Usimcheke, mwangalie kwa huruma. 😭
Kwa sababu huyo amebaki kidogo tu

Mabingwa wa hesabu hali ilikuaje huko?
 
Nakumbuka kipindi nime admit pale mjini kati, akaja mama mmoja kajikwatua 👄 ya pink

Na kuniuliza hujambo,

Mimi, sijambo shikamoo

Aliyejikwatua:: mnasubiri kusajiliwa ndiyo nikamjibu

Eehe course gani,

Mmi, utawala

Yeye, course ngumu kila semester nili sup yaan bora ukasome insurance

Mimi okay mama mkwatuaji

Cc Seran
 
Kwahiyo ukasoma insurance?
 
Mfumo mzima wa elimu tanzania ni mbovu na unavyo kwenda juu ndiyo ubovu unazidi ...nilisema hapa kuwa mishahara ya walimu na madaraja ya walimu wote tanzania izingatie ufaulu wa wanafunzi wao ...hapo ndiyo utakuwa mwisho wa mwalimu wapumbavu na upumbqvu wao... kama amjaona kesho tu walimu wakifundisha kwa heshima na adabu na bidii yote.
 
Ulifanya ACSEE ukapita vizuri. Maths ukapata A😎
Kwa sababu wewe na hesabu mlikuwa kama mapacha waliozaliwa siku moja, ukaamua kuingia university uchukue Statistics, Pure Mathematics na kila course yenye namba ndani yake. 😂
Ukasema:
“Mimi si fala bana. Dunia inahitaji kujua uwezo wangu.” 😂
Semester ya kwanza ikaenda vizuri tu.
Semester ya pili ndiyo Mungu akaanza kukufundisha humility. 🥲

Kijana wa wenyewe akaanza kunywa dawa za ulcers. 🥵
Usingizi ukawa unaupata kwa msaada wa sleeping pills. 😭
Ukikaa anawaza derivatives.
Ukioga anawaza probability.
Ukilala anaota matrices. 😂😭

SECOND YEAR:
Hapo sasa ndipo degree inaanza kukutengeneza upya. 😂

Lecturer anaingia class, anaanza kuongea kama ana-communicate na viumbe wa sayari nyingine. 👽
Unaangalia board…
Unaangalia lecturer…
Unaangalia notes…
Unaangalia rafiki yako…

Kila mtu ana uso wa:
"Bro… tunaelewa kweli?” 😭😂
Unaamua kuuliza swali.
Lecturer anakasirika:

“I have already explained this!” 😤

Na moyoni unasema:
“Professor, hata wewe sijui kama umeelewa unachotufundisha.” 😂

Nilipofanya ACSEE nilikuwa na A ya Maths, nikaingia university nikachukua kila kitu kilichokuwa na hesabu ndani yake kwa sababu nilijiona mimi ndiye BABA WA MATHEMATICS. 😂😂
Mwaka wa kwanza haujaisha…
Miwani tayari.
Machoni unaona equation hata ukiangalia kuku.

Na ukifika Level 3 Calculus…
Hapo sasa siyo tena education. Ni spiritual warfare. 😭😂
Calculus Level 3 inaweza kukufanya uanze kufikiria:
“Labda nilizaliwa kwa ajili ya kilimo.” 😂😂
Probability nayo usiichezee.
Inaweza kukufanya upungue kilo bila hata kwenda gym. 😭😂

Nadhani wanafunzi wa Engineering nyinyi mliona mengi kwenye lecture halls. 😂😭
Ukisikia mtu anasema:
“Ninateseka na SMA 401…”
Usimcheke, mwangalie kwa huruma. 😭
Kwa sababu huyo amebaki kidogo tu

Mabingwa wa hesabu hali ilikuaje huko?
Matatizo ya kusoma kikoloni haya, siku hizi kila kitu cha Stanford na MIT kiko Youtube na zaidi preprint papers zipo www.arxivx.org , unajifunza huku una pause unavyotaka.

Mfano, calculus si ngumu hivyo, ila kuna hesabu kama za factoring, function, trig identities etc, usipozijua, halafu ukalazimishwa kukariri derivative na integral bila kuelewa ni nini, kuelewa calculus ni vigumu.

Tatizo Tanzania kuna watu wanasoma calculus mwanzo mpaka mwisho, ukimuuliza hizi hesabu ni za nini, nielezee kwa lugha nyepesi hata kwa Kiswahili tu, hawawezi kukuelezea. Hawajaelewa, wanakariri.

Tatizo ukiwa unasoma huku una majukumu ya familia hesabu huwezi kuzielewa.

Ukisoma huku unafukuzia wanawali huwezi kuzielewa.

Ukisoma huku unafakamia pombe huwezi kuelewa.

Ukisomeshwa na ma profesa wanaotaka kukukomesha huwezi kuelewa hesabu wala somo lolote.

Ukisoma huku una njaa hujui mlo utatoka wapi, huwezi kuelewa.

Ukisoma kwa kupanda daladala vikumbo vya watu tu vinaondoa ulivjojifunza.

Hesabu zinataka utulivu, kazi yako iwe shule tu, ikibidi uwe kama mfungwa fulani wa hesabu unajiondoa akili kama Grigori Perelman.

Yani wenzako wanaangalia mpira huko, wanafukuzia mademu, wewe una solve ma Riemann Zeta function.

Unakuwa mtawa wa dini ya hesabu.

Wengi hawawezi nidhamu hiyo.
 
Hisabati ni somo ambalo mtu hawezi kushindwa akilijua. Ukitaka kujua hilo, angalia jinsi walimu wanavyoweka alama kwenye hisabati.

Calculus; Ukijua tu ni kanuni gani swali linakuhitaji utumie na ukiandika, unapata alama. POWER RULE, Product rule, ukiandika tu, mwalimu anakupa alama, njia pia ukionyesha inakupa alama. Sasa kuna somo rahisi na zuri kama hesabu?

Katika maswali matano ya hisabati yenye alama 20, ukifanya matatu vizuri. Hupati supp chuo kikuuu. Ukijua hisabati, unajua tu.

Ni sawa na Economics; kuna swali la maelezo, unaweza kwenda OP, lakini swali la hesabu unapata hata 10 kati ya 25. Kwa maoni yangu, hisabati ni somo zuri ukilijua, haliwezi kukuangusha moja kwa moja ni ngumu.

Mtu anaulizwa "mention the rights and the responsibilities of a citizen" ni swali gumu sana hilo. Tofauti na ukiambiwa kwenye Calculus; "Any number power zero is equal to one, demonstrate". Hapo unaelezea basic rule ya integral rule unachukua maksi hizo. 😊
 
Back
Top Bottom