Fahamu kuhusu Talaka na taratibu zake Kisheria

Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
112
95
FAHAMU kuhusu TALAKA na taratibu zake KISHERIA.

It's me
Mr George Francis
0713736006
mr.georgefrancis21@gmail.com

TALAKA ni ruhusa au amri ya kisheria inayotolewa na Mahakama pale ambapo mume au mke anataka kumwacha mwenzake. Hii ni hati inayoidhinisha kuvunjika kwa ndoa baina ya wanandoa.

Na ili tuseme ndoa imevunjika ni lazima talaka itolewe na ili TALAKA itolewe ni lazima Mahakama ijiridhishe kuwa ndoa hiyo imevunjika kiasi cha kutoweza kurekebishika yaani haiwezekani tena kwa wanandoa hao kuweza kuendelea na ndoa hiyo. Soma kifungu cha 99 cha Sheria ya Ndoa.

Kama hakuna TALAKA iliyotolewa lakini wanandoa wameacha kuishi tena pamoja, hapo tunasema wametengana tu lakini hawajaachana. Kutengana sio TALAKA. Kutengana ni hali ya mume na mke kuacha kuishi pamoja au kukaa mbalimbali. Kutengana kunaweza kuwa kwa mapatano kati ya wanandoa hao au kwa amri ya Mahakama. Mahakama itatoa amri hiyo endapo mmoja ya wanandoa atapeleka maombi Mahakamani.

Lengo la wanadoa kutengana ni kutaka kuwapa wanandoa hao muda wa kutafakari kama wanaweza kuendelea na ndoa hiyo au la. Baadae wanaweza kusameheana na kurudiana au kuishi tena pamoja. Lakini kuachana kwa TALAKA lengo ni kutokuwa na nia ya kutaka kurudiana tena kutokana na sababu zisizoweza kurekebishika.

Ukienda kusoma Mathayo 5 : 31 neno la Mungu linasema
"Imenenwa pia, mtu akimwacha mkewe na ampe hati ya TALAKA."
Kumbe TALAKA ni muhimu ili kuthibisha kuwa ndoa imevunjika na haipo tena. Baada ya TALAKA kutolewa, mume au mke atakuwa huru kuoa au kuolewa na mtu mwingine.

Join Telegram: TANZANIA LAWYERS FORUM 🎓

Chombo chenye mamlaka ya kutoa TALAKA ni Mahakama tu. Mahakama hiyo itatoa TALAKA kwa ndoa ambayo imedumu kwa miaka miwili au zaidi isipokuwa tu endapo mlalamikaji au mwombaji wa TALAKA ataoa sababu za msingi zitakazo onesha ugumu wa kuendelea kwa ndoa hiyo. Soma kifungu cha 100 (1)&(2) cha Sheria ya Ndoa.

Mwanandoa kabla ya kupeleka ombi au shauri la TALAKA Mahakamani, hatua ya kwanza anatakiwa kupeleka malalamiko kwenye Baraza la usuluhishi la ndoa yanayoanzishwa na waziri mwenye dhamana katika maswala ya ndoa takribani kila kata.

Mwanandoa anaweza kupeleka pia malalamiko yake katika mabaraza mengine yaliyoanzishwa katika jumuiya husika kwa dhumuni la kufanya kazi ya usuluhishi kama ilivyo katika Baraza la usuluhishi la ndoa. Soma kifungu cha 102(1)&(2) cha Sheria ya Ndoa.
Mfano kupeleka shauri katika ustawi wa jamii au mabaraza ya dini kama vile BAKWATA kwa waumini wa dini ya kiislamu au Kanisani katika mabaraza yanayohusiana na usuluhishi wa migogoro ya ndoa.

Baraza litasikiliza na endapo litashindwa kusuluhisha au kupata muafaka stahiki kati ya wanandoa hao basi Baraza litatoa cheti ambacho kitaonesha kuwa limeshindwa kusuluhisha mgogoro wa ndoa. Hapo sasa mwanadoa anaweza kupeleka shauri lake Mahakamani akiwa ametayarisha madai yake ya TALAKA.

Madai ya TALAKA yanatakiwa kuonesha mambo kama vile
✓Majina ya wanandoa
✓ Majina ya watoto, jinsia na umri wao
✓Sababu za kupeleka shauri hilo Mahakamani
✓Taarifa za mwenendo au kesi yoyote iliopita
✓Makubaliano yoyote kuhusiana na matunzo au mgawanyo wa mali za familia
✓Madai husika ya nini anataka kifanyike. Kuongeza maalifa soma kifungu cha 106(1)(a-g) cha Sheria ya Ndoa.

Maombi ya madai ya TALAKA yanatakiwa yaambatanishwe na hati iliyotolewa na Baraza la usuluishi ndani ya miezi sita kabla ya kupeleka shauri hilo la madai ya TALAKA Mahakamani. Hii ni Kwa mujibu wa vifungu vya 106(2) na 104(5) vya Sheria ya Ndoa.

Hati ya Baraza la usuluhishi haitahitajika endapo mambo yafuatayo yatathibitika
✓Mwombaji wa TALAKA alitelekezwa na hajui wapi alipo mwanandoa mwenzake.
✓Mlalamikiwa anaishi nje ya Tanzania na inaonekana kutokuwa na uwezekano wa kufika Mahakamani ndani ya miezi sita baada ya siku ambayo shauri husika limefikishwa Mahakamani.
✓Endapo mlalamikiwa alitakiwa kuhudhuria katika Baraza la usuluhishi lakini alishindwa kufika kwa makusudi.
✓Endapo mlalamikiwa amefungwa gerezani kifungo cha maisha au kwa kipindi cha miaka takribani mitano.
✓Endapo mlalamikaji atathibisha kwamba mlalamikiwa amepata ukichaa au ugonjwa wa akili usiotibika.
✓Endapo Mahakama itajiridhisha kuwa kuna sababu zilizo nje ya uwezo zinazopelekea hati ya Baraza la usuluhishi ishitajike.
Hii ni kwa mujibu wa vifungu vya 106(2) na 101(a-f) vya Sheria ya Ndoa.

