Hebu Sikieni Furaha Yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hebu Sikieni Furaha Yangu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ms Judith, Jan 17, 2011.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  leo nimepata furaha kubwa sana. kuna mkaka mmoja aliwahi kuniapproach miaka ya nyuma akitaka kunichumbia na aliniambia ukweli kuwa alishadivorce na alipata mtoto mmoja kabla ya hiyo talaka. siku moja nikampa mtihani kuwa ampigie mtalaka wake simu mbele yangu amwambie kuwa licha ya talaka yao, anaomba wazae mtoto mmoja zaidi kwani hapendi kuwa na watoto na wanawake tofauti. alisita sana kwani alisema mtalaka wake ana maneno makali sana tena saa nyingine ya kashfa na angeweza kumtukana. baada ya kumhakikishia kuwa kama atamtukana nitamkubalia ombi lake palepale, alikubali.

  alipompigia, mkewe alikuwa tofauti na alivyomtarajia. alicheka kwanza kwa mzaha, baadaye akamuuliza "leo una nini wewe, kitu gani kimekupata hadi unafikiria hivyo? natamani nikuone leo nijue kilichokupata!" walipokata simu alishangaa sana kwa maongezi yale, nilimwambia kuwa Mungu akishaunganisha watu huwa hawawezi kutengana, nikamwambia aendelee kumpigia simu kama hizo na amtafute ila akimkataa, tutakubaliana kuoana. sasa leo kanipigia simu anasema kuwa kakubali kuzaa naye! wow. God is at work! i am soooooo happy wapendwa.

  jamani ALICHOKIUNGANISHA MUNGU, MWANDAMU ASIKITENGANISHE please!!!!!!!!!!!!!
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ulikuwa unangoja mkono uanguke uudake..ha ha haaaaa!
  Jitafutie mtu wako bana...kwanini usubiri aliyekataliwa?
  Mi siamini kama furaha yako hiyo ni ya ukweli, maana ni kisebusebu na kiroho papo, yaani ile nataka sitaki!..
   
 3. RR

  RR JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Kwamba umefurahi kushtuka ungeweza kutendwa???
   
 4. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  hapana kaka, ni kuwa nisingemkubalia kwa kuwa wakati ule nilikuwa bado nasoma na pia sijisikii kuwa na mtu ambaye alishaoa na kuacha so, nilikuwa namuombea kwa Mungu amsaidie wasameheane na mwenzake badala ya kutafuta wapya na Mungu amejibu maombi yangu. ndiyo siri ya furaha yangu
   
 5. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  hapana kumbuka talaka si mpango wa Mungu na mie wakati ule nilikuwa nasoma, so nilikuwa sihitaji kuingia kwenye masuala ya ndoa na kusema kweli ile ilikuwa ni njia ya "kidiplomasia" tu ya kumkataa, lakini Mungu akajibu maombi yetu.
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hahahaha ulikuwa unanyatia kama fisi mkono udondoke wewe ndo udake!! hahaha sasa haujadondoka duh wanawake bana
   
 7. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Huyu nae kaanza mambo ya bujibuji..
  Bora tu waoane
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Huyu waoane na Bujibuji sio?
   
 9. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  KWAMBA amewwaunganisha waliojitenganisha
   
 10. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  lo, wanaume bwana hisia zenu zote ni hukohuko. wala sikuwa namtaka nilikuwa nataka kuwapatanisha. halafu sikuwa na mpango na ndoa wakti huo kwani nilkuwa bado niko chuoni
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Aaaah kumbe naona huyo mwanaume halipi angekuwa analipa angemdaka juu kwa juu
   
 12. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  ya buji2 ni yapi hayo?
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Nani kakwambia watu wakiwa chuoni hawaolewi?
   
 14. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mmmh mimekuelewa sana mpz lkn unadhani ww hasa ni sababu ya wao kurudiana? walikuwa wanapendana hao na its only a mata of time and time heals everything,jamaa alikuwa bado in dilema lkn kiukweli anampenda mkewe,angekuwa na nia na ww hasaaaaa,wala hata sim asingepiga kwa huyo mkewe sema tu matatizo yalimfanya aje na gia ya kukuoa.lkn kiukweli ulitakiwa kustuka mapemaaaaaaaaaaaa,wengi tunao mtaani,marafiki zetu,ndugu zetu etc ugonjwa wa mapenzi ni mby sana na wala hauna tiba!
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Jan 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,854
  Likes Received: 83,324
  Trophy Points: 280
  Judy namfahamu dada mmoja msomi wa hali ya juu na ni maarufu sana pale Muhimbili. Huyu alizaa na mume lakini wakashindana na hatimaye ndoa yao kuvunjika wakiwa na mtoto mmoja. Huyo dada wakati yuko majuu akaamua kupata mtoto wa pili lakini hakutaka kuzaa na mwanaume mwingine ila yule yule waliyezaa naye mtoto wao wa kwanza.

  Watu wengi walimhoji kwamba mwisho wa ndoa yao haukuwa mzuri je haoni kama kufanya kitu kama hicho kunaweza kukasababisha matatizo mbele ya safari. Akadai kwamba hataki kuolewa tena na asingependa watoto wake kila mmoja awe na baba tofauti. Hivyo akamjulisha mwenzie kwamba atakuwa Dar na nia yake hiyo ya kupata mimba nyingine toka kwa mwanaume yule na mimba kweli ikaitika. Sidhani kama kulikuwa na mapenzi ya kweli zaidi ya kubebeshwa mimba.

  Mdada baada ya kushika mimba akakata kabisa mawasiliano sijui katika siku za hivi karibuni kama yamerudi tena. Na alishajifungua muda mwingi tu. Kwa hiyo inawezekana kabisa huyo mdada bado anataka kuendelea na jamaa ingawaje jamaa hataki kufanya hivyo. Hii ndiyo sababu dada huyo kakubali kirahisi kushika mimba tena ya huyo jamaa.
   
 16. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #16
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  true sister
   
 17. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #17
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  haha, wengine hatuangalii hayo kaka
   
 18. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #18
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  kila mtu na mipango yake kaka
   
 19. RR

  RR JF-Expert Member

  #19
  Jan 17, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Orait...got u....so it wasn't for u.... it was rather for them.....
  Hivi katika hili who wanted ana out....him or her?
   
 20. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #20
  Jan 17, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hii ngumu kumeza Miss Judith!!!!!!
   
Loading...