Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,447
- 7,830
John Heche
Akiwa kwenye mjadala wasafi fm, John Heche amekanusha uvumi aliolizwa na mwandishi kuhusu kuwepo kambi mbili ndani ya Chadema huku yeye Heche akiwa kambi ya Tundu Lissu.
Heche amesema mara ya kwanza kuingia kikao cha kamati kuu ilikuwa 2011 na alikuta mjadala wa fedha unajadiliwa, Heche anasema jinsi watu walivyokuwa wanavutana alijua ndio siku ya chama kupasuka ambapo Dk. Slaa alibananishwa na kina Mabere Marando na prof. Baregu.
Heche amesema hawawezi kuwa na uongozi ambao hauwezi kuhojiwa.
Kuhusu Mbowe kuwa mwenyekiti muda mrefu(miaka 19), amesema ni jambo zuri akiachia mtu mwingine lakini wanaoongea hivyo wachukue fomu, hawawezi kumuondoa mwenyekiti na chama kibaki bila mwenyekiti.