Siku yangu inavyomalizika kwa bahati

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
6,803
12,660
Habari ya mchana,

Mwaka huu mwezi wa 1 niliingia JamiiForums. Nilikuta uzi jamaa mmoja ameuanzisha unaosema


Je, kuna jambo lolote ambalo hutalisahau mwaka huu 2020 ambalo limekutokea sasa!

Kila mtu ali-share jambo lake ,mimi nilishea jambo langu pia, kwa faida ya ambao hawakusoma ule uzi nilishea hivi

2020

18 September 2020 majira ya saa 5 asubuhi, nikiwa kazini kwangu alikuja mdada wa umri wa miaka 22(sitamtaja jina) alikuja akiwa na lengo la kutoa mimba. Ukweli sikupendezwa na hiko kitendo ukitegemea niliwahi kuapa sitafanya hilo jambo katika taaluma yangu mpaka mwisho wa pumzi zangu, lakini ikabidi nimuhoji kwanini amefika hatua ile ya kutaka kutoa mimba.

Dada alianza kueleza yeye kwao ni Makambako alikuja Dar akiwa na umri wa miaka 14 kwa ajili ya kazi za ndani, baada ya kufanya kazi kwa mwaka mmoja Boss wake alikua mkarimu sana kiasi alimchukulia kama binti yake hapo basi akamtafutia sehemu ya kujifunza ushonaji na baada ya muda kwa kua binti alikua muislam na boss ni mkristu, bint alimuomba ampeleke madrassa ili asome dini yake.

Boss alikubali na akampeleka alisoma madrassa kwa mwaka mmoja huko huko akapata Mwanaume wa kumuoa alipofikisha miaka 17 akaolewa, boss kwa kushirikiana na ndugu zake akamuozesha. Maisha ya ndoa yalikua magumu kwa jambo moja yule bwana alikua mlevi sana japo alimjali kwa kila kituila dosari ilikua ulevi na baadae akaanza mambo ya kumpiga, baada ya kuishi kwa miaka 2 ndani ya ndoa walipata mtoto wa kike.

Siku moja alikua ameenda mjini aliporudi alikuta mwanaume amehamisha kila kitu kwenye chumba walichokua wanakaa na mbaya zaidi alikuta talaka ikiwa imeshaandikwa na hakujua mahala yule mwanaume alipoelekea na ukizingatia hata mwenye nyumba alijua tu wanahama na mkewe japo kodi yao ilikua imebaki miezi 5 kuisha, pigo lingine ilikua yule boss wake alihamia Mwanza miezi 6 tu tangu alipoolewa hivyo kwa Dar akawa hana ndugu.

Mama mwenye nyumba akamwambia akae tu pale alimpa msaada wa kumpa godoro dogo na maisha yalianzia hapo, maisha yakawa magumu kwakuwa hakua na kipato na kazi hana kula yake ikawa ya tabu na baada ya muda alipata kibarua cha kuuza maji kwa mama mmoja na malipo yalikua 2500 kwa siku kazi ilikua ngumu sana kwake lakini hakua na chaguo ukizingatia alikua na mtoto mdogo baada ya kuhangaika sana kwa muda mrefu kuna kipindi mtoto wake aliugua hivyo akijikuta akitumia pesa ndogo kumtibia. Akajikuta anadaiwa kodi ya miezi 7 katika nyumba akawa na hofu kubwa ya kufukuzwa lakini Mama mwenye nyumba wala hakua akipiga kelele.

Mwaka 2020 February mama mwenye nyumba alifiwa na baba yake hivyo alisafiri kwenda kwao kigoma alikaa huko miezi 2..huku nyuma alikosa msaada siku moja wakati anatembeza maji alikutana na bodaboda aliyekua amemzoea sana akamwambia shida yake kua anaumwa na hana pesa yakwenda hospital anaomba amkopeshe hela na angemlipa kidogo kidogo. Yule boda boda alikubali lakini kwa sharti moja alale nae na angempa elfu 30 bila kutaka kurejeshewa. Alikubali na wakaenda kulala lakini baada ya tendo asubuhi alipewa elfu 10 na alipohoji jamaa akamwambia kubali uwe mpenzi wangu nitakuhudumia.

