Seran
JF-Expert Member
- Feb 7, 2025
- 32,064
- 91,668
Hostel atateseka vyakula huyu!Unajua hata akikaa kwako, naona haijaakaa poa, hostel ni chaguzi Bora
Mimi hostel nilikaa semester moja, nikaona wasinitanie, ikabidi nikapange nje
Hostel atateseka vyakula huyu!Unajua hata akikaa kwako, naona haijaakaa poa, hostel ni chaguzi Bora
Mimi hostel nilikaa semester moja, nikaona wasinitanie, ikabidi nikapange nje
Ndiyo kilichonifanyaga kukimbia hostel, mimi siwezagi Kula kwa ratiba. Ikifika sjui saa ngapi ukale, Usipoenda kutafuta chakula kitakuwa kimeisha au wamefunga.Hostel atateseka vyakula huyu!
Ndio hapo sasa! Bora uwe na ka geto kako freshy tu!Ndiyo kilichonifanyaga kukimbia hostel, mimi siwezagi Kula kwa ratiba. Ikifika sjui saa ngapi ukale, Usipoenda kutafuta chakula kitakuwa kimeisha au wamefunga.
Mwisho wa siku unaishia Kula vitu vya ajabu, Mimi nakulaga nikijiskia njaa, siwezi Kula Milo mitatu au miwili. Nikijitahidi Sana ni miwili nikiwa na KAZI.
Nikiwa ghetto ninakuwa na focus na consistence, ata saa kumi usiku naweza kupika.
Ngoja na yeye aje na Mathematical Modelling au Analytical Calculus😄Equation x Mathamatician au na wewe upo kijijini tu ulikimbia!
Utayari na dhamira, mazingira (uwezeshaji wa vitendea kazi & aina ya shule na walimu) na utulivu wa akili husababisha ufaulu mzuri kwa mwanafunzi yeyote.Matatizo ya kusoma kikoloni haya, siku hizi kila kitu cha Stanford na MIT kiko Youtube na zaidi preprint papers zipo www.arxivx.org , unajifunza huku una pause unavyotaka.
Mfano, calculus si ngumu hivyo, ila kuna hesabu kama za factoring, function, trig identities etc, usipozijua, halafu ukalazimishwa kukariri derivative na integral bila kuelewa ni nini, kuelewa calculus ni vigumu.
Tatizo Tanzania kuna watu wanasoma calculus mwanzo mpaka mwisho, ukimuuliza hizi hesabu ni za nini, nielezee kwa lugha nyepesi hata kwa Kiswahili tu, hawawezi kukuelezea. Hawajaelewa, wanakariri.
Tatizo ukiwa unasoma huku una majukumu ya familia hesabu huwezi kuzielewa.
Ukisoma huku unafukuzia wanawali huwezi kuzielewa.
Ukisoma huku unafakamia pombe huwezi kuelewa.
Ukisomeshwa na ma profesa wanaotaka kukukomesha huwezi kuelewa hesabu wala somo lolote.
Ukisoma huku una njaa hujui mlo utatoka wapi, huwezi kuelewa.
Ukisoma kwa kupanda daladala vikumbo vya watu tu vinaondoa ulivjojifunza.
Hesabu zinataka utulivu, kazi yako iwe shule tu, ikibidi uwe kama mfungwa fulani wa hesabu unajiondoa akili kama Grigori Perelman.
![]()
Grigori Perelman - Wikipedia
en.wikipedia.org
Yani wenzako wanaangalia mpira huko, wanafukuzia mademu, wewe una solve ma Riemann Zeta function.
Unakuwa mtawa wa dini ya hesabu.
Wengi hawawezi nidhamu hiyo.