Kutoa TALAKA sio kipaumbele cha Mahakama ndio maana sheria inasisitiza kesi za migogoro ya ndoa na TALAKA zianzie katika mabaraza ya usuluhishi ili kusudi wahusika waweze kusuluhishwa na kumaliza tofauti zao.

Mahakama haiwezi kuruhusu TALAKA pale ambapo mwombaji wa TALAKA ndiye mwenye makosa. Huwezi kupata haki juu ya makosa yako mwenyewe. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 107(1)(a) cha Sheria ya Ndoa.

Ni lazima pawepo na sababu ya msingi ili Mahakama iruhusu kutolewa kwa TALAKA. Ni lazima ndoa ionekane kuwa imevunjika kiasi cha kutoweza kurekebishika. Sababu zinazoweza kuthibitisha kuwa ndoa evunjika kiasi cha kutoweza kurekebishika ni kama hizi zifuatazo.
(a). Uzinzi uliopitiliza (adultery) - Hii ni zinaa inayofanywa kati ya mwanaume na mwanamke tofauti na mume au mke halali wa ndoa.
Kwa lugha nyingine tunasema ...
"Adultery - means a voluntary sexual intercourse between a married person and someone other than their lawful spouse.

Uzinifu unaweza kuwa sababu inayopelekea TALAKA. Hili sababu hii ya uzinifu iweze kukubaliwa ni lazima mlalamikiwa awe ameshiriki zinaa na mtu mwingine tofauti na mume au mke wake. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 107(2)(a) cha Sheria ya Ndoa.

Kufanya zinaa sio lazima kuwe na mwingiliano uliokamilika kati ya washiriki wa zinaa hiyo. Hatakama uume haujaingia vizuri kwenye uke bado itahesabika kuwa mwanaume au mwanamke anayelalamikiwa amefanya uzinzi.
Mfano: Kwenye kesi ya DENIS vs DENIS, Mahakama iliamua kwamba "any degree of penetration however slight will suffice."

Kwa mujibu wa kesi hii, mwanaume nawanamke wakifumaniwa wamelala pamoja itasemekana kuwa wamefanya uzinifu na ikumbukwe pia sio rahisi kupinga isipokuwa labda mwanaume huyo anayetuhumiwa kushiriki zinaa athibitike kuwa ni anisi (impotent), yaani uume wake hauna uwezo wa kusimama.

(TAHADHARI: Hii ni sheria ya ndoa, na hapa naelezea mambo ya ndoa, hivyo usijali kuhusu misamiati inayotumika. Kikubwa ni kukufanya uelewe na kuifurahia mada hii.

It's me
Mr George Francis
0713736006
mr.georgefrancis21@gmail.com

Endelea kusoma..

Sasa hili mlalamikiwa akutwe na hatia ya uzinzi ni lazima awe amefanya kitendo hicho kwa hiari yake. Hivyo basi, mwanamke aliyebakwa hatohesabika kuwa amefanya uzinzi. Hii ni kwasababu ameshiriki tendo la zinaa kwa kulazimishwa au pasipo hiari yake. Lakini jukumu la kuthibitisha kuwa kweli amebakwa na hakufanya kwa hiari yake lipo upande wake.

Mazingira yafuatayo yanaonesha kutendeka kwa kosa la uzinifu.
✓Kulala pamoja hotelini au gest house na mtu ambaye sio mume wala mke halali wa ndoa.
✓Kwenda katika madanguro
✓Kuishi uchumba na mtu mwingine
✓Kuzaa na mtu mwingine
✓Kuoa mtu mwingine wakati tiari upo kwenye ndoa inayoendelea. (Conviction of bigamy) na mazingira mengine yanayo endana na haya.

(b) Ukatili (Cruelty) - Hii ni hali ya kuumiza au kusababisha madhara kwa mtu mwingine. Ukatili unaweza kuwa ni wa kihisia au wa kudhuru mwili wa unaofanywa na mume au mke kwa mwenza wake au kwa watoto. Kutokana na vitendo vya ukatili Mahakama inaweza kutoa amri ya TALAKA na kuvunja ndoa. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 107(2)(c) cha Sheria ya Ndoa.

Lakini ikumbukwe kwamba katika maisha ya ndoa kupishana kauli, kugombana au kukwaruzana ni mambo yanyokubalika lakini mambo hayo yasivuke kiwango.
Mfano: kwenye kesi ya CHARLES AOKO vs DORINA GIBOGA, Mahakama iliamua kwamba
"matukio mawili ya kumpiga mwanamke hakuwezi kufanya ndoa ivunjike kiasi cha kushindwa kurekebishika. Hizo ndio raha na shida zenyewe katika ndoa."

Lakini katika kesi ya SAID MOHAMED vs ZENA ALLY, Mahakama iliamua kwamba
"kitendo cha mwanaume kumpiga mkewe na kumvua nguo zake mbele za watu na mbele za baba yake mkwe kilikuwa ni kitendo cha ukatili kilichopelekea madhara ya kimwili na kiakili."

Mambo yanayoashiria vitendo vya ukatili katika ndoa ni kama haya yafuatayo.
✓Ukatili wa kudhuru mwili
✓Ukatili wa kijinsia
✓Unyanyasaji au Ukatili wa kihisia
✓Vitisho na lugha za matusi
✓Kulazimisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile au kulawiti.

Hivyo, ukatili dhidi ya mke au mume unaweza kuwa ni sababu mojawapo inayoweza kuifanya Mahakama kutoa amri ya TALAKA.

(c). Kutekeleza au Uasi (Desertion). - Hii ni hali ya kutelekeza familia. Mume au mke ana haki ya kudai TALAKA endapo mume au mke wake ameamua kuiacha familia na kwenda kuishi mahala pengine kwa hiari yake mwenyewe bila sababu yoyote ya msingi kwa miaka agharau mitatu. Mahakama inaweza kutoa amri ya TALAKA endapo hilo litathibitishwa na mlalamikaji. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 107(2)(e) cha Sheria ya Ndoa.

Kunaweza kuwa na simple desertion yaani mume au mke kuamua kuacha kuishi pamoja na mwenza wake. Wakati mwingine wanaweza kuishi wote katika nyumba moja lakini mume au mke hataki kushirikiana chochote na mwenza wake.

Lakini pia kunaweza kuwa na constructive desertion, ambako mume au mke anaweza kufanya matendo ambayo yanaweza kumsababisha mwenza wake aondoke hapo nyumbani. Kama wewe ndio umekuwa chanzo cha mume au mke wako kuchukua maamuzi ya kuondoka huwezi kuibuka na kudai TALAKA kanakwamba mwenye kosa sio wewe.
Huwezi kudai TALAKA chini ya sababu hii kama wewe ndio sababu ya mume au mke wako kuacha familia na kuondoka. Lakini unaweza kudai TALAKA kama wewe ndiye uliyeondoka kutokana na sababu zisizoweza kuvumilika zilizofanywa na mume au mke wako. Mfano, kutishiwa kuuwawa, vipigo vya malakwamala na mambo mengine kama hayo.
Hivyo, inatakiwa mtu awe ametelekeza familia kwa miaka angharau mitatu na iwe amefanya hivyo kwa hiari yake mwenyewe.

(d). Kifungo cha jela - mume au mke anaweza kuomba Mahakama itoe amri ya TALAKA, endapo mume au mke wake amefungwa kifungo cha maisha jela au kifungo kisichopungua miaka mitano. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 107(2)(g) cha Sheria ya Ndoa.

(e). Ukichaa au ugonjwa wa akili.
Hii ni hali ya kutokuwa na akili timamu kulikothibitishwa na madaktari bingwa wa akili. Madaktari bingwa hao ni lazima wathibitishe kuwa hakuna matumaini ya kupata nafuu au kupona. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 107(2)(h) cha Sheria ya Ndoa.

KWA UJUMLA, sababu zipo nyingi hizi ni baadhi tu ya sababu ambazo endapo zitathibitika na kwa kuzingatia na ushahidi pamoja na mazingira mengine, basi Mahakama inaweza kutoa amri ya TALAKA kama ilivyoombwa na mmoja kati ya wanandoa husika.

It's me
Mr George Francis
0713736006
mr.georgefrancis21@gmail.com

MUHIMU
Kama kawaida kila jambo lina mipaka yake. Hivyo hata katika utoaji wa TALAKA pia kuna mipaka. Kuna sababu ambazo zinaweza kuifanya Mahakama isikubali kutoa amri ya TALAKA. Sababu hizo ni kama hizi zifuatazo.
(i). Kama mwombaji wa TALAKA ndiye mwenye makosa. Hivyo, huwezi kunufaika kwa makosa yako mwenyewe. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 107(1)(a).
Mfano: Katika kesi ya ATHANAS MAKINGWA vs DARIN HASSAN, Mahakama ilisema kwamba
"Kama kosa ni la mwenyewe anayeomba TALAKA bila sababu maalumu, amri ya TALAKA haitatolewa."

(ii). Kula njama (collusion). - Hiki ni kitendo cha wanandoa kula njama ya kuidanganya Mahakama. Kutokana na sababu hii Mahakama itatupilia mbali madai ya TALAKA yaliyowasilishwa Mahakamani. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 87 cha Sheria ya Ndoa.

Hiki ni kitendo ambacho wanandoa wamekubaliana kuficha ukweli au kutoeleza ukweli wote mbele ya Mahakama. Hapa hawatoi maelezo yenye kusaidia kubaini ukweli wa tatizo lao au kuzalisha story za uongo ilimradi tu Mahakama ikubali kutoa amri ya TALAKA. Hivyo basi, kutokana na sababu hii Mahakama haitakubali kutoa amri ya TALAKA.

(iii). Kupuuza au kusamehe au kujifanya kutoona. (Condonation). Hii ni hali ambayo mume au mke kupuuzia kosa ambalo limetendwa na mke au mume wake. Mahakama haitakubali kutoa amri ya TALAKA kama ikigundua kuwa mume au mke alionesha kuvumilia au kupuuza kosa lililowahi kufanywa na mke au mume wake. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 86 cha Sheria ya Ndoa.

Viashiria vinavyoonesha kuwepo kwa hali hii ya kupuuza makosa ni kama hivi vifuatavyo.
✓Kujua kosa lililotendeka
✓ Kusamehe kwa kutoamua kuchukua hatua
✓Kuonesha kuwa kosa hilo linavumilika.
Mfano: kwenye kesi ya MARIAM TUMBO vs HAROLD TUMBO,
"Mwanaume alifanya uzinifu kwa kwenda kuishi na mwanamke mwingine. Mkewe wa ndoa alijua lakini hakuchukua hatua zozote. Hivyo, Mahakama iliamua kuwepo kwa hali ya kuvumilika na haikutoa amri ya TALAKA. Mke halali wa ndoa katika kesi hii alijua kuwa mume wake anaishi pia na mwanamke mwingine kwa miaka minne lakini alivumilia na hakuchukua hatua zozote. Bada ya miaka minne ndio akapeleka shauri Mahakamani akidai kupewa TALAKA kwa kosa ambalo aliweza kulivulia kwa miaka minne. Mahakama iliona kuwa kama aliweza kupuuza kwa miaka yote hiyo minne basi kosa hilo linavumilika, hivyo haikutoa amri ya TALAKA.

(iv). Ushirikiano katika kutenda kosa. (Connivance). Hii ni hali ya wanandoa wenyewe kushirikiana katika kuruhusu uzinifu. Mahakama haiwezi kuridhia kutoa amri ya TALAKA kwasababu wahusika wote wawili wameshirikiana katika kuruhusu uzinifu kati yao. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 85 cha Sheria ya Ndoa.

Hapa kuna
~ushirikiano wa mojakwamoja (active connivance) na

~ushirikiano usio wa mojai (passive connivance.)

Katika ushirikiano wa mojakwamoja, mume au mke anakuwa amerihusu mke au mume wake afanye uzinifu na mtu mwingine kwa sababu zao binafsi. Mfano: mke anamruhusu mume wake afanye zinaa na mfanyakazi wao wa kazi za ndani.
Mfano hai ni katika kesi ya RICHMOND vs RICHMOND,
"ambapo watu wawili waliopo kwenye ndoa walikubaliana kubadirishana wanawake" hapa huwezi kuja kudai Mahakama itoe amri ya TALAKA kwa kosa la uzinifu wakati mlalamikaji amekubali mwenyewe mkewe kushiriki zinaa na mtu mwingine.

Katika ushirikiano usio wa mojakwamoja, hii ni pale ambapo mume au mke anamkuta mkewe au mumewe anazini au anataka kuzini lakini anaamua kumuacha tu anendelee kuzini na wala hachukui hatua zozote za kuzuia tendo lisifanyike. Huyu baada ya muda hawezi kuja kuiomba Mahakama itoe amri ya TALAKA wakati yeye akiruhusu mwenyewe uzinifu ufanyike.

Hivyo, unatakiwa kufahamu kuwa TALAKA inaweza kuwa ni haki yako lakini wakati mwingine haki hiyo unaweza ukaikosa kutokana na sababu mbalimbali zilizopo kwa mujibu wa sheria.

Mada hii ni ndefu sana lakini imesheheni vitu vingi vya muhimu. Hivyo kama umepata fursa ya kusoma makala hii yote tangu nilipoanza kuelezea hadi hapa nilipofikia sina shaka kuwa umeweza kujifunza mambo mengi sana muhimu na yatakayo kusaidia katika maisha yako. Hii ni kwasababu kuwa ndoa ni ibada na wengi wetu tumeshaoa au kuolewa, tutaoa au kuolewa au vinginevyo. Na changamoto zinazoweza kupelekea TALAKA pia zipo nyingi.

Lakini kabla hatujakimbilia katika TALAKA tujitahidi kwanza kumaliza tofauti zetu. Hata katika vitabu vya dini mfano biblia katika kitabu cha MARKO, 10: 4, 5 neno la Mungu linasema
10: 4. "Wakasema, Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya TALAKA na kumwacha"
Marko 10:5-9
10: 5. "Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii."

10:6. "Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke."

10:7. "Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe."

10:8. Na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja."

10: 9. "Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe."

KWAHIYO, kumbe kuachana sio mpango wa Mwenyezi Mungu bali ni kutokana na ugumu wa mioyo ya wanadamu imeruhusiwa kuachana kwa TALAKA.

Kwa leo naishia hapa. Mada hii imeandaliwa na kuletwa kwako nami mwanasheria na mwalimu wa maisha.
A Lawyer and LifeCoach
Mr George Francis.

Kama unataka kushare usiedit chochote, give me my credit.
Kwa maoni na ushauri usisite kunitafuta.
SIMU: 0713736006.
EMAIL: mr.georgefrancis21@gmail.com

Ahsante kwa kuendelea kujifunza.
IMG_20221028_074436_220.jpg
 
AbuuMaryam

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
2,341
4,102
Sheria za duniani zinajichanganya zenyewe kwa zenyewe tu...

Mara uzinifu ni sababu inayoweza kupelekea ukadai talaka mahakamani na ikatolewa... Wakati huo huo eti ukikaa muda mrefu bila kupeleka mahakamani ukaja kupeleka sio kosa tena...

Kwenye UISLAAM SHERIA ZAKE NI MNYOOFU.. MOJA NI MOJA... HAKUNA NYINGINE...
 
Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
112
95
Sheria za duniani zinajichanganya zenyewe kwa zenyewe tu...

Mara uzinifu ni sababu inayoweza kupelekea ukadai talaka mahakamani na ikatolewa... Wakati huo huo eti ukikaa muda mrefu bila kupeleka mahakamani ukaja kupeleka sio kosa tena...

Kwenye UISLAAM SHERIA ZAKE
 
Marashi

JF-Expert Member
Apr 14, 2018
2,744
4,108
Je baada ya talaka kutolewa, ni sharti mahari kurudishwa au ndo inakua imetoka?
Mfano mwanamke aliyeachwa kwa talaka akitolewa mahari upya.

Na iwe wanandoa hawakuzaa na waliishi pamoja miezi 6 na kutengana kisha talaka ikatolewa.
 
pye Chang shen

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
10,361
4,610
Kuna tofauti kuacha na kutoa talaka? Yaani nikimwambia mwananke nimekuacha inatosha au ni mpaka nimpe karatasi?
Kwa mujibu wa serikali, najua kwenye dini kutamka tu inatosha hayo mengine ni maonyesho tu
 
Atufigwegwe god

JF-Expert Member
Sep 24, 2018
1,506
1,931
Hivi mfano kwa walioishi bila ndoa kwa miaka labda kumi ,wakabahatika kupata watoto ,wakajenga nyumba, ikatokea mwanamke akawa na tabia zisizofaa,mwanaume akahamua amtimue, Je huyo mwanamke anaweza akaenda mahakamani au baraza la kata kufungua madai ya kugawana Mali?

Na je kwenye kugawana Mali kawaida inakuwa Ni % ngapi labda anastaili mwanamke,

Kuna kijana ana changamoto naona wanaenda mwishoni na mkewe, mkewe Ni kawa Malaya ,kwenye simu yake anachati na wanaume zaidi ya watatu, na wote inaonesha washamla, jamaa anasema wakilala kitandani mwanamke huwa analala na nguo,na jamaa akijaribu kumgusa anakuwa mkali,kiufupi hampi kabisa, na ikitokea kampa Basi kwa mbinde,

Na jamaa kwenye uchunguzi ndio amebaini mwanamke Ni Malaya haswaa, kingine mwanamke kutwa anashinda kwa shoga zake, nyumbani kupika Ni house girl,

Mwanamke kabila Ni mgogo, jamaa ni mnyamwezi,

Amenifuata leo kunieleza,maana Mimi ndio Kama mzee wake
 
Okays, Katika mgawanyo wa mali kila mtu ana haki yake. Hii haijalishi ni nani aliyetenda kosa lililopelekea kuachana.
Hivyo mwanamke ana haki kuja kufungua shauri la kudai mgawanyo wa mali.
Lakini kuhusu mgawanyo sio lazima owe 50% kwa 50%. Yeyote kati Yao anaweza akapata zaidi au pungufu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo sababu ya ufujaji wa mali za familia ulifanywa na mmoja wa wanandoa. Hii inaweza kusababisha apate mgao pungufu ya mwenzake.

Lakini yote kwa yote itategemea na utetezi wao utakaowasilishwa Mahakamani.
 
Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
112
95
Kuna tofauti kuacha na kutoa talaka? Yaani nikimwambia mwananke nimekuacha inatosha au ni mpaka nimpe karatasi?
Kwa mujibu wa serikali, najua kwenye dini kutamka tu inatosha hayo mengine ni maonyesho tu
Kuachana bila talaka tafsiri yake ni kwamba mmetengana, yaani mmeacha kuishi pamoja. Hapo mwanamke haruhusiwi kuolewa wala mwanaume kuoa mtu mwingine.

Kutengana kunaweza kuwa Kwa maneno kama mnavtofanya au kunaweza kuwa pia Kwa idhini ya Mahakama.

Lakini, talaka inamaanisha mmeachana jumla na hakuna lengo la kuja kurudiana tena. Hapa tunasema ndoa imevunjika lakini kuachana bila talaka ndoa inakuwa bado haijavunjika.

Mume au mke atapata nafasi ya kutuliza akili kisha baadae kuamua kurudiana au kuamua kudai talaka.

That's what I may respond to this question.
Ahsante.
 
Mulama

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
2,893
1,622
Kifungu 107 (2) (a) maana yake hakuna ndoa halali in dis kantri zote ni batiri kabsaa!
 
ngome1838

JF-Expert Member
Feb 20, 2019
1,959
2,291
FAHAMU kuhusu TALAKA na taratibu zake KISHERIA.

It's me
Mr George Francis
0713736006
mr.georgefrancis21@gmail.com

TALAKA ni ruhusa au amri ya kisheria inayotolewa na Mahakama pale ambapo mume au mke anataka kumwacha mwenzake. Hii ni hati inayoidhinisha kuvunjika kwa ndoa baina ya wanandoa.

Na ili tuseme ndoa imevunjika ni lazima talaka itolewe na ili TALAKA itolewe ni lazima Mahakama ijiridhishe kuwa ndoa hiyo imevunjika kiasi cha kutoweza kurekebishika yaani haiwezekani tena kwa wanandoa hao kuweza kuendelea na ndoa hiyo. Soma kifungu cha 99 cha Sheria ya Ndoa.

Kama hakuna TALAKA iliyotolewa lakini wanandoa wameacha kuishi tena pamoja, hapo tunasema wametengana tu lakini hawajaachana. Kutengana sio TALAKA. Kutengana ni hali ya mume na mke kuacha kuishi pamoja au kukaa mbalimbali. Kutengana kunaweza kuwa kwa mapatano kati ya wanandoa hao au kwa amri ya Mahakama. Mahakama itatoa amri hiyo endapo mmoja ya wanandoa atapeleka maombi Mahakamani.

Lengo la wanadoa kutengana ni kutaka kuwapa wanandoa hao muda wa kutafakari kama wanaweza kuendelea na ndoa hiyo au la. Baadae wanaweza kusameheana na kurudiana au kuishi tena pamoja. Lakini kuachana kwa TALAKA lengo ni kutokuwa na nia ya kutaka kurudiana tena kutokana na sababu zisizoweza kurekebishika.

Ukienda kusoma Mathayo 5 : 31 neno la Mungu linasema
"Imenenwa pia, mtu akimwacha mkewe na ampe hati ya TALAKA."
Kumbe TALAKA ni muhimu ili kuthibisha kuwa ndoa imevunjika na haipo tena. Baada ya TALAKA kutolewa, mume au mke atakuwa huru kuoa au kuolewa na mtu mwingine.

Join Telegram: TANZANIA LAWYERS FORUM 🎓

Chombo chenye mamlaka ya kutoa TALAKA ni Mahakama tu. Mahakama hiyo itatoa TALAKA kwa ndoa ambayo imedumu kwa miaka miwili au zaidi isipokuwa tu endapo mlalamikaji au mwombaji wa TALAKA ataoa sababu za msingi zitakazo onesha ugumu wa kuendelea kwa ndoa hiyo. Soma kifungu cha 100 (1)&(2) cha Sheria ya Ndoa.

Mwanandoa kabla ya kupeleka ombi au shauri la TALAKA Mahakamani, hatua ya kwanza anatakiwa kupeleka malalamiko kwenye Baraza la usuluhishi la ndoa yanayoanzishwa na waziri mwenye dhamana katika maswala ya ndoa takribani kila kata.

Mwanandoa anaweza kupeleka pia malalamiko yake katika mabaraza mengine yaliyoanzishwa katika jumuiya husika kwa dhumuni la kufanya kazi ya usuluhishi kama ilivyo katika Baraza la usuluhishi la ndoa. Soma kifungu cha 102(1)&(2) cha Sheria ya Ndoa.
Mfano kupeleka shauri katika ustawi wa jamii au mabaraza ya dini kama vile BAKWATA kwa waumini wa dini ya kiislamu au Kanisani katika mabaraza yanayohusiana na usuluhishi wa migogoro ya ndoa.

