Heri ya Siku ya Kuzaliwa Rais Samia

Heri ya Siku ya Kuzaliwa Rais Samia

Happy Birthday, President Dr. Samia Suluhu Hassan! 🎉 On this special day, may your leadership continue to inspire and uplift the nation. Your dedication to progress and unity is commendable, and we wish you success in all your endeavors.

May each year bring new accomplishments, joy, and fulfillment. As you celebrate another year of life, may you find strength, wisdom, and resilience to navigate the challenges ahead. Your leadership has been a beacon of hope, and we are grateful for your commitment to the well-being of the people.

May the coming year be marked by prosperity, peace, and continued strides towards a brighter future. Your vision for a better nation resonates with many, and we are confident that your leadership will leave a lasting positive impact.

Here's to a day filled with joy, surrounded by loved ones, and a year ahead filled with accomplishments and success. Happy Birthday, President Samia Suluhu Hassan! 🥳🇹🇿

Sincerely,
Bright and Genius Editors
www.bgeditors.com
contact@bgeditors.com
Phone: +255687746471
Uteuzi unatafutwa hapa.
 
Samia anatakiwa kuondoka madarakani mara moja maana kazi ya urais haiwezi. Sasa hivi umeme ni mgao kwa zaidi ya miezi sita na hana cha kufanya.

Akili ya kawaida inakataa kabisa, miaka ya magufuli (ambaye alikuwa kiongozi wa hovyo) hapakuwa na mgao. Umeme umeenda wapi? Nini kimetokea?

Huyu hatakiwi kuwa na heri, lolote baya limkute. Hatuwezi kukaa na joto lote hili na hakuna umeme huku yeye anazurura nchi mbalimbali.
Samia kwenye umeme kafeli
Mwendokasi kafeli
Bado wanajenga BRT njia ya Nyerere kuelekea Gongo la Mboto. Sasa sijui wanataka kutuambia nini?
Mimi kuna wakati mpaka naona aibu kumwambia mtu mimi ni Mtanzania.
Kuwa Mtanzania sio suala la kujivunia. Ni suala la kuvumilia.
 
Mheshimiwa waziri mama Dkt. Gwajima D tafadhali sana, naomba mfikishie hili Mh. Rais kwenye vikao vya baraza lenu la mawaziri kaliongee. Ama kama kuna namna nyingine nzuri ya kuongea naye ongea naye, kuhusu suala la umeme.

Kwenye umeme mama Samia binafsi sioni juhudi zake. Kama nakosea naomba mnisamehe na mnikumbushe. Kiangazi mabwawa yanakauka, haya sasa mvua kila siku mbona hakuna nafuu?
Viongozi wa serikali mnatuambia tujiajiri, sawa, lakini mbona umeme wenyewe haupo?

Mnataka tukalime?
Hatuwezi sote kuwa wakulima. Kila mtu anazitazama fursa katika angle yake. Mimi nikitazama mabango sehemu za biashara, magari, nguo, na vifaa vingine naona fursa ya kufanya print works. Naamua kuwekeza nguvu huko, nakaa na mashine zangu masaa 7 hakuna power. What a shameful country?
Vipi kijana wa salon
Vipi kijana wa welding
Vipi kijana wa wooden furniture?
Vipi kuhusu mshonaji? Hata yule aliyeomba cherehani, pengine mtaleletea ya umeme. Mtakuwa mmemsaidia?
Huko mama Samia nchi za watu anakokwenda mara kwa mara hajifunzi? Haulizi, haoni? Wenzetu wanafanyaje kupata reliable sources of energy?

Noneteheless, naomba mfikishie mh Rais alivunje shirika la umeme Tanzania. Tuwe na mamlaka za umeme kila mkoa kama ambavyo inafanyika kwenye maji. Kila mkoa utarithi mali za Tanesco mkoani kwake. Na kila mkoa utafute vyanzo vya uhakika vya umeme. Shida ya umeme ya Mwanza haitakuwepo Dar. Na ya Dar haitakuwepo Dodoma. Nchi nzima tatizo ni moja. Kwanini?
Pengine shirika la umeme Dar es Salaam lingefikiria kuzalisha umeme toka baharini, kuna upepo na mawimbi mengi, Pwani, Lindi, Mtwara wangetumia mto kama Rufiji na Ruvuma na bahari pia.

Wenye umeme wa ziada watauza kwa mikoa yenye uhitaji, bei nzuri ili nao wauze kwa watumiaji wake.
REA iachwe kama ilivyo RUWASA iendelee kushughulikia vijijini huko.

RAIS SAMIA TAFADHALI IVUNJE TANESCO
 
Back
Top Bottom