Mwanamke alikubali lakini ndani ya wiki moja aligundua mwanaume alikua malaya sana hivyo akaomba waachane baada ya kumfumania mara mbili, jamaa kwa nyodo akasema sawa baada ya mwezi aliona mabadiliko na baada ya kupima akajikuta mjamzito alipomfuata jamaa alikataa akasema sina mpango wa mtoto chukua 10 ukanunue vidonge utoe. Kweli yule bint akaenda kutafuta vidonge(Misoprostal) akapata kwa elfu 15 akaweka lakini aliona damu kidogo sana akajua imetoka akendelea mambo mengine lakini baada ya miezi miwili akaona bado tumbo linakua na haelewi..alipopima tena akakuta bado mjamzito akazidi changanyikiwa akamfuata tena mwenye mimba yake.

Jamaa yule alimkana kua hamjui kwani alishampa hela ya kutoa na alishamwambia imetoka hivyo akamtafute mwenye hiyo mimba,aliendelea kumsumbua mpaka jamaa siku moja akampiga na jamaa kuhama kijiwe na mtaa. Alijaribu majaribio mengi ya kutaka kuitoa lakini ikashindikana hivyo alijichanga na ilipofika elfu 18 akaja kituoni ninapofanya kazi kujaribu. Aliponieleza hayo nikamuhurumia lakini bado sikumuamini nikamwambia mimi sitoi mimba na hapa haturuhusu kutoa mimba na kwakua umejaribu kuitoa hiyo mimba bila mafanikio usiitoe fanya uzae. Alibembeleza sana ila nikasimamia msimamo wangu. Nilimpa elfu 5 kumuongezea pesa akaondoka.

Baada ya siku nne akarudi tena akiwa analia nimsaidie hana ndugu na maisha yanazidi kua magumu ana mtoto mdogo na bado mimba inamsumbua kisha hata kazi zake za kuuza maji za juani ni ngumu kuzurula, nikamwambia tena siwezi kufanya hilo jambo..nikamuuliza tena kipato chako kwa siku sh ngapi? Akasema 2500 ndo anayolipwa nikamwambia basi aache kutembeza maji mimi nitakua ninampa kila wiki elfu 30 kama pesa ya kujikimu, ikiwemo na kumlipia kodi, hapo akakubali nikaanza kumchunguza kidogo kidogo nikakuta kweli ana maisha magumu kuliko yale aliyonihadithia nikamuanzisha clinic kituoni kwetu ila jambo nina hofu nalo ameandika jina langu la kwanza kama jina la baba(na nilipohoji akanambia kwake ni kama shukrani na kwa kuwa mtoto hana baba basi jina langu lingefaa).

Mwezi wa kumi na moja zilinyesha mvua nyingi nyumba anayoishi iliporomoka akawa hana pa kukaa nikamshauri aende kwao akajifungulie na kipindi hiko chote mama yake na ndugu zake niliwasiliana nao wakiwa huko kijijini na wanajua yote, na sikuona busara akajifungulie huko maana najua changamoto zake, ila baada ya changamoto ya makazi ikabidi nimsafirishe hadi kwao na imebaki kumuhudumia kila ninapoweza.

Kufupisha stori. Jambo hili ndugu zangu staff wenzangu na marafiki wengine wanajua ila sijawahi mwambia mpenzi wangu kwakua yuko mbali ila akirudi nitamueleza kila kitu. Nilishangaa kujikuta tu nafanya yote hayo lakini nina furaha nimeokoa maisha ya yule mtoto na tunatarajia mwezi huu ajifungue salama. Sijui ni kwa vipi itakuaje kuhusu baba yake mtoto lakini mimi kwa kiasi fulani najisikia amani nimetimiza majukumu yangu na huko alipo nadhani baada ya kujifungua atamlea vyema na nitatoa msaada kadri ninavyoweza japo sina kipato kikubwa.

Yapo mambo mengi yaliyotokea kwa mwaka 2020 lakini hili ndo jambo la kwanza nimelipa uzito mkubwa sana.

NB: Sijasimulia kisa hiki kujisifu ila nimeona nishee nanyi ndugu zangu wa humu ili kama kuna mahala nimekosea nielezwe na pia kutoa angalizo kwa wanaume wanaokataa mimba zao ni wanasababisha matatizo makubwa sana kwa wasichana.

#Ndefu ila tuvumiliane

Leo 27/01/2021

Niliamka nikiwa mchovu sana kwakua wiki nzima nalala saa 6 na kuamka saa 11 alfajir ,leo nilipata nafasi ya kulala mpaka saa 3 asubuhi. Nimeamka sikua na dk wala sms kwenye simu yangu siku ilianza kwa kuboa kiukweli nikakumbuka natakiwa kwenda serikali ya mitaa ili wakanijazie fomu zangu kuna mahala nahitaji kufungua duka la dawa, nikajianda nikafika sehemu husika nikakuta ukiritimba sikufanikiwa kujaziwa masharti yalikua kibao na hela juu walikua wanataka, nikakubaliana na M/Kiti nitarudi J3. Nikiwa njiani narudi nilijikwaa sehemu mpaka nikakaa chini kwa maumivu. Nikaona heri nirudi nyumbani nitatoka jioni.

Nikafika home saa 5 na dk 24 asubuhi nikaona nilale. Nimekuja kuamshwa na simu saa 8 na dk 11 mchana mpigaji ni nani? Alikua ni binti aliyebeba ule ujauzito anaongea kwa furaha huku akilia "Feyzal tumepata mtoto wa kike, M/Mungu ni mwema nimefurahi sana kunivusha salama"

Baada ya hayo maneno Moyo wangu ulijawahi na furaha na machozi ya mbali yalinilenga hakika nimefurahi M/Mungu amenipa mtoto leo, hakika Mungu ni mwema. Nimeshajiandaa nampitia mama yangu ili twende tukamuone mtoto. Naombeni jina la kike zuri kwa ajili ya binti yangu tafadhali.

#There is no victory without history
 
Dah Ubarikiwe kwa moyo wa utu mkuu!

Mtoto amepatikana unayemuita 'wako' na ndugu zako akiwemo mama mnafuraha mnoo.. na mnaenda kumwona mtoto 'wenu' sawa lakini NAIONA DHAHAMA MBELE YAKO, WEWE NA HUYO MPENZI WAKO ALIYEMBALI Mwenyezi Mungu akusimamie!
 
Asante sana!! Nina furaha sana na kwakua wiki iliyopita nilimrudisha Dar na yupo kwa sista yangu kazi imekua rahisi, nipo kwenye usafiri Kila mmoja ana furaha Mama amefurahi zaidi.
Sijui kwanini stori yako imenigusa! So sad but hongera mkuu kuwa na humanity personality.. chagua jina we mwenyewe mkuu.
 
Dah kuna watu Mungu akwaleta duniani kusaidia watu, mkuu Mungu atauongezea sana. Utapokea sana, nahisi kuna nguvu ya kutoa, mimi uwa nikitoa napata sana ila kuna muda mwingine roho ya kutoa inakuwa ngumu sana yani.

Hongera sana. Kuna jamaa yangu mmoja alinifundisha kutoa, kuna kipindi nilikuwa nina matatizo, msaada alionipa sitokaa niusahau, maana alinipa msaada ambao labda ni wazazi wanaweza kukupa maana kwa kipindi hicho na mpaka sasa sidhani kama mimi naweza kumpa msaada huo mtu.

Lakini mambo yamemchenjia now hayuko sawa, leo nimejikuta namtumia pesa from no where baadaye nikampigia nikamuuliza umeona sms, akanijibu sijasoma sms nilikwua busy kidogo. Basi nikakata simu, baadae kanitumia sms anasnishukuru sana sana.

Kitu ambacho yeye hajui ni kwamba msaada alionipa three years ago, kipindi ambapo karibia kila aliyekuwa karibu yangu was mocking me sijawahi kuusahau mpaka leo huenda yeye ameshasahau.
Wema hauozi mkuu keep it up. Umewekeza.
 
Dah Ubarikiwe kwa moyo wa utu mkuu!

Mtoto amepatikana unayemuita 'wako' na ndugu zako akiwemo mama mnafuraha mnoo.. na mnaenda kumwona mtoto 'wenu' sawa lakini NAIONA DHAHAMA MBELE YAKO, WEWE NA HUYO MPENZI WAKO ALIYEMBALI Mwenyezi Mungu akusimamie!
Mkuu mpenzi wangu hajui ila anakuja mwezi ujao likizo nitamueleza kila kitu...Mama ndiye alinishauri nimrudishe Dar ili ajifungulie huku hivyo anaweza kua msaada kumueleza Mpenzi wangu maana anajulikana na ni Mwanamke smart sana....anapita humu Jf najua leo akisoma huu uzi atahisi kitu kama kweli amenifuatilia leo.
 
Mkuu ni kweli...hongera sana.
Dah kuna watu Mungu akwaleta duniani kusaidia watu, mkuu Mungu atauongezea sana. Utapokea sana, nahisi kuna nguvu ya kutoa, mimi uwa nikitoa napata sana ila kuna muda mwingine roho ya kutoa inakuwa ngumu sana yani...
 
hakika nimefurahi M/Mungu amenipa mtoto leo, hakika Mungu ni mwema. Nimeshajiandaa nampitia mama yangu ili twende tukamuone mtoto. Naombeni jina la kike zuri kwa ajili ya binti yangu tafadhali.
hapa ndio umenichanganya mkuu
 
Hongera sana kwa kusaidia bila kuomba tunda kimasihara,.

Baadhi ya wanaume huwa tunazingua Sana yani, masingle maza wanapitiaga wakat mgumu Sana na chanzo ni sisi wanaume alaf badae tunawasema vbaya inaskitisha mnoo.japo Wengine huwa wanajitakia wenyewe.

ila kwa mujibu wa iman tunaambiwa wema hauozi na ubaya hausahauliki vile utakavyo fanya ndivyo utakavyo lipwa.

Hongera kwa kumpa msaada huyo dada
 
Dah kuna watu Mungu akwaleta duniani kusaidia watu, mkuu Mungu atauongezea sana. Utapokea sana, nahisi kuna nguvu ya kutoa, mimi uwa nikitoa napata sana ila kuna muda mwingine roho ya kutoa inakuwa ngumu sana yani.

Hongera sana. Kuna jamaa yangu mmoja alinifundisha kutoa, kuna kipindi nilikuwa nina matatizo, msaada alionipa sitokaa niusahau, maana alinipa msaada ambao labda ni wazazi wanaweza kukupa maana kwa kipindi hicho na mpaka sasa sidhani kama mimi naweza kumpa msaada huo mtu.

Lakini mambo yamemchenjia now hayuko sawa, leo nimejikuta namtumia pesa from no where baadaye nikampigia nikamuuliza umeona sms, akanijibu sijasoma sms nilikwua busy kidogo. Basi nikakata simu, baadae kanitumia sms anasnishukuru sana sana.

Kitu ambacho yeye hajui ni kwamba msaada alionipa three years ago, kipindi ambapo karibia kila aliyekuwa karibu yangu was mocking me sijawahi kuusahau mpaka leo huenda yeye ameshasahau.
Wema hauozi mkuu keep it up. Umewekeza.

Wema hauozi mkuu, itabakia hivyo mpaka Yesu anarudi.
 
Back
Top Bottom