Baraza litasikiliza na endapo litashindwa kusuluhisha au kupata muafaka stahiki kati ya wanandoa hao basi Baraza litatoa cheti ambacho kitaonesha kuwa limeshindwa kusuluhisha mgogoro wa ndoa. Hapo sasa mwanadoa anaweza kupeleka shauri lake Mahakamani akiwa ametayarisha madai yake ya TALAKA.

Madai ya TALAKA yanatakiwa kuonesha mambo kama vile
✓Majina ya wanandoa
✓ Majina ya watoto, jinsia na umri wao
✓Sababu za kupeleka shauri hilo Mahakamani
✓Taarifa za mwenendo au kesi yoyote iliopita
✓Makubaliano yoyote kuhusiana na matunzo au mgawanyo wa mali za familia
✓Madai husika ya nini anataka kifanyike. Kuongeza maalifa soma kifungu cha 106(1)(a-g) cha Sheria ya Ndoa.

Maombi ya madai ya TALAKA yanatakiwa yaambatanishwe na hati iliyotolewa na Baraza la usuluishi ndani ya miezi sita kabla ya kupeleka shauri hilo la madai ya TALAKA Mahakamani. Hii ni Kwa mujibu wa vifungu vya 106(2) na 104(5) vya Sheria ya Ndoa.

Hati ya Baraza la usuluhishi haitahitajika endapo mambo yafuatayo yatathibitika
✓Mwombaji wa TALAKA alitelekezwa na hajui wapi alipo mwanandoa mwenzake.
✓Mlalamikiwa anaishi nje ya Tanzania na inaonekana kutokuwa na uwezekano wa kufika Mahakamani ndani ya miezi sita baada ya siku ambayo shauri husika limefikishwa Mahakamani.
✓Endapo mlalamikiwa alitakiwa kuhudhuria katika Baraza la usuluhishi lakini alishindwa kufika kwa makusudi.
✓Endapo mlalamikiwa amefungwa gerezani kifungo cha maisha au kwa kipindi cha miaka takribani mitano.
✓Endapo mlalamikaji atathibisha kwamba mlalamikiwa amepata ukichaa au ugonjwa wa akili usiotibika.
✓Endapo Mahakama itajiridhisha kuwa kuna sababu zilizo nje ya uwezo zinazopelekea hati ya Baraza la usuluhishi ishitajike.
Hii ni kwa mujibu wa vifungu vya 106(2) na 101(a-f) vya Sheria ya Ndoa.

Kutoa TALAKA sio kipaumbele cha Mahakama ndio maana sheria inasisitiza kesi za migogoro ya ndoa na TALAKA zianzie katika mabaraza ya usuluhishi ili kusudi wahusika waweze kusuluhishwa na kumaliza tofauti zao.

Mahakama haiwezi kuruhusu TALAKA pale ambapo mwombaji wa TALAKA ndiye mwenye makosa. Huwezi kupata haki juu ya makosa yako mwenyewe. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 107(1)(a) cha Sheria ya Ndoa.

Ni lazima pawepo na sababu ya msingi ili Mahakama iruhusu kutolewa kwa TALAKA. Ni lazima ndoa ionekane kuwa imevunjika kiasi cha kutoweza kurekebishika. Sababu zinazoweza kuthibitisha kuwa ndoa evunjika kiasi cha kutoweza kurekebishika ni kama hizi zifuatazo.
(a). Uzinzi uliopitiliza (adultery) - Hii ni zinaa inayofanywa kati ya mwanaume na mwanamke tofauti na mume au mke halali wa ndoa.
Kwa lugha nyingine tunasema ...
"Adultery - means a voluntary sexual intercourse between a married person and someone other than their lawful spouse.

Uzinifu unaweza kuwa sababu inayopelekea TALAKA. Hili sababu hii ya uzinifu iweze kukubaliwa ni lazima mlalamikiwa awe ameshiriki zinaa na mtu mwingine tofauti na mume au mke wake. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 107(2)(a) cha Sheria ya Ndoa.

Kufanya zinaa sio lazima kuwe na mwingiliano uliokamilika kati ya washiriki wa zinaa hiyo. Hatakama uume haujaingia vizuri kwenye uke bado itahesabika kuwa mwanaume au mwanamke anayelalamikiwa amefanya uzinzi.
Mfano: Kwenye kesi ya DENIS vs DENIS, Mahakama iliamua kwamba "any degree of penetration however slight will suffice."

Kwa mujibu wa kesi hii, mwanaume nawanamke wakifumaniwa wamelala pamoja itasemekana kuwa wamefanya uzinifu na ikumbukwe pia sio rahisi kupinga isipokuwa labda mwanaume huyo anayetuhumiwa kushiriki zinaa athibitike kuwa ni anisi (impotent), yaani uume wake hauna uwezo wa kusimama.

(TAHADHARI: Hii ni sheria ya ndoa, na hapa naelezea mambo ya ndoa, hivyo usijali kuhusu misamiati inayotumika. Kikubwa ni kukufanya uelewe na kuifurahia mada hii.

It's me
Mr George Francis
0713736006
mr.georgefrancis21@gmail.com

Endelea kusoma..

Sasa hili mlalamikiwa akutwe na hatia ya uzinzi ni lazima awe amefanya kitendo hicho kwa hiari yake. Hivyo basi, mwanamke aliyebakwa hatohesabika kuwa amefanya uzinzi. Hii ni kwasababu ameshiriki tendo la zinaa kwa kulazimishwa au pasipo hiari yake. Lakini jukumu la kuthibitisha kuwa kweli amebakwa na hakufanya kwa hiari yake lipo upande wake.

Mazingira yafuatayo yanaonesha kutendeka kwa kosa la uzinifu.
✓Kulala pamoja hotelini au gest house na mtu ambaye sio mume wala mke halali wa ndoa.
✓Kwenda katika madanguro
✓Kuishi uchumba na mtu mwingine
✓Kuzaa na mtu mwingine
✓Kuoa mtu mwingine wakati tiari upo kwenye ndoa inayoendelea. (Conviction of bigamy) na mazingira mengine yanayo endana na haya.

