Heri ya Krismas na Mwaka Mpya 2013

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,591
Merry-Christmas.gif
Wapendwa wana JF, ni matumaini yangu kuwa nyote mu wazima wa afya na mnaendelea vyema na shughuli zenu za kila siku.

Kwanza kabisa tunapaswa kumshukuru Mungu muumba wa mbingu na nchi pamoja na vyote vilivyomo ndani yake kwa kutulinda na kutujalia afya njema katika kipindi kizima cha mwaka 2012. Tuzidi kumuomba ili aweze kutujalia zaidi na zaidi katika kipindi kiajcho cha mwaka 2013 na kuendelea kwani yeye ndiye muweza wa yote.

Ninapenda kuchukua nafasi hii kutoa salamu za dhati kwa wana JF na wananchi wote kwa ujumla katika kipindi hiki cha msimu wa sikuu ya Krismasi na huku tukijiandaa kuukaribisha mwaka mpya 2013 ambao tutakuwa tumeufikia ndani ya siku chache zijazo.

Kama kuna mahali niliwakosea katika kipindi kilichopita naomba mniwie radhi kwani mimi pia ni binadamu na kila binadamu ana mapungufu yake na kusameheana ndio muendelezo mzuri wa maisha yetu na kwa yale mema tuliyoyafanya kwa kipindi hicho. Nawasihi tusiyaache na tuyaendeleze zaidi na zaidi.

Wapendwa wana JF naomba kuwaasa kuwa na amani na utulivu katika kusherehekea sikuu ya krismasi na mwaka mpya kwani ni mengi ambayo hutokea katika kipindi hiki, hivyo basi yatupasa kujipanga vizuri na tusherehekee kwa amani na utulivu.

Baada ya kusema haya machache naomba niwatakie sikukuu njema ya Krismasi na makaribisho mema ya mwaka mpya 2013 wanachi na wadau wote wa JF popote mlipo. Pia naomba niwape nafasi na nyie wadau muweze kutuma salamu zenu za sikukuu kwa muwapendao kupitia thread hii.

Last edited by a moderator:
Asante sana Mkuu
Kwa wakati huu ni muda wa kutafakari ni wapi tulikosea na wapi twapaswa kujisahihisha ili kuweza kurudi katika mstari ulioonyooka
Kimaisha pia ni wakati wa kutafakari ni yapi tuliyafanya kwa ufanisi katika mipango yetu ya mwaka huu na wapi ambapo tulishindwa kufikia malengo yetu
Asante sana na tuombeane tuweze kuumaliza mwaka huu salama
Asante sana Meezy na akina Arushaone, Erickb52, Baba V, Kaunga, AshaDii, Asprin< Bishanga, Blaki Womani, sweetlady, snowhite, HorsePower, Preta, gfsonwin, Filipo, St. Paka Mweusi @st. ivuga, marejesho, na my wife wangu mpendwa Dena Amsi nawatakia maandalizi mema ya sikukuu zijazo hapa
 
Asante sana Meezy na akina Arushaone, Erickb52, Baba V, Kaunga, AshaDii, Asprin< Bishanga, Blaki Womani, sweetlady, snowhite, HorsePower, Preta, gfsonwin, Filipo, St. Paka Mweusi Saint Ivuga, marejesho, na my wife wangu mpendwa Dena Amsi nawatakia maandalizi mema ya sikukuu zijazo hapa

Salamu zimefika. Pamoja sana mkuu.
 
stevoh sijakusahau bana heri ya xmass na mwaka mpya ujao mkuu
najua mwaliko wako upo kamili
 
Last edited by a moderator:
Asante sana Mkuu
Kwa wakati huu ni muda wa kutafakari ni wapi tulikosea na wapi twapaswa kujisahihisha ili kuweza kurudi katika mstari ulioonyooka
Kimaisha pia ni wakati wa kutafakari ni yapi tuliyafanya kwa ufanisi katika mipango yetu ya mwaka huu na wapi ambapo tulishindwa kufikia malengo yetu
Asante sana na tuombeane tuweze kuumaliza mwaka huu salama
Asante sana Meezy na akina Arushaone, Erickb52, Baba V, Kaunga, AshaDii, Asprin< Bishanga, Blaki Womani, sweetlady, snowhite, HorsePower, Preta, gfsonwin, Filipo, St. Paka Mweusi @st. ivuga, marejesho, na my wife wangu mpendwa Dena Amsi nawatakia maandalizi mema ya sikukuu zijazo hapa
Ahsante Mr Rocky ! Ubarikiwe
 
Asante kutukumbuka, Pamoja daima!
 
Mkuu Meezy shukrani sana!

Uwe na maandalizi mema ya krismas na mwaka mpya! Mwenyezi Mungu akujalie afya njema!

Afu karibu moshi kwetu!
 
Last edited by a moderator:
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom