Hela ndogo ndogo unazozidharau ndo chanzo cha kufeli kwenye maisha yako

amshapopo

JF-Expert Member
Sep 7, 2014
733
1,273
Wasalam,

Watanzania wengi tumekuwa na tabia ya kudharau pesa ndogo ndogo tuzipatazo. Chukulia mtu anaingiza ujira wa 10,000 kwa siku anakula na kutumia yote bila kusave chochote. Just imagine kama angesevu hata 3,000 kila siku kwa mwezi angeweza hata nunua mfuko wa mbolea kutosha kuanzia kulima hata mahindi. Angeweza nunua hata kuku ama mbuzi kuanzisha mtaji.

Mfano bei ya mbuzi ama kuku zinashuka sana kuanzia mwezi wa kwanza mwishoni Hadi mwezi wa tatu hapo unaweza ukanunua kwa bei chee ukafuga ukaja uza kwa faida mwezi wa 10-12.

- Ishi kwa malengo Ili upige hatua kwenye maisha.
  • Bajeti ya maskini tajiri haiwezi. Jibane kwa mda ufanikishe usione aibu kuchekwa bahili.
  • Mbele ni kweupe ukianza jibana leo na kuwekeza.
  • Omba mungu sana kwa kila ufanyalo coz maharamia no wengi.
  • Usijilinganishe na wengine, utatengeneza sonona na kukata tamaa

Mwisho, Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe usidharau hela hata kama ni ndogo kwani kitu kikubwa huanza na kidogo.

Asante.
 
Binafsi michango ya harusi naumia sana nikitoa maana ni upotevu wa hela tu japokua michango mingine ni midogo.
 
Mkuu,umenena vyema…ujumbe bora sana

Haba na haba hujaza kibaba

Kuna kitu kinaitwa compounding effect

Kupata chakula na kukila chote n tabia ya kitoto.

Kupata fedha na kuitumia yote n moja kati ya tabia ya hovyo sana.

Mtu mmoja mwenye hekima aliwah kusema “kwa kila fedha unayoipata,kiasi fulan lazima kitengwe kwaajil ya kesho yako.
 
Very Sure
 
Back
Top Bottom