(b) Ukatili (Cruelty) - Hii ni hali ya kuumiza au kusababisha madhara kwa mtu mwingine. Ukatili unaweza kuwa ni wa kihisia au wa kudhuru mwili wa unaofanywa na mume au mke kwa mwenza wake au kwa watoto. Kutokana na vitendo vya ukatili Mahakama inaweza kutoa amri ya TALAKA na kuvunja ndoa. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 107(2)(c) cha Sheria ya Ndoa.

Lakini ikumbukwe kwamba katika maisha ya ndoa kupishana kauli, kugombana au kukwaruzana ni mambo yanyokubalika lakini mambo hayo yasivuke kiwango.
Mfano: kwenye kesi ya CHARLES AOKO vs DORINA GIBOGA, Mahakama iliamua kwamba
"matukio mawili ya kumpiga mwanamke hakuwezi kufanya ndoa ivunjike kiasi cha kushindwa kurekebishika. Hizo ndio raha na shida zenyewe katika ndoa."

Lakini katika kesi ya SAID MOHAMED vs ZENA ALLY, Mahakama iliamua kwamba
"kitendo cha mwanaume kumpiga mkewe na kumvua nguo zake mbele za watu na mbele za baba yake mkwe kilikuwa ni kitendo cha ukatili kilichopelekea madhara ya kimwili na kiakili."

Mambo yanayoashiria vitendo vya ukatili katika ndoa ni kama haya yafuatayo.
✓Ukatili wa kudhuru mwili
✓Ukatili wa kijinsia
✓Unyanyasaji au Ukatili wa kihisia
✓Vitisho na lugha za matusi
✓Kulazimisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile au kulawiti.

Hivyo, ukatili dhidi ya mke au mume unaweza kuwa ni sababu mojawapo inayoweza kuifanya Mahakama kutoa amri ya TALAKA.

(c). Kutekeleza au Uasi (Desertion). - Hii ni hali ya kutelekeza familia. Mume au mke ana haki ya kudai TALAKA endapo mume au mke wake ameamua kuiacha familia na kwenda kuishi mahala pengine kwa hiari yake mwenyewe bila sababu yoyote ya msingi kwa miaka agharau mitatu. Mahakama inaweza kutoa amri ya TALAKA endapo hilo litathibitishwa na mlalamikaji. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 107(2)(e) cha Sheria ya Ndoa.

Kunaweza kuwa na simple desertion yaani mume au mke kuamua kuacha kuishi pamoja na mwenza wake. Wakati mwingine wanaweza kuishi wote katika nyumba moja lakini mume au mke hataki kushirikiana chochote na mwenza wake.

Lakini pia kunaweza kuwa na constructive desertion, ambako mume au mke anaweza kufanya matendo ambayo yanaweza kumsababisha mwenza wake aondoke hapo nyumbani. Kama wewe ndio umekuwa chanzo cha mume au mke wako kuchukua maamuzi ya kuondoka huwezi kuibuka na kudai TALAKA kanakwamba mwenye kosa sio wewe.
Huwezi kudai TALAKA chini ya sababu hii kama wewe ndio sababu ya mume au mke wako kuacha familia na kuondoka. Lakini unaweza kudai TALAKA kama wewe ndiye uliyeondoka kutokana na sababu zisizoweza kuvumilika zilizofanywa na mume au mke wako. Mfano, kutishiwa kuuwawa, vipigo vya malakwamala na mambo mengine kama hayo.
Hivyo, inatakiwa mtu awe ametelekeza familia kwa miaka angharau mitatu na iwe amefanya hivyo kwa hiari yake mwenyewe.

(d). Kifungo cha jela - mume au mke anaweza kuomba Mahakama itoe amri ya TALAKA, endapo mume au mke wake amefungwa kifungo cha maisha jela au kifungo kisichopungua miaka mitano. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 107(2)(g) cha Sheria ya Ndoa.

(e). Ukichaa au ugonjwa wa akili.
Hii ni hali ya kutokuwa na akili timamu kulikothibitishwa na madaktari bingwa wa akili. Madaktari bingwa hao ni lazima wathibitishe kuwa hakuna matumaini ya kupata nafuu au kupona. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 107(2)(h) cha Sheria ya Ndoa.

KWA UJUMLA, sababu zipo nyingi hizi ni baadhi tu ya sababu ambazo endapo zitathibitika na kwa kuzingatia na ushahidi pamoja na mazingira mengine, basi Mahakama inaweza kutoa amri ya TALAKA kama ilivyoombwa na mmoja kati ya wanandoa husika.

It's me
Mr George Francis
0713736006
mr.georgefrancis21@gmail.com

MUHIMU
Kama kawaida kila jambo lina mipaka yake. Hivyo hata katika utoaji wa TALAKA pia kuna mipaka. Kuna sababu ambazo zinaweza kuifanya Mahakama isikubali kutoa amri ya TALAKA. Sababu hizo ni kama hizi zifuatazo.
(i). Kama mwombaji wa TALAKA ndiye mwenye makosa. Hivyo, huwezi kunufaika kwa makosa yako mwenyewe. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 107(1)(a).
Mfano: Katika kesi ya ATHANAS MAKINGWA vs DARIN HASSAN, Mahakama ilisema kwamba
"Kama kosa ni la mwenyewe anayeomba TALAKA bila sababu maalumu, amri ya TALAKA haitatolewa."

(ii). Kula njama (collusion). - Hiki ni kitendo cha wanandoa kula njama ya kuidanganya Mahakama. Kutokana na sababu hii Mahakama itatupilia mbali madai ya TALAKA yaliyowasilishwa Mahakamani. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 87 cha Sheria ya Ndoa.

Hiki ni kitendo ambacho wanandoa wamekubaliana kuficha ukweli au kutoeleza ukweli wote mbele ya Mahakama. Hapa hawatoi maelezo yenye kusaidia kubaini ukweli wa tatizo lao au kuzalisha story za uongo ilimradi tu Mahakama ikubali kutoa amri ya TALAKA. Hivyo basi, kutokana na sababu hii Mahakama haitakubali kutoa amri ya TALAKA.

(iii). Kupuuza au kusamehe au kujifanya kutoona. (Condonation). Hii ni hali ambayo mume au mke kupuuzia kosa ambalo limetendwa na mke au mume wake. Mahakama haitakubali kutoa amri ya TALAKA kama ikigundua kuwa mume au mke alionesha kuvumilia au kupuuza kosa lililowahi kufanywa na mke au mume wake. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 86 cha Sheria ya Ndoa.

Viashiria vinavyoonesha kuwepo kwa hali hii ya kupuuza makosa ni kama hivi vifuatavyo.
✓Kujua kosa lililotendeka
✓ Kusamehe kwa kutoamua kuchukua hatua
✓Kuonesha kuwa kosa hilo linavumilika.
Mfano: kwenye kesi ya MARIAM TUMBO vs HAROLD TUMBO,
"Mwanaume alifanya uzinifu kwa kwenda kuishi na mwanamke mwingine. Mkewe wa ndoa alijua lakini hakuchukua hatua zozote. Hivyo, Mahakama iliamua kuwepo kwa hali ya kuvumilika na haikutoa amri ya TALAKA. Mke halali wa ndoa katika kesi hii alijua kuwa mume wake anaishi pia na mwanamke mwingine kwa miaka minne lakini alivumilia na hakuchukua hatua zozote. Bada ya miaka minne ndio akapeleka shauri Mahakamani akidai kupewa TALAKA kwa kosa ambalo aliweza kulivulia kwa miaka minne. Mahakama iliona kuwa kama aliweza kupuuza kwa miaka yote hiyo minne basi kosa hilo linavumilika, hivyo haikutoa amri ya TALAKA.

(iv). Ushirikiano katika kutenda kosa. (Connivance). Hii ni hali ya wanandoa wenyewe kushirikiana katika kuruhusu uzinifu. Mahakama haiwezi kuridhia kutoa amri ya TALAKA kwasababu wahusika wote wawili wameshirikiana katika kuruhusu uzinifu kati yao. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 85 cha Sheria ya Ndoa.

Hapa kuna
~ushirikiano wa mojakwamoja (active connivance) na

~ushirikiano usio wa mojai (passive connivance.)

Mfano hai ni katika kesi ya RICHMOND vs RICHMOND,
"ambapo watu wawili waliopo kwenye ndoa walikubaliana kubadirishana wanawake" hapa huwezi kuja kudai Mahakama itoe amri ya TALAKA kwa kosa la uzinifu wakati mlalamikaji amekubali mwenyewe mkewe kushiriki zinaa na mtu mwingine.Hivyo, unatakiwa kufahamu kuwa TALAKA inaweza kuwa ni haki yako lakini wakati mwingine haki hiyo unaweza ukaikosa kutokana na sababu mbalimbali zilizopo kwa mujibu wa sheria.

Mada hii ni ndefu sana lakini imesheheni vitu vingi vya muhimu. Hivyo kama umepata fursa ya kusoma makala hii yote tangu nilipoanza kuelezea hadi hapa nilipofikia sina shaka kuwa umeweza kujifunza mambo mengi sana muhimu na yatakayo kusaidia katika maisha yako. Hii ni kwasababu kuwa ndoa ni ibada na wengi wetu tumeshaoa au kuolewa, tutaoa au kuolewa au vinginevyo. Na changamoto zinazoweza kupelekea TALAKA pia zipo nyingi.

Lakini kabla hatujakimbilia katika TALAKA tujitahidi kwanza kumaliza tofauti zetu. Hata katika vitabu vya dini mfano biblia katika kitabu cha MARKO, 10: 4, 5 neno la Mungu linasema
10: 4. "Wakasema, Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya TALAKA na kumwacha"
Marko 10:5-9
10: 5. "Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii."

10:6. "Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke."

10:7. "Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe."

10:8. Na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja."

10: 9. "Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe."

KWAHIYO, kumbe kuachana sio mpango wa Mwenyezi Mungu bali ni kutokana na ugumu wa mioyo ya wanadamu imeruhusiwa kuachana kwa TALAKA.

Kwa leo naishia hapa. Mada hii imeandaliwa na kuletwa kwako nami mwanasheria na mwalimu wa maisha.
A Lawyer and LifeCoach
Mr George Francis.

Kama unataka kushare usiedit chochote, give me my credit.
Kwa maoni na ushauri usisite kunitafuta.
SIMU: 0713736006.
EMAIL: mr.georgefrancis21@gmail.com

Ahsante kwa kuendelea kujifunza.
View attachment 2400256
Itakuwaje endapo kanisa likakataa kujaza fomu iliyotoka mahakamani kwa kisingizio cha kutaka wenza warudiane? Ogopa sana kufunga ndoa za kikristo hasa wakatoliki na walutheri.Haya madhehebu ni wakatili sana na wakolini hakuna mfano
 
Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
112
95
Itakuwaje endapo kanisa likakataa kujaza fomu iliyotoka mahakamani kwa kisingizio cha kutaka wenza warudiane? Ogopa sana kufunga ndoa za kikristo hasa wakatoliki na walutheri.Haya madhehebu ni wakatili sana na wakolini hakuna mfano
Ndoa ni maridhiano kati ya mke na mume, kama Mahakama imeidhinisha TALAKA hakuna wa kuzuia hili lisifanyike.
 
ngome1838

JF-Expert Member
Feb 20, 2019
1,959
2,291
Ndoa ni maridhiano kati ya mke na mume, kama Mahakama imeidhinisha TALAKA hakuna wa kuzuia hili lisifanyike.
Talaka za dini za kikristo, muombaji anapewa fomu aipeleke kanisani kwake kule ndio kimbembe.Hawajazi ni usumbufu mwanzo mwisho wakijifanya wanakaa vikao vya usuluhishi na wakilazimisha suluhu wakati mmoja anaumia
 
6 Reactions
Reply
Top Bottom