Michael Amon
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 8,775
- 3,610
Kwanza kabisa tunapaswa kumshukuru Mungu muumba wa mbingu na nchi pamoja na vyote vilivyomo ndani yake kwa kutulinda na kutujalia afya njema katika kipindi kizima cha mwaka 2012. Tuzidi kumuomba ili aweze kutujalia zaidi na zaidi katika kipindi kiajcho cha mwaka 2013 na kuendelea kwani yeye ndiye muweza wa yote.
Ninapenda kuchukua nafasi hii kutoa salamu za dhati kwa wana JF na wananchi wote kwa ujumla katika kipindi hiki cha msimu wa sikuu ya Krismasi na huku tukijiandaa kuukaribisha mwaka mpya 2013 ambao tutakuwa tumeufikia ndani ya siku chache zijazo.
Kama kuna mahali niliwakosea katika kipindi kilichopita naomba mniwie radhi kwani mimi pia ni binadamu na kila binadamu ana mapungufu yake na kusameheana ndio muendelezo mzuri wa maisha yetu na kwa yale mema tuliyoyafanya kwa kipindi hicho. Nawasihi tusiyaache na tuyaendeleze zaidi na zaidi.
Wapendwa wana JF naomba kuwaasa kuwa na amani na utulivu katika kusherehekea sikuu ya krismasi na mwaka mpya kwani ni mengi ambayo hutokea katika kipindi hiki, hivyo basi yatupasa kujipanga vizuri na tusherehekee kwa amani na utulivu.
Baada ya kusema haya machache naomba niwatakie sikukuu njema ya Krismasi na makaribisho mema ya mwaka mpya 2013 wanachi na wadau wote wa JF popote mlipo. Pia naomba niwape nafasi na nyie wadau muweze kutuma salamu zenu za sikukuu kwa muwapendao kupitia thread hii.
Last edited by a